Elections 2010 Alichokiomba Dr Slaa ni kusitisha kutangaza matokeo, sio Umwagaji damu

Majina yote weka hapa. Ukweli uko pale pale. Hakuna mtu anataka kutokuwa mwoga kwa au mnafiki kwa kuleta fujo ambazo hazina tija. Twende mbele na turudi, si njia njema.
Tujadili hoja.

hoja ipi hiyo? ya wewe kujiita kuwa ni mwanachadema wakati unajua kabisa ukweli sio huo?

Acha crap zako bana, ukileta bange hapa, utazipata tu maana haya nyani haangaliwi usoni.

Unafiki wako peleka huko huko Lumumba walikokutuma.
 
Wote (au wengi) tumesikia alichosema.

Ameomba kura zisitishwe kutangazwa.

Mimi ningeongeza kuwa, matokeo yajumlishwe upya kwa kutumia namba za mwanzo zilizopatikana katika kila kituo na kusainiwa na mawakala wa vyama vyote.

Kama kweli ccm mmeshinda, kwa nini msikubali kura zijumlishwe upya (sio kuhesabiwa upya)?

Mwafrika, kila mwenye macho na masikio, ameyaona na kuyasikia madudu ya NEC kwenye uchaguzi wa mwaka huu, kwa kifupi maroroso ni mengi tuu, lakini kwa vile Dr. Alisaini kuzikubali zile rules of the game, kama ana malalamiko yoyote, angeanzia kuyapeleka kwa refa (NEC) ndipo akaja na vyombo vya habari na hatimaye ayakabidhi kwa umma.

NEC inajua inachokifanya,( kuna posti niliposti kule nyuma kuhusu matokeo ya mwisho, nilitukanwa sana, nikashauri tusubiri nami bado nasubiri) na itaendelea na inachokifanya, Kesho saa 11 jioni, watatangaza matokeo ya mwisho na baada ya hapo hakuna hata mahakama yenye uwezo wa kufanya chochote. Jumamosi Saa 4:00 Uwanja wa Taifa, JK ataapishwa, kitakachofuata ni kusubiri 2015!.

Kila mpenda demokrasia wa kweli, lazima anaumizwa na kinachoendelea, naamini hata wana CCM wa ukweli, hawaipendi hali hii ya kupewa ushindi wa mezani, lakini Dr, anapaswa kuyapeleka malalamiko yake kunakohusika kwanza, ndipo na aumwage mtama kwenye kuku wengi.

Kwenye kulijadili hili, naombeni ushabiki tuuweke pembeni, tutangulize maslahi ya taifa.
 
hoja ipi hiyo? ya wewe kujiita kuwa ni mwanachadema wakati unajua kabisa ukweli sio huo?

Acha crap zako bana, ukileta bange hapa, utazipata tu maana haya nyani haangaliwi usoni.

Unafiki wako peleka huko huko Lumumba walikokutuma.

Crap ni nini kama unavyoitumia hapa? Bange tena?!
Pili, siyo lazima niwe mwana-chadema ili niweze m-support Slaa. Naweza niwe nipo nipo tu na nika-support yoyote. Na wewe hulazimishwi kuwa chochote kile. Mimi nasema hali halisi moyoni kwangu, siyo mwanachama yoyote na nina support ninaye mpenda.
Muhimu ni kuwa hapa tunaongelea mambo halisi ya nchi, yanayomuhusu mpiga au asiyepiga kura yaani Watanzania.

Mwafrica kama unaenda kwa bangi leo kunywa chai unielewe.
 
Mwafrika, kila mwenye macho na masikio, ameyaona na kuyasikia madudu ya NEC kwenye uchaguzi wa mwaka huu, kwa kifupi maroroso ni mengi tuu, lakini kwa vile Dr. Alisaini kuzikubali zile rules of the game, kama ana malalamiko yoyote, angeanzia kuyapeleka kwa refa (NEC) ndipo akaja na vyombo vya habari na hatimaye ayakabidhi kwa umma.

Kweli kabisa

NEC inajua inachokifanya,( kuna posti niliposti kule nyuma kuhusu matokeo ya mwisho, nilitukanwa sana, nikashauri tusubiri nami bado nasubiri) na itaendelea na inachokifanya, Kesho saa 11 jioni, watatangaza matokeo ya mwisho na baada ya hapo hakuna hata mahakama yenye uwezo wa kufanya chochote. Jumamosi Saa 4:00 Uwanja wa Taifa, JK ataapishwa, kitakachofuata ni kusubiri 2015!.

Nakumbuka ile thread yako na kama unakumbuka, nilijizuia kusema sana.

Kila mpenda demokrasia wa kweli, lazima anaumizwa na kinachoendelea, naamini hata wana CCM wa ukweli, hawaipendi hali hii ya kupewa ushindi wa mezani, lakini Dr, anapaswa kuyapeleka malalamiko yake kunakohusika kwanza, ndipo na aumwage mtama kwenye kuku wengi.

Kwenye kulijadili hili, naombeni ushabiki tuuweke pembeni, tutangulize maslahi ya taifa.

Kuna kosa gani kwenye kutangazia wanachama wake kinachoendelea?
 
Mwanjelwa: Mheshimiwa Dr. Willbrod Peter Slaa anagombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hagombei Ubunge! Kwa mantinki hiyo hana wajibu wa kuwapigania wagombea Ubunge. Wagombea hao wanaweza kujitetea wenyewe majimboni mwao! Pia wanaweza kutetewa na CHADEMA kama chama na sio Dr. Slaa. Tafadhali epuka kabisa kushusha heshma na hadhi ya Dr. Slaa - Rais Mtarajiwa!! Dr. Slaa andelea kulinda kura zako. CHADEMA, wafuasi wake na Watanzania wenye nia njema kwa nchi yao - endeleeni kumtetea na kumlinda mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA, Dr. Willbrod Peter Slaa mpaka kieleweke! Haya shime WAZALENDO!
 
Ningekuwa uarabuni walai tena ile kazi ya kujitoa mhanga ningeitekeleza.
Wanabahati nimezaliwa na uoga kidogo wa kujitoa mhanga
 
Nimewapata wote hapo nitawajibu kwa pamoja.
Labda kama mtaniona sijui kama mmoja wenu alivyosema au ni namna ya kudai haki, vyovyote vile. Lakini, haikuwa busara hata kidogo kwa mtu wa kiwango chake kuongea kitu alichooongea. Hata kama unagombea roho yako isitoke, huwezi lazimisha roho za wengine pia zitoke!. Ni kiwango cha chini kabisa cha busara kwa mtu kama Dr. Slaa kuongea namna ile. Mnaonipinga hapo juu, je mmeweza elewa kwanini Slaa hajaongelea kuhusu Ubunge wakati kwenye Ubunge ndiyo kuna malalamiko zaidi kuliko Urais? NImemsikia BBC jioni akisisitizia matokeo ya Urais tu, kwanini isiwe Ubunge na Udiwani? Sikutarajia, hamna mtu alitarajia. Nilichodhani mimi, angetuambia sisi wafuasi, tusubiri matokeo kwanza na baada ya hapo twende mahakamani.

Hapa ndipo tumefika watu wanasema TOGETHER we stand, Divided it is time to GO.

Swali dogo: Kama anachosema ni upuuzi SI TUME IKUBALI KUHESABU UPYA MATOKEO ILI UONGO WAKE UDHIHIRIKE????
 
Nadhani wameshapeleka malalamiko yao NEC kwanza kabla leo hawajaongea na wanahabari, nimesoma kwenye Mwanahalisi Marando kasema wameshapeleka malalamiko yao huko lakini kama unavyojua NEC wanaweka pamba masikioni kwasababu wanajua wanachokifanya
 
kwenda huko.Kuna uhusiano gani kati ya kurudiwa uchaguzi/uhesabiwaji wa kura na uchochezi?wewe ndo naona mchochezi,kama unasapot basi wewe si mtanzania na huna uchungu na nchi yetu inayoliwa na mafisadi,mahakamani???????????:nono:
 
Kimsingi anayemwaga damu ni yule anayeiba kura za wananchi akitaka mwananchi achekelee.....katu hatutakubali..Yule ambae alisema atashinda kwa gharama yoyote na kile anachokifanya sasa ndio anamwaga damu....hembu watanzania tuache unafiki na tujaribu kuvaa viatu vya anayerdhulumiwa kabla hujapotosha wananchi....MUDA WA KUPOTOSHANA UMEISHA......Dr slaa yuko sahihi......MAkame atajutia anachokifanya!!!!!
 
Hivi kisheria wakipokea malalmiko mahakama wanweza kusitisha zoezi linaloendelea kabla ya wahuni kujitangaziwa usshindi wa kutengenezwa?. Kama hilo lipo naona lichangamkiwe ili walau tuwe tumejaribu na NEC ionekane kughairi amri ya mahakama!
Just trying.
 
wanajaribu kuzuia maana matokeo yakitangazwa ndio imetoka hivyo
 
Mwanjelwa anaanza ulikua mnafiki.....kama ulikua unamsapoti dr slaa basi acha...mana hata ye hakutaki...kinana jana aliongea upupu wake...kwa unafiki wako ukakaa kimya...hatukuhitaji nchi hiii.....Ukimnyima mtu haki yake maana yake wewe ndo hutaki amani!!!!
 
Mwafrika, kila mwenye macho na masikio, ameyaona na kuyasikia madudu ya NEC kwenye uchaguzi wa mwaka huu, kwa kifupi maroroso ni mengi tuu, lakini kwa vile Dr. Alisaini kuzikubali zile rules of the game, kama ana malalamiko yoyote, angeanzia kuyapeleka kwa refa (NEC) ndipo akaja na vyombo vya habari na hatimaye ayakabidhi kwa umma.

NEC inajua inachokifanya,( kuna posti niliposti kule nyuma kuhusu matokeo ya mwisho, nilitukanwa sana, nikashauri tusubiri nami bado nasubiri) na itaendelea na inachokifanya, Kesho saa 11 jioni, watatangaza matokeo ya mwisho na baada ya hapo hakuna hata mahakama yenye uwezo wa kufanya chochote. Jumamosi Saa 4:00 Uwanja wa Taifa, JK ataapishwa, kitakachofuata ni kusubiri 2015!.

Kila mpenda demokrasia wa kweli, lazima anaumizwa na kinachoendelea, naamini hata wana CCM wa ukweli, hawaipendi hali hii ya kupewa ushindi wa mezani, lakini Dr, anapaswa kuyapeleka malalamiko yake kunakohusika kwanza, ndipo na aumwage mtama kwenye kuku wengi.

Kwenye kulijadili hili, naombeni ushabiki tuuweke pembeni, tutangulize maslahi ya taifa.

Pasco nakumbuka lile bandiko lako kaka!! hakuna demokrasia....Jk ANAFIKIRI KUWA AKISTEP DOWN SIJUI ATAUFA AU HIYO MIAKA MITANO SIJUI NDIO ITAMBADILISHA AWE Mungu
 
nimefuatilia kwa makini sana uchaguzi wa mwaka huu. Nimevutiwa sana kwa jinsi shamra shamra na msisimko mkubwa sana. Hakika tanzania tumekomaa kisiasa na tunaelekea kwema.

Tatizo langu linakuja pale mmoja wa wagombea, hapa namaanisha dr. Slaa kuanza kwa maksudi kabisa kutaka kuanzisha fujo zisizo na maana. Kwa jinsi alivyozipanga points zake kwa kusema kura za urais zisimamishwe na si kura za ubunge nadhani kila mmoja anafahamu kuwa alikuwa anakwepa kuudhi washirika wake walioshinda ubunge. Kwa maana hii tunatambua kuwa janja yake kubwa ni kutaka serikali ya kitaifa iundwe. Mimi nakubaliana na hiyo point, ila approach aliyotumia kwa kweli inanipa wasi wasi kama kweli ana busara na ni mtu aliyekomaa kisiasa.

Kama kiongozi mkubwa si busara kuanza kuchochea ghasia. Hicho kitendo kimenikera sana na sikutarajia kwa kiongozi niliyempa points nyingi sana kabla.

Tusimame kama watanzania. Kama kuna shida na matokeo, tusubiri kwanza then twende mahakamani.
mkunduuu..................................
 
Kwani unaongelea Uchaguzi wa nchi gani? Kama ni huu wa tz basi unaonekana kama mtu aliyezinduka baada ya kuzimia siku nne. Kwamba hujui nini kimetokea tz tangu jmosi iliyopita. Basi ukae kimya usikilize waloshuhudia kilichotokea.
 
Mag3, Sophist, fishyfish wote mna haki ya kusema, aidha niwe coward, mwoga au vyovyote vile mtavyoita, hata siku moja kushindwa na kudai haki violently is never is solution. Ninachokifahamu ni kukaribisha De campo na wenzake na kuishia kutoaminiana baada ya kiongozi wetu kupelekwa pale. Kuna namna tele za kudai haki, na si kuhamasisha watu waingie mitaani. Hata hivyo, ninavyojua kwa nchi hii hakuna mtu atakuwa tayari kuwa chambo. Tuna muda na kama tumeweza kuchukua viti 51 kama wapizani, kwanini tusiweze kuchukua nchi muda ukifika?!

kwa hiyo nyie ndugu niliowataja hapo juu, mawazo ni mazuri kwa kuandika hapa hapa ili kuyajadili na si mazuri kivitendo mtaani. Bahati nzuri hayo mnayoyasema na kuchochea hamjawahi yapata ila kwa kuona kwenye TV. Ni mbaya sana.

Mkuu hapo kwenye red hebu elezea kidogo ni namna gani watanzania wanaweza kudai haki yao baada ya Tume kumtangaza mtu ambae hawajamchagua kwenye nafasi ya uraisi maana wabunge wanaweza kwenda mahakamani, sasa kwa nafasi ya uraisi hebu tupe hiyo namna nyingine ya kudai haki yetu maana ni lazima tuidai
 
Back
Top Bottom