Alichosema Nape kuhusu wanaoponda Diamond kukabidhiwa bendera

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,817
4,059
Nape NNauye akihojiwa na kipindi cha Planet Bongo kuhusu watu kuponda Diamond kupewa bendera ya taifa kuiwakilisha Tanzania Afrika kusini amedai watanzania ni watu wa ajabu na wanapenda kunung'unika na kubeza kila jambo na akiwajibu atakuwa anazidi kuwakuza na watakuwa wanabeza zaidi
Pia ametolea mfano wa msanii Shakira alipoenda kutumbuiza Afrika Kusini alienda na bendera ya taifa lake sasa anashangaa watanzania kuhoji msanii wa nchi yao anapopewa bendera ya nchi yao

 
huyu jamaa kuna picture alionekana office kwa almasi akishangaa kuliko ikulu.Na alamsi akiwa kama soro fulani.
 
Chama mfu chadema kazi kukosoa kila kitu wakati wao hata ofisi ya chama imewashinda kwa miaka 25!!!!
Toa upumbavu hapa
.CCM ilijenga jengo gani zaidi ya yale tuliochangia kwa lazima hata kama hatukuwa wanachama
 
Watu sio directly wanamponda Diamond..!! Watu wanamponda waziri Nape na Wizara yake kuwa IMESHINDWA KUFUFUA MICHEZO HASA WA MPIRA WA MIGUU...!!

Yaani, badala ya timu yetu ya Mpira wa miguu kwenda Gabon kucheza na kushiriki mashindano, hatuna timu imara, Waziri yupo, Wizara ipo, na wananchi hawaoni kabisa juhudi za wizara kufufua hata mchezo mmoja kuwa na nguvu kubwa. hasa football, Sasa badala yake Diamond ndio anabeba bendera ya Taifa, hatumpondi Diamond, ingependeza zaidi na zaidi Timu yetu ya Taifa iwe kule na bendera yetu, sasa tumekuwa washereheshaji tu kwa kuwaimbia, na ijulikane wazi si juhudi za Wizara zimemsaidia Diamond hapana, ni personal efforts.. ingefaa sana Timu yetu ya Mpira iende Gabon na bendera yetu, Waziri na Wizara yake wamefeli sana, asitake kuficha madhaifu ya wizara yake kusema tunamponda Diamond, sisi tungependa ona TIMU YETU YA MPIRA IKO GABON, full stop.!! Aache kelele tunataka football, hatuoni juhudi zake zozote kufufua football..!!
 
Back
Top Bottom