Alininyanyasa sana nilipofukuzwa kazi, MUNGU ameniona, sasa yamegeuka

Mkuu Mimi nakushauri usimwache Mkeo! Maadamu amekuangukia na kukupigia magoti Msamehe na endelea naye kwa mstakabali wa watoto wako.Watoto ni Muhimu zaidi kuliko kitu kingine,wao hawajui kitu lakini kwao HAKUNA KAMA Mama!
Pia Fahamu kuwa ASILIMIA KUBWA ya Wanawake ndivyo walivyo.Hata kama utamwacha na kumchukua mwingine,siku mambo yakikuharibikia mfano umekosa kazi hata huyo Mwingine anaweza kukufanyia vituko na kukuacha vile vile.
Ni viumbe dhaifu kabisa katika maswala ya ndoa.
Pili fahamu kwa kizazi chetu hiki ASILIMIA KUBWA ya Wanawake wanaolewa na PESA na Vitu alivyonavyo Mwanaume hawaolewi na MWANAMME SURUALI.Kwa hiyo vikiondoka vitu hivyo ndipo utakapowajua!
Mkuu ushauri wangu tena,kwa kuwa Mungu amekubariki akakupa kazi na huenda atakuongezea zaidi,USIMWACHE MKEO!
 
christo devries Kuna wakati binadamu anatawaliwa na shetani hadi anasahau wema wa mungu katika maisha yake... Naamini hali iliyokukuta imekufanya kutaka lau kulipa kisasi japo kumkomoa mhusika ili roho yako iridhike na uwe huru utumwani.....Kwa maelezo yako nahisi bado una chembechembe za upendo kwa mkeo hata kama unaunganishwa na watoto.

Wanawake wote wanafanana na mkeo katika majibu ya kihasara japo katika mazingira tofauti. Ukiniuliza mimi nitakuambia mkeo alifanya hivyo kama sehemu ya kukupa changamoto za wewe kutafuta kazi au kujishika katika biashara...Inawezekana ulipouza magari uliigiza maisha yale ya zamani bila kujua hela uliyo nayo ni fixed na mkeo hakupata nafasi ya kukushauri kwa sababu ulishahisi hakupendi na hakujali tena.... Wanaume tulio wengi tunakumbwa na haka kamdudu ka kutojiamini na hata kujihisi vibaya na wakati mwingine kujawa na hasira pale tunaposhuka kipato kutoka kwa wake zetu.....

USHAURI Mkeo bado anafaa kuwa mke na tena akawa bora kuliko zamani, huyu ni mropokaji na mwenye kujidai japo kwa kutaka uchakarike, wapo wale washirikina na wasiopenda maendeleo ya waume zao. Rudi kwa mkeo ukiwa kama baba, mme na rafiki kisha umweleze yote uliyoandika hapa na nyongeza kama unazo na usisahau kumwambia ni kwa jinsi gani ulighadhifika na hata kuahidi kutoishi nae tena.

Baaada ya hapo atakuomba msamaha mkiwa wawili then umpe mahitaji yako kwake kama sehemu ya kitubio chake na umwahidi kurudisha mahusiano yaliyoharibika kati yake na ndugu zako kwani nionavyo mimi wewe ndiye daraja lililovunjika. Ushuhuda kuna jamaa yangu aliambiwa na wazazi, ndugu na familia mkewe ni mbaya na wakamsaidia kumtalaka ila my friend cha kwanza ni cha kwanza ameoa mke mwingine yaani sijui nikyeleze lipi ila sasa amebaki yatima wa ndugu kwani amemkosanisha na marafiki, wazazi na ndugu wote na amebaki njia panda huku ndugu wakimshauri amwache na amrudie wa kwanza huku ikiwa tayari jioni

Hitimisho
Ujumbe ni mrefu sana ila ungeniuliza umemaliza ningekujibu hapana...Ukiona nashauri jema na ukahitaji msaada zaidi niPM sitoshindwa kukushauri lililo jema kwako. "Ishini na hao wanawake kwa akili" "Na ukiona maisha ya ndoa huyawezi na ni bora usioe kabisa" Kuna maana kubwa hapa kaka.
usimudanganye bana,, huyo hafai kuwa mke mzee baba,,labda ungeshauli kuwa km nikumusamahe amueamehe tu ila asiish nae tena;huyo yupo kimasrahi kwake!!chukua tano zako na yy vile vile,, yan hapi ili waish kwa aman ni lazima huyo bwana awe not mda ote
 
Mkuu Mimi nakushauri usimwache Mkeo! Maadamu amekuangukia na kukupigia magoti Msamehe na endelea naye kwa mstakabali wa watoto wako.Watoto ni Muhimu zaidi kuliko kitu kingine,wao hawajui kitu lakini kwao HAKUNA KAMA Mama!
Pia Fahamu kuwa ASILIMIA KUBWA ya Wanawake ndivyo walivyo.Hata kama utamwacha na kumchukua mwingine,siku mambo yakikuharibikia mfano umekosa kazi hata huyo Mwingine anaweza kukufanyia vituko na kukuacha vile vile.
Ni viumbe dhaifu kabisa katika maswala ya ndoa.
Pili fahamu kwa kizazi chetu hiki ASILIMIA KUBWA ya Wanawake wanaolewa na PESA na Vitu alivyonavyo Mwanaume hawaolewi na MWANAMME SURUALI.Kwa hiyo vikiondoka vitu hivyo ndipo utakapowajua!
Mkuu ushauri wangu tena,kwa kuwa Mungu amekubariki akakupa kazi na huenda atakuongezea zaidi,USIMWACHE MKEO!
Huu ni ushauri wa hovyo kabisa kuwahi kutokea hapa Jf, hadi nimekukasirikia na nimekublock kabisa.....☹️
 
Wazazi wangu hawataki kusikia kabisa neno msamahakwa matendo aliyotufanyia.
Ungana na wazazi wako, Anza maisha mapya, Yenye furaha na amani.

Songa mbele na mipango yako.

Endelea kutoa huduma kwa watoto wako kama ufanyavyo sasa.

Maisha ni furaha na amani katika nafsi yako, umeshndwa kupata furaha na amani ya nafsi toka kwa mke wako.

Huyo mke hakufai.

---
Uzi wa 2015, leo ndio nimeuona
 
Siku moja nisiyopenda kuikumbuka nilitwa ofisini kwa bosi wangu na kukabidhiwa barua ya kufukuzwa kazi
Hiyo ilikua ni baada ya uchunguzi wa miezi kdhaa wa kosa nililokua nimelifanya bahati mbaya. Miezi mitatu nyuma nilimuingizia pesa mteja kimakosa kwenye akaunti yake kiasi cha million mia tatu na hamsini ambazo alitakiwa kuwekewa Mteja mwingine halali kupata pesa hizo.

Kama humu ndani Kuna banker ataelewa nachokisema, kwamba makosa kama haya benki ni kawaida sana. Ukigundua kosa kama hili unawahi una reverse hiyo entry una m-credit anaetakiwa shida ni kama uliemwekea kimakosa akawahi kuzichukua ndipo yanakukuta yaliyonikuta mimi.

Baada ya kufukuzwa kazi mke wangu alibadilika kabisa
Nilishuhudia yafuatayo:-

(1) Alitamka mimi ni mjinga ndio maana nimefukuzwa kazi.

(2) Chake kikawa chake tu.

(3) Akawa anawaambia wazi watoto kuwa kitu fulani kimenunuliwa na yeye na sio mimi.

(4) Muda wa kurudi home ukabadilika sasa anarudi usiku mwingi, nampa kipigo cha nguvu anazira na kukimbilia kwao, kwenye usuluhishi anawaambia wasuluhishi kwamba mimi namuonea wivu kwa kuwa ana kazi mimi sina.

(5) Niliuza Gari zangu mbili ili nipate mtaji wa kufanya biashara hivyo nikawa sina Gari nilijua maadam wife ana Gari tutatumia wote maana hata yeye wakati hana Gari alikua akitumia magari yangu.

Kinyume na matarajio hakutaka kabisa niguse Gari lake mimi nikawa mtu wa miguu.Majirani wakawa wanashangaa mfumo wetu wa maisha.

(6) Life yetu ya bedroom ikawa imekufa no intimacy no love making nothing. Alianza kidogo kidogo leo mara aseme anaumwa, kesho kachoka, hadi mwezi unaisha. Nikaamua isiwe tabu nikaacha kuulizia tena, nae akawa amepotezea moja kwa moja.

Hata wazazi wangu aliwa mistreat sana wakawa hawaji tena kwangu, mama yangu akawa ananitumia vitu kwa njia basi kutoka nyumbani kama mchele, maharage, unga na kadhalika ili na mm nionekane nachangia.Wakuu siku ya kufa nyani miti yote huteleza. Kila nilichojaribu kukifanya ili nijinasue kinakwama, nakuta mtaji wote unakata naanza moja.Ilikatika miaka minne nikiwa kwenye hali hii maana nilipata matatizo 2010. Mwaka Jana kuna Dada mmoja tulisoma wote primary school akaamua kunisaidia, huyu dada tulikutana Posta accidentally tukapeana contact
mimi nilishamsahau ila yeye alinikumbuka.

Baadae akaniunganisha na mumewe ambae ni HR manager kwenye shirika fulani, nikamwelezea ukweli wote na akaniingiza kaziniWife sikumwambia kuwa nimepata kazi akaanza kuona nakuja na mahitaji ndani, nikawa naondoka zangu alfajiri narudi usiku mwingi. Nikaita mafundi wakabomoa ukuta wote wa fensi uliokua umeoza waliiba sana cement wakati wa ujenzi ukajengwa upya, vitu vyote vilivyochoka ndani nikabadilisha. Wife alishangaa sana ila akashindwa kuniuliza maana hadi hapo tulikua hatuongeleshani zaidi ya salam za asubuhi na jioni tu basi.

Wana jf siwezi kuwaficha sehemu niliyopata naingiza hela Mara kumi ya ile kazi yangu ya benki, hii sikutokana na mshahara bali njia mbali mbali katikati ya mwezi kitengo chetu tupo wanne,hali ikiwa nzuri huwa tunagawana hadi laki mbili kila siku, kama hali ni mbaya tunagawana laki moja kwa siku hii ni mbali na ile tunayogawana mwisho wa mwezi kama million 3 each person mshahara ni mdogo tu ni laki saba tu kwa mwezi.Maana mshikaji alisema anaweza kuniingiza kazini ila kama mfanyakazi wa kawaida kwa kuwa benki nilifukuzwa hakukua na reference wala background check so nikaamua kufuta kwenye CV kuwa nilifanya bank.

Nimeanza mchakato wa talaka kupitia mwanasheria mmoja rafiki yangu, mwezi January mwaka huu amemwandikia barua ya kumtaarifu uamuzi huo na copy Ustawi wa jamii pia, baadae tutafungua shauri la talaka.Kinyume na matarajio yangu wife kwa kuwa alishañichoka na hakuna kinachoendelea kati yetu nilijua angekubali tu. Cha ajabu hivi sasa kupitia wazee wake wameniita kikao zaidi ya Mara 6 sasa ili tusuluhishe tofauti zetuKawa mpole sana, alidhan nitaendelea kuteseka milele

Wakuu sasa sipo nyumbani kwa hasira ya mambo aliyonitendea hivi sasa sipo nyumbani nimepanga upande wa nyumba nimeanza ujenzi ili nihamie. Kila siku lazima nipite kwa watoto niwaone ndo niondoke. Nimesimama njia panda, mm binafsi nilishaamua simtaki tena huyu mwanamke ila wazee na viongozi wa dini tunakoabudu wanasema turudiane juzi mke wangu alinipigia magoti tukiwa kikaoni kwamba nimsamehe, nifute kusudio la kuomba talaka mahakamani. Wazazi wangu hawataki kusikia kabisa neno msamahakwa matendo aliyotufanyia.

NB: Nimetaja kipato ili kuwapa mwanga na uelewa wa tatizo isichukuliwe vinginevyo

Nimesikia amepata matatizo kazini ila sina uhakika na taarifa hizo

Naomba ushauri wenu

Mrejesho
 
Wazazi bana huwa hawamchoki mtoto,Chunga sana thaman ya wazazi wako_Wao ndyo mlango wa pepo
Mimi siwezi kuishi na mwanamke kama huyo hafai hafia

Hakuna dhambi kubwa kwa mwanaume kama;
1.Kumsomesha mwanamke
2.Kumrudia mwanamke aliyekunyanyasa
3.Kuoa mwanamke aliyezaa na mtu halafu mtu huyo yupo

Songs mbele achana naye huyo.

Note my words
 
Hautokaa kuwa na amani na huyo mwanamke.....hautomuamini, zaidi hana mapenzi na wewe.
 
ao wazee walikua wap wakati mwanamke anakunyanyasa!?..

Anyways moyo niwako ila ujue ukirudiana nae na mambo yakaenda kombo tena huna chako
 
Back
Top Bottom