Wakuu habari zenu,
Kuna binti nilimpa mimba mwaka 1995 wote tukiwa wanafunzi wa kidato cha nne mjini Mwanza na wote tulisoma shule moja na darasa moja. Alipoitwa na mkuu wa shule kuhusu tetesi za yeye kuwa na mimba alikiri mbele ya mkuu na akanitaja mimi kama mhusika wa mimba kinyume na makubaliano yetu kwamba asinitaje.
Nilipoitwa mbele ya baraza la shule na mbele ya mwalimu mkuu nilimkana na kujibu sihusiki, hii ilitokana na ukweli kwamba ningefukuzwa shule na ndoto zangu zingeishia pale.Hivyo shule iliamua kumfukuza binti pekee.Mtaani niliendelea kumuona na kumfariji hadi nilipomaliza form six na kuchaguliwa kujiunga na UDSM.
Nikiwa mwaka wa mwisho alikuja chuoni kuniona na kunipa taarifa kuwa mtoto alifariki kwa pneumonia na walishazika na akaangua kilio kizito pale chuoni, niliumia nikajikaza nikasema ndio maisha nikasonga mbele.Tangu wakati huo hatukuonana tena, mimi baada ya chuo nikapata scholarship Marekani kufanya master's kupitia NGO moja ya kidini baba alikua mchungaji sasa amestaafu.
Hata baada ya masters niliendelea kukaa Marekani nikitafuta maisha kwa muda mrefu nikapata mtanzania mwenzangu tukawa wachumba na tukaamua turudi home kufanya maisha huku Dar es salaam tukarudi na tukafunga ndoa, tumebarikiwa watoto wawili.
Mwaka jana nilipata taarifa zilizonishtua kuwa mwanangu yupo hai na ni binti mkubwa tu na kwamba alikua akijiandaa na mitihani ya form four huko Mwanza. Nikahangaikia likizo kazini nikaipata November nikasafiri kwenda Mwanza kuhakikisha hizo habari ili niweze kumwona mtoto Mwanza.
Nikafikia hotel na kesho yake chanzo changu cha habari kikanipeleka shuleni kwa mtoto ambapo ulikua ni siku ya graduation yao. Nilipomuona mtoto nililia mno ni mzuri ajabu na anafanana na mimi hadi aibu, aliponiona alishtuka kwa jinsi tulivyofanana muda kidogo mama yake akafika na mumewe, hatukua tumeonana miaka mingi sana alishtuka sana kuniona almanusura adondoke chini.
Wakuu nililazimika kuwa mpole ili tumalize shughuli, baadae ilitokea sintofahamu kubwa mtoto akitaka kujua mumu ni nani, mama akidai hanijui, mm nikamwambia binti mimi ni baba yako, ikawa ni fujo tupu waalimu wakatupeleka ofisini. Walimu wakamsuta mama mtu kwa jinsi tulivyofanana na yule mtoto.Yule mumewe akaanza kumtukana mama mtu kwamba kwa nini alimdanganya baba wa mtoto alifariki kumbe yupo hai.
Wakuu hadi sasa kuna ugomvi mkubwa hawataki nimchukue mtoto, ila mtoto anataka kuishi na mimi wananiapia viapo vyote kwamba haitotokea nimchukue huyo mtoto hata kwa dawa. Mimi makazi yangu ni Dar wao wapo Mwanza, nashindwa kulishugulikia hili jambo ipasavyo kutokana na kazi kunibana nashindwa kusafiri, nitumie njia gani nipate haki yangu, mbaya zaidi mume amekua upande wa mkewe. Naomba kujua kisheria imekaaje.
Naomba ushauri wenu