Kwa bahati mbaya sijaweza kusikiliza hiyo clip, imegoma. Ila Pengo ana uhuru na haki ya kutoa maoni yake binafsi kama raia wengine kuhusu katiba, sipingi hilo.
Tatizo ni pale kama na yeye ni miongoni mwa hao TEC na alikuwepo wakiweka msimamo wao na mbaya zaidi kama hauongelea mtazamo wake huko kwenye TEC hadi walipotoa tamko na yeye akaja kutoa toleo tofauti na wenzake patakua na tatizo.
Narudia tena, sijasikiliza hiyo clip huenda ni tatizo la kiufundi kwenye PC yangu, ila kwa mantiki wananchi inabidi waeleweshwe kuhusu katiba pendekezwa kisha wao waamue wanachotaka.
Mimi naona maaskofu walikuwa sahihi na Pengo hakuwa sahihi kwa sababu zifuatazo:
1. Maaskofu waliandika waraka wao katika mazingira ambayo kila kiongozi wa serikali alikuwa akisisitiza kura ya maoni itapigwa Aprili 30 wakati mchakato wa uandishwaji kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ulikuwa unaendelea kwa kusuasua, muda wa kutoa elimu ya uraia na kampeni vilikuwa bado vinazua maswali mengi kwa mujibu wa sheria na pia nakala za katiba hazikuwa zimewafikia wananchi wengi ambao wangeshiriki kupiga kura.
2. Kama wadau wengine walivyokuwa wameishaishauri serikali kuahirisha mchakato, maaskofu nao walitaka mchakato uahirishwe ili uandishwaji wa wapiga kura kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ufanyike vizuri na pia kuwe na nafasi ya kutosha ya kutoa elimu ya uraia na kampeni.
3. Pamoja na haya, serikali ilisisitza kura iko palepale!
4. Katika mazingira haya, maaskofu waliona kama serikali itaendelea kusisitiza "kura ya maoni iko palepale" wakati kuna hizo kasoro basi ni heri waumini washiriki kujiandikisha na waipigie kura ya hapana katiba inayopendekezwa.
5. Wanaoona kuwa maaskofu walikosea wanataka kusema kwamba mchakato wa kujiandisha, kutoa elimu ya uraia na kampeni na usomaji wa katiba na kuelewa maudhui yake kungewezekana tu by Aprili 30.
6. Sasa tujiulize hii ilikuwa kwa maslahi ya nani ikiwa hadi sasa watu wengi hawajajiandikisha na hawajaisoma hiyo katiba?
7. Katika mazingira haya kweli Pengo na wanaomwuunga mkono wanaona serikali ilikuwa sahihi tu kulazimisha kura ya maoni ifanyike Aprili 30?
8. Kitu kingine mbona serikali inawasihi wananchi kuipigia kura ya ndiyo katiba inayopendekezwa na hakuna anayeona ni kuingilia uhuru wa wananchi wa kuchagua (mfano ujumbe kuhusu katiba inayopendekezwa unaosomwa kila siku TBC)?