Alikiba kutoa mavazi ya jinsi,miwani,viatu,na vinywaji.

Supervision

JF-Expert Member
Jun 16, 2016
265
203
HAYA NDIYO MASHINDANO TUNAYOTAKA YAKUSAIDIA TAIFA

Zikiwa zimepita wiki mbili toka Mwimbaji mwingine staa wa Bongofleva Diamond Platnumz kuzindua Perfume yake, leo May 11, 2017 kupitia 255 ya XXL Mwimbaji staa wa ‘aje’Alikiba ameweka wazi kuwa moja ya mipango yake ni kutoa mavazi aina ya jeans, miwani, viatu na vinywaji vya energy vyenye jina lake.

Alikiba amesema kuwa hiyo ni mipango mizito na hatarajii kuifanya kiholela kwani hata mwanzo alifanya kama promotion lakini sasa hivi hayupo tayari kuikosea serikali na amejipanga kufungua na duka ili watu wake waweze kupata kwa urahisi.

“AK ni Brand ya Alikiba nashukuru imekuwa kubwa watu wanavaa lakini pia ipo na ya King Kiba nayo ni brand yangu na zipo official kabisa na kazi zitakapoanza watapata product zote’ – Alikiba

“Kuna Malengo makubwa sana tumeyaweka lakini siwezi kusema sasa hivi ila kuna Jeans Viatu na Glasses tayari zishatoka soon wataziona maana hizi zitakuwa za kwanza sababu tayari zishatoka na kuna energy drink”– Alikiba
 
Ni mradi mzuri na unaofaa kabisa, maana katika maisha mambo mengi tunajifundisha kupitia kwa wengine.

Ngoja waje na wenye mawazo ya mlengo wa kushoto watoe maoni yao pia.
 
Hicho kinywaji kitakuwa hakikauki nyumbani kwangu.
Fanya mambo Kiba,tupo wa kukusapoti.

Mashabiki wa ukweli hatuishii insta,tunakusapoti ktk kazi zako pia.
Ila sasa...uangalie na kipato cha Watanzania tulio wengi,mambo ya kutuuzia bidhaa laki utafeli.
Kila la kheri.
True nami ntakunywaaa daily kam nyonyo la mama but si kwa bei 10,5000
 
Hicho kinywaji kitakuwa hakikauki nyumbani kwangu.
Fanya mambo Kiba,tupo wa kukusapoti.

Mashabiki wa ukweli hatuishii insta,tunakusapoti ktk kazi zako pia.
Ila sasa...uangalie na kipato cha Watanzania tulio wengi,mambo ya kutuuzia bidhaa laki utafeli.
Kila la kheri.
TEAM KIBA wana maneno!
True nami ntakunywaaa daily kam nyonyo la mama but si kwa bei 10,5000
 
Kinywaji kiitwe

Alikiba soft drink

Alikiba energy drink

KingKiba energy drink

au

Kingkiba juice

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom