Alikuwa binadamu kweli?

We ulikutana na jini tu, huenda hata ulipelekwa juu ya mti huwa inakuwa hivyo unapelekwa sehemu unakutana na watu ila siku ukija itafuta ukaiona utashangaa kila mtu anashangaa mbona hakuna mtu kama huyo
Unanitisha
 
Ile mail mliokua mnawasiliana akiwa aneenda Marekani ndiyo ingekua nzuri kumfuatilia, cha ajabu nayo imepoteza how comes ulikua unafuta msg zake? Ukienda kwenye list ya watu ulikua unachat nao utaipata lazima iwe pale, nani atakua ameifuta
Miaka kumi imepita
Na tuki la kwenda kwenye hiyo nyumba ni miaka sita imepita
 
Historia inaanza hivi...

Kipindi nkiwa bado shule secondari miaka kumi sasa imepita,nilinunuliwa simu na bro wangu. Siku moja ghafla mida ya mchana iliingia SMS kutoka kwa namba ngeni ikisomeka "ukitoka hostel nijulishe uniazime kitabu chako" sikumbuki sawa sawa but nimeotea tu kwa kumbukumbu.

Nikaanza kuchat nae kitabu gani na wewe nani
Ndipo mbele akagundua amekosea number na kuomba radhi kwamba alikuwa anamtumia mdada mmoja classmate wake namba zinafanana
baadae tukaanza kufahamiana kwa kuendelea kuchat.

Alijitambulisha anaitwa Jimmson Henry, anasoma chuo kikuu mlimani (UDSM). Yuko mwaka wa pili bachelor degree ya information technology (IT). Anaishi hostel za mabibo lakini kwao tabata.

His paternity origin is Ngazdja from Comoros islands,and Lindi mtwara kwa upande wa mama. He was so talkative,cheerful,funny na utani mwingi!

Tuliendelea na mazoea ya kuwasiliana,alinieleza mengi kuhusu maisha yake.nami yangu pia.

Mwisho sababu ya ujana akaanza kuniomba nafasi,nami nikampaa bila hata kumuona.

Mazoea yaliendelea ikafika muda nipo likizo akaomba tufahamiane kwetu tunapoishi,alianza yeye nikamleta kwetu hadI bi mkubwa alimuona.

Ikafika zamu yangu nikaunga "tuisheni" kwao maeneo ya tabata liwiti.

Nilivyofika kwao aliweza kunitambulisha kwa mdogo wake wa kiume hawapishani sana kiumri anaitwa James. Tuliongea mengi na kuna mzee jirani pia alikuwa ni seremala naye akamuuliza huyu nani akanitambulisha rafiki yake.

Baada ya kuondoka tukaanza kuwasiliana ananiambia we ni mzuri sana hadi huyu mzee hapa jirani ananitania yule mrembo umemtoa wapi,kakangu piaa!

Few months later akamaliza mwaka wa pili na kuwa likizo na mimi nkiwa natarajia kuingia mitihani yangu ya final.

Akanijuza kapata mwaliko america kutoka kwa rafiki zake wawili na taratibu zote za visa,tickect kafanya kwa gharama za wenyeji wake akafanikiwa kwenda. Alikaa kwa miezi mwili tunawasiliana kwa njia ya email nkiwa na mdogo wake.

Akirudi na tukaanza kuwasiliana as usually.

Kufupisha kuna kipindi alikua anapitia majukumu magumu ya kifamilia kama mtoto wa kwanza kwao,akawa anakosa hata muda nami. Nami nikawa frustrated na mambo yangu tukakorofishana na kupotezeana.

Baada ya mwaka mmoja nikiwa chuo sikuweza kuhimili alikuwa amenikaa sana kichwani hadI napata msongo wa mawazo.

Nikajiambia kwao napakumbuka nijaribu kwenda.
Nilipanga weekend asubuhi nikaifikia nyumba nikiwa nimekaa mbali kidogo nione kama atatokea mtu.

Masaa yalipita nikahisi hawapo japo mlango upo wazi. Akatokea mdada mrefu mweupe nikajua atakuwa member mojawapo wa familia.

Nilisogea na kumsalimia akanijibu nikaanza kumuulizia jamaa wakaanza kushangaa hawamjui. Nilitaka details zote hadI wadogo zake na Dada zake hawamjui
kuulizia ile nyumba wale wadada wanadai wao wameishi pale tangu udogoni na mtaa mzima wanawajua. Haijawahi kuishi familia nyingine hata kupangisha
nikawauliza kama kuliwahi kuwa na mzee seremala upande wa nyumba anaranda mbao wanajibu hakujawahi kuwa na fundi seremala hapo.

Na nikiangalia like eneo naona tupu hakuna dalili yoyote hata mzee kuacha mabenchi ya mbao.

Kuna maduka around nikawa nawauliza wanadai hawajahi kuishi na mtu wa aina hiyo, hawamjui
Lakini nyumba ni ile ile hadI ndani kuko vile vile. Mpaka sasa sipati jibu.

Maana alishare nami vitu vingi mno mpaka harusi ya mdogo wake ilifanyika kwenye nyumba hiyohiyo.

Safari zake zote.mamake ahata akiwa anaumwa na2julishwa nimpe pole mkwe. Plans zake zote.

Mfano alivorudi kutoka America alipewa zawadi ya gari akaghairi sababu hana uwezo wa kuhudumia, akaomba badala yake atumiwe vifaa vya office tufungue stationary kubwa kijitonyama.

Alikua so bright kiasi anapata nafasi za kazi kwenye biashara na makampuni za maprofessor wake. Kila kitu ndani ya ofisi anashare nami.

Mpaka sasa ananiwinda kichwani kama mzimu na hapo kwao ndo hivi kama nilivyopakuta sijapata majibu hadI sasa.

Alikuwa nani?
Polee,, watu wa mtandaoni wakati mwingine siyo wenyewe!?

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Hutaki kuamini lakini ndiyo ukweli, na ndiyo maana ukaambiwa origin yake ni Commoro mengi hujitambulisha commoro, pemba, Oman n.k. Na wala hakukosea namba alikuwa kakulenga wewe sema una bahati. Ukikaa ukatafakari sana utagundua kuna vitu havikuwa vya kawaida kwake.
Hivi miaka ya nyuma kuna watu walikimbia vita kwa mitumbwi visiwa vya Comoro na wengi wakajikuta Tanzania?
Historia ya babake
 
Back
Top Bottom