Alikataa nisimuoe kisa ualimu

Alikataa nisimuoe kisa ualimu

Mi kumuacha mtu ni mpaka unipige matukio ya kinyuklia na nikikuacha nimekuacha sirudi nyuma

Watoto ndo wanaacha mwanaume kwa sababu zisizo eleweka km hizo ulizotaja
Hongera. Now you are matured enough...kapeace.

Hata maisha ya ndoa unaweza kuyahimili.
 
bikra umetoa wewe so!?? what is bikra!?? mke daktari anatosha.. biashara zinahitaji upanuzi.. usiruhusu ngono zikupoteze.. ukiona mawazo yanakuja ukifika home waite wanao.. jiambie.. "leo namcheat mke wangu alonizalia wanangu wazuri hivi, sikuwa na kitu alinipenda nilivyo.. leo natafuta kuachana na kumnyima amani.. Mungu nisamehe hata kuwaza haya" achana na watoto wa mjini mzee
 
oa mkuu, umemchakaza na sasa amejutia anataka kurudi oa tu
 
Miaka kumi iliyopita yani 2009 niligraduate bachelor of Education in Arts UDSM nilikuwa na mpenzi wangu aliyekuwa anaitwa Rechael yeye alikuwa anasoma Bachelor of Tax .. IFM .
Hakika tulipendana na kuendana sana ila alikuwa sister duu sana hakupenda niseme kuwa mimi ni mwalimu by professional eti nitamtia aibu kwa marafiki zake.

Baada ya sisi wote kuhitimu sikumaliza hata mwezi nikapata kazi kufundisha St Anton mbagala na nilikuwa napata take home 700k kwa mwezi huku yeye akiwa bado anahaha kutafuta ajira but haikuwa issue nilimpa kila alichokitaka kadri ya uwezo wangu nikapanga nimuoe.

Kumwambia nimuoe akagoma eti hawezi kuolewa na mwalimu aina yeyote ni aibu kubwa sana kwake na familia yake sio siri niliumia sana but kwakuwa mimi sipendi fake love nikaamua bora tuachane.

Ktk pitapita zangu nikakutana na mtoto Glory ambaye alikuwa anasoma KCMC bachelor of Medicine akanipenda kweli na Inshaalah nilimuoa na mpaka sasa ni mke wangu na tumezaa watoto wawili.

Huwezi amini ile dharau ya Rechael ilinifanya nirudi shule kusoma zaidi na sasa Alhamdulillah nimefika sehemu nafanya kazi nzuri zaidi kwa maslahi zaidi huku nikiwa na miradi kibao hapa mjini ikiwemo uber, bodaboda, maduka etc.

Leo ktk pitapita zangu mitandaoni nikakutana na friend request kucomfirm kumbe ni Rechael akiniuliza maswali kibao na kunilaumu eti yeye ilikuwa ni ujana na ujinga tu tu hivyo haikuwa akili yake akaomba nimsamehe sana kwani bado ananipenda sana.

Nikamwambia siunajua kuwa nina mke sasa kajibu ndio ila yeye hajali na hawezi kubali kunitoa moyoni ni utoto tu hivyo yupo tayari nimuoe mke wa pili nikakumbuka wimbo wa "barua" ya Bushoke aliposema "kumpenda bado ninampenda msemakweli mpenzi wa Mungu" ila ninachofikiria ni mke wangu wa sasa.

Nimuoe mke wa pili au nimfanye outside chick hizo ni option nilizojipa coz bado ninampenda ukizingatia ni mtoto wa kiislamu full maadili bikra yenyewe kikombe nimekidondosha mimi kikavunjika!
Ila je ananipenda tu nikiwa na hadhi je nikiporomoka itakuwaje mana mshika mawili moja humponyoka au kukosa yote.

Nishaurini wadau ila naomba ushauri kutoka wanajf ambao atleast wana 30 yrs na kuendelea mana jf ya sikuhizi utoto mwingi
Rachel ni nyoka hata Mimi amenifanyia hivyo hivyo
 
Mbavu mbili haziwezi kuingia kwenye mdomo moja lazima nyingine itaingia mdomoni na nyinyine puani, tumia akili
 
Hata ww bado una utoto na ujana ..
Vijana endeleeni na utoto wenu
Tulia mshono na mkeo bro ...
Rachel Scale ishamwingia akaze tu.
 
bikra umetoa wewe so!?? what is bikra!?? mke daktari anatosha.. biashara zinahitaji upanuzi.. usiruhusu ngono zikupoteze.. ukiona mawazo yanakuja ukifika home waite wanao.. jiambie.. "leo namcheat mke wangu alonizalia wanangu wazuri hivi, sikuwa na kitu alinipenda nilivyo.. leo natafuta kuachana na kumnyima amani.. Mungu nisamehe hata kuwaza haya" achana na watoto wa mjini mzee
Asante
 
.
59716026_2487817697906167_6524825401670238208_n.jpeg
 
  • Thanks
Reactions: THT
Back
Top Bottom