Alichosema Pengo kuhusu kura ya maoni

Alichosema Pengo kuhusu kura ya maoni

Hii nchi inashindwa kupiga hatua sio kwa sababu watu wabaya wanaongoza nchi vibaya, bali kwa sababu watu wazuri wamenajipambanua kuto CHAGUA UPANDE. Kwa kufanya hivyo ni sawa na kuruhusu MBABE aendelee kueneza propaganda zake.

CCM ndio chama Tawala, viongozi wake waandamizi serikalini wamesikika wakiomba Wananchi KUPIGA KURA YA NDIO kwa KATIBA INAYOPENDEKEZWA ilhali mambo waliyopewa kipaumbele ni matakwa yao sio matakwa ya UMMA. Serikali ina fedha na miundo mbinu ya kusambaza agenda yao ya KURA YA NDIO.

Ni vizuri wakatokea makundi mengine bila kujali nafasi zao katika jamii kuonyesha dira bila UNAFIKI, huu sio wakati wa kuchagua VUGUVUGU ni kuchagua MOTO au BARIDI kwa maslahi mapana ya taifa.

Hainiingii akilini kiongozi kama Kardinali Pengo haoni UBATILI WA KATIBA INAYOPENDEKEZWA iliyoandikwa ikiwa na msingi wa utengano na ubaguzi ikisheheni michango ya MATUSI, KEJELI, ULAGHAI, UHASAMA, UBABE, UHUNI kuwa WACHUNGAJI WETU WA DINI watuache tuamue WENYEWE kama NDIO au HAPANA.

Nini nafasi ya KANISA?
Je, kanisa litaweza kumbadilisha muumini kutenda mema wakati sheria za kazi anayoitegemea kumpatia kipato inaruhusu ubadhirifu, wizi, ufisadi, kukosa haki na usawa?

Kauli kama hizi zinatia shaka sana hasa ikizingatia Askofu wa Kanisa KATOLIKI alipokea MCHANGO/ZAKA kutoka kwa RUGEMALILA, fedha ambayo ni DHULUMA KWA UMMA.

JE? PENGO anataka kutuambia anabariki DHULUMA?
Hatukumsikia kumkemea Askofu aliyepokea SADAKA ya milioni 80 kupitia akaunti yake binafsi sambamba na wateule wengine kina Andrew Chenge, Prof.Tibaijuka, William Ngeleja.

Katika mazingira kama haya WANANCHI tunatakiwa KUPUUZA USHAURI KAMA HUU, na badala yake tuukatae UHERODI katika Tanzania yetu. Hata katika biblia wapo waongozi wa dini walioshirikiana na watawala kuhakikisha YESU KRISTO anauawa.
 
Back
Top Bottom