Alininyanyasa sana nilipofukuzwa kazi, MUNGU ameniona, sasa yamegeuka

christo devries

New Member
May 6, 2015
1
60
Siku moja nisiyopenda kuikumbuka nilitwa ofisini kwa bosi wangu na kukabidhiwa barua ya kufukuzwa kazi
Hiyo ilikua ni baada ya uchunguzi wa miezi kdhaa wa kosa nililokua nimelifanya bahati mbaya. Miezi mitatu nyuma nilimuingizia pesa mteja kimakosa kwenye akaunti yake kiasi cha million mia tatu na hamsini ambazo alitakiwa kuwekewa Mteja mwingine halali kupata pesa hizo.

Kama humu ndani Kuna banker ataelewa nachokisema, kwamba makosa kama haya benki ni kawaida sana. Ukigundua kosa kama hili unawahi una reverse hiyo entry una m-credit anaetakiwa shida ni kama uliemwekea kimakosa akawahi kuzichukua ndipo yanakukuta yaliyonikuta mimi.

Baada ya kufukuzwa kazi mke wangu alibadilika kabisa
Nilishuhudia yafuatayo:-

(1) Alitamka mimi ni mjinga ndio maana nimefukuzwa kazi.

(2) Chake kikawa chake tu.

(3) Akawa anawaambia wazi watoto kuwa kitu fulani kimenunuliwa na yeye na sio mimi.

(4) Muda wa kurudi home ukabadilika sasa anarudi usiku mwingi, nampa kipigo cha nguvu anazira na kukimbilia kwao, kwenye usuluhishi anawaambia wasuluhishi kwamba mimi namuonea wivu kwa kuwa ana kazi mimi sina.

(5) Niliuza Gari zangu mbili ili nipate mtaji wa kufanya biashara hivyo nikawa sina Gari nilijua maadam wife ana Gari tutatumia wote maana hata yeye wakati hana Gari alikua akitumia magari yangu.

Kinyume na matarajio hakutaka kabisa niguse Gari lake mimi nikawa mtu wa miguu.Majirani wakawa wanashangaa mfumo wetu wa maisha.

(6) Life yetu ya bedroom ikawa imekufa no intimacy no love making nothing. Alianza kidogo kidogo leo mara aseme anaumwa, kesho kachoka, hadi mwezi unaisha. Nikaamua isiwe tabu nikaacha kuulizia tena, nae akawa amepotezea moja kwa moja.

Hata wazazi wangu aliwa mistreat sana wakawa hawaji tena kwangu, mama yangu akawa ananitumia vitu kwa njia basi kutoka nyumbani kama mchele, maharage, unga na kadhalika ili na mm nionekane nachangia.Wakuu siku ya kufa nyani miti yote huteleza. Kila nilichojaribu kukifanya ili nijinasue kinakwama, nakuta mtaji wote unakata naanza moja.Ilikatika miaka minne nikiwa kwenye hali hii maana nilipata matatizo 2010. Mwaka Jana kuna Dada mmoja tulisoma wote primary school akaamua kunisaidia, huyu dada tulikutana Posta accidentally tukapeana contact
mimi nilishamsahau ila yeye alinikumbuka.

Baadae akaniunganisha na mumewe ambae ni HR manager kwenye shirika fulani, nikamwelezea ukweli wote na akaniingiza kaziniWife sikumwambia kuwa nimepata kazi akaanza kuona nakuja na mahitaji ndani, nikawa naondoka zangu alfajiri narudi usiku mwingi. Nikaita mafundi wakabomoa ukuta wote wa fensi uliokua umeoza waliiba sana cement wakati wa ujenzi ukajengwa upya, vitu vyote vilivyochoka ndani nikabadilisha. Wife alishangaa sana ila akashindwa kuniuliza maana hadi hapo tulikua hatuongeleshani zaidi ya salam za asubuhi na jioni tu basi.

Wana jf siwezi kuwaficha sehemu niliyopata naingiza hela Mara kumi ya ile kazi yangu ya benki, hii sikutokana na mshahara bali njia mbali mbali katikati ya mwezi kitengo chetu tupo wanne,hali ikiwa nzuri huwa tunagawana hadi laki mbili kila siku, kama hali ni mbaya tunagawana laki moja kwa siku hii ni mbali na ile tunayogawana mwisho wa mwezi kama million 3 each person mshahara ni mdogo tu ni laki saba tu kwa mwezi.Maana mshikaji alisema anaweza kuniingiza kazini ila kama mfanyakazi wa kawaida kwa kuwa benki nilifukuzwa hakukua na reference wala background check so nikaamua kufuta kwenye CV kuwa nilifanya bank.

Nimeanza mchakato wa talaka kupitia mwanasheria mmoja rafiki yangu, mwezi January mwaka huu amemwandikia barua ya kumtaarifu uamuzi huo na copy Ustawi wa jamii pia, baadae tutafungua shauri la talaka.Kinyume na matarajio yangu wife kwa kuwa alishañichoka na hakuna kinachoendelea kati yetu nilijua angekubali tu. Cha ajabu hivi sasa kupitia wazee wake wameniita kikao zaidi ya Mara 6 sasa ili tusuluhishe tofauti zetuKawa mpole sana, alidhan nitaendelea kuteseka milele

Wakuu sasa sipo nyumbani kwa hasira ya mambo aliyonitendea hivi sasa sipo nyumbani nimepanga upande wa nyumba nimeanza ujenzi ili nihamie. Kila siku lazima nipite kwa watoto niwaone ndo niondoke. Nimesimama njia panda, mm binafsi nilishaamua simtaki tena huyu mwanamke ila wazee na viongozi wa dini tunakoabudu wanasema turudiane juzi mke wangu alinipigia magoti tukiwa kikaoni kwamba nimsamehe, nifute kusudio la kuomba talaka mahakamani. Wazazi wangu hawataki kusikia kabisa neno msamahakwa matendo aliyotufanyia.


NB: Nimetaja kipato ili kuwapa mwanga na uelewa wa tatizo isichukuliwe vinginevyo

Nimesikia amepata matatizo kazini ila sina uhakika na taarifa hizo

Naomba ushauri wenu
 
Pole saana
First details za kampuni yako mpya usingeweka
huwezi jua nani anapita humu ...ukabadilishwak kitengo ukarudi yule yule

Pili kuhusu mkeo.....wewe ndo utaamua nini ukifanye hata ukimsamehe hakuna tatizo
wanawake sometimes wana taka mume uwe kama baba yake
umsamehe kila siku.....

Mwisho ni lazima sasa ujifunze makosa yako

mume sio kutoa mahitaji tu..unapaswa kujifunza bonding....
bonding na mkeo ilikuwa ndogo........hata ukioa mwingine yaweza tokea haya haya...

halafu waswahili wanasema 'bora kukosea kujenga nyumba kuliko kukosea kuoa'
 
Ngoja waje manguli I hope watakushauri zaid,but kwa upande wangu me naona mungu amekuonyesha rangi halisi ya huyo kinyonga,HAKUFAI KABISA.tena anaonekana atakuwa na michepuko mingi tu.Tupa kuleeee.
 
Pole ila kubali pia na wewe una makosa yako,ya kupiga maybe hasira, tu,chondechonde na hiyo kazi mpya, hizo deal zenu hizo, yasije yakakukuta ya mwanzo, angalia wewe mwenyewe kama uko tayari kumpa second chance muanze upya,mwanzo utakuwa mgumu, Ila hakuna asiekosea, maybe ameshajifunza
 
Katika hili nimejifunza tu umuhimu wa Mama! Mungu awajalie Mama zetu na alaaniwe Mtu atayemdharau Mama yake, pamoja na yote bado Mama alikutumia vyakula! Mi nisingemsamehe hata Kidogo, ila naona Wataka msamehe na sitaingilia, sasa nashauri muulize Mama yako na atakacjosema fuata!
christo devries
 
Last edited by a moderator:
Katika hili nimejifunza tu umuhimu wa Mama! Mungu awajalie Mama zetu na alaaniwe Mtu atayemdharau Mama yake, pamoja na yote bado Mama alikutumia vyakula! Mi nisingemsamehe hata Kidogo, ila naona Wataka msamehe na sitaingilia, sasa nashauri muulize Mama yako na atakacjosema fuata!

mi nimependa pale aliposema anampa kipigo cha nguvu....
 
Duh! Pole sana mkuu. Hawa viumbe tunaishi nao kwa Neema tu, ila ni wabinafsi na wakatili sana. Kaka hapa wewe ndo muamuzi wa mwisho coz unajua mapito ulopitia, watu wengine watachukulia kirahisi tu.
 
Daah asee pole sana. Hapo hata nikikushauri usamehe na uendelee nae huyo mke wako. Real love haitokuwepo kamwe maishani mwako. Mi ningekushauri tu ufanye lile jambo ambalo unahisi litakupa furaha maishani mwako.
Kama ni kumwacha na kumwoa mwingine sawa. Ama kama utaweza samehe na kusahau pia sawa.
 
christo devries

"Hakuna msiba usiokuwa na mwenziwe" this is fact I was facing the same , real the same.....I even thought U wrote for me!!...!
Just follow The Boss advices..for your decision...WANAWAKE WOTE BABA YAO MMOJA" Bora uoe darasa la 7 kijijin hata ukikosa mia mtafungua genge na maisha yataenda na atakuombea kila siku..

..lakini hawa tunasema wasom wenzetu...ajabu hata mambo yakiwa mazuri still wanataka kuwa competitors na husband hao......hakuna kitu kinaumiza katika familia kama hichi cha baba hichi mama...hapo ujue direction imepotea....ya family......

"ukitaka kuoa binti angalia mama yake"....tabia ya changu changu chake changu inaanzia kwao.ktk familia....!! binafsi nimekuwa sijawai ona kitu cha baba na mama ktk familia yetu...!!
'
 
Last edited by a moderator:
Mkuu pole sana kwa matatizo ya miaka minne. Ndoa ni kwenye shida na raha, mume hatakiwi amtelekeze mkewe akiwa na shida yoyote ile hata kama ni ugonjwa hali kadhalika mke.

Huna mke hapo matatizo hayana leo wala kesho kwahiyo yanini umrudie huyu wakati ameshakuonyesha wewe na wazazi wako ubinadamu wake!?

Usifanye makosa ya kurudiana na huyu, songa mbele na maamuzi yako ya kumtaliki. Dah! hawa wanawake wengine wanashangaza sana kwa roho zao mbaya, wana roho mbaya zaidi ya shetani!!!
 
Back
Top Bottom