Shida sio waaminifu na mkishalipwa mwenye kazi ndio anakuwa kibarua kuwatafuta mafundiba wewe una kampuni?
Ni kweli mafundi wengi sio waaminifu. Sababu kubwa ni pale ambapo wanakuwa na ahadi nzuri Kwa client ilhali hawawezi kuzitimiza.
.......Wanaahidi kumaliza kazi Kwa mda mfupi ilihali haiwezekani
........ Wanaahidi kufanya kazi nzuri na Kwa wakati ilihali budget hazitoshi.
Kama sijakosea hizo mbili hapo juu ndio changamoto mnazipata kwa mafundi wengi.
NINI KINASABABISHA HIYO CHANGAMOTO :
Pressure au hofu ya kukosa kazi.
Kama unavyojua hii field imevamiwa na watu wengi sana ( idadi ya mafundi ni kubwa kuliko idadi ya kazi au tender) Kwa kua kazi moja inagombaniwa na mafundi wengi MTEJA (clients) wanahulka ya kumchagua fundi aliye cheap bila kujari uhalisia WA kazi.
Mfano.
Kazi amboyo budget yake halisi ni 4m kwasababu ya ushindani fundi atakubali hata kwa 3m. Kimbembe kinaanza 3m ikikata na bado kazi haijakamilika.
Pia kazi ambayo kiuhalisia inakamilika Kwa siku 30, ILI kumfurahisha boss na apate kazi, fundi ataahidi KUKAMILISHA Kwa siku 20.
Pamoja na hayo yote, changamoto zipo Katika Kila field. Mabank yanalaumiwa na wateja, TANESCO wanalaumiwa , Dawasa, hata Katika mawizara lawama zipo.
Jambo la mhimu nikujitahidi kuziondoa hizi changamoto Kwa kupatana Kwa haki.
Umeniuliza Kama Nina kampuni?
Jibu ni hapana mm si miliki kampuni. Ila nikipata kazi inayonilazimu kuwa chini ya kampuni, Huwa natumia kampuni.
Natanguliza shukran zangu, endapo ukihitaji fundi, TRY ME.