Nunua na Aliexpress: Tuelimishane manunuzi mtandaoni

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,796
Wapendwa wa familia kubwa ya JamiiForums. Waswahili wanasema KIZURI KULA NA NDUGUYO.

Tunaingia kwenye zama za biashara na manunuzi mitandaoni, yaani muuzaji na mnunuzi hamfahamiani kabisa bali kuna mtu wa kati anayewakutanisha (dalali).

Huyu dalali amejenga uaminifu pande zote mbili kati ya muuzaji na mnunuzi, hivyo atapokea malipo ya mnunuzi atamjulisha muuzaji kuwa malipo yake anayo, muuzaji atatuma bidhaa husika. Mnunuzi akiipokea atathibitisha kuwa amepokea na dalali atapeleka malipo kwa muuzaji.

Nitaweka baadhi ya bidhaa nionazo ni unique kila wakati na utakayoipenda utaingia mtandaoni mwenyewe ama kupitia wakala.

Vilele nakaribisha maswali kuhusu manunuzi ya mtandaoni. App ninayotumia mimi ni Aliexpress lakini pia ziko nyingine nyingi.

-1100202614-1565220773.jpg
-291408246-1494925124.jpg
-1756715671538406067.jpg
 
mm nataka kununua Vitu alibaba vipi unaweza nisaidia???
Sitaki kuharibu biashara ya mtu lakini kulinishinda kule ...hata hivyo haya maduka mawili ya mtandaoni inaelekea mmiliki ni mmoja.

Ilianza Alibaba ilipoharibu akaja na Aliexpress nadhani....kwakuwa icloud inasoma Alibaba.

By the way ulikuwa unahitaji vitu gani?
 
Mimi nahitaji msaada wa kuship kwa haraka kutoka AliExpress, last time niliagiza mzigo March umefika Dar July hii na bado mmoja haujafika.
Dadeki..😅

Ukitaka ufike mapema zaidi tumia wasafirishaji Kama dhl n.k ila gharama zake usinune.. halafu mbona imekuchukua muda mrefu hivyo maana najua free shipping huwa ni mwezi Sasa wewe duh! Au ndo tuseme corona..😜
 
Dadeki..😅

Ukitaka ufike mapema zaidi tumia wasafirishaji Kama dhl n.k ila gharama zake usinune.. halafu mbona imekuchukua muda mrefu hivyo maana najua free shipping huwa ni mwezi Sasa wewe duh! Au ndo tuseme corona..😜
Yes Corona ilichangia mzigo kuchelewa. DHL bei mkasi sana wana App yao pia nilijaribu daah ni changamoto sana upande wa charges.
 
Back
Top Bottom