we mwanjelwa mtazamo wako wa mwanzo ulikuwa negative kwa Dr. Slaa wala usitake kujikoshwa kuwa ni Chadema baada ya kupewa live. Ondoka hapa na upuuzi wako
Kama ni busara wewe ndiye huna busara, kwa kuwa hata mambo yaliyo ya hekima na busara wewe bado huwezi kuyatambua. Nina wasiwasi na upeo wako wa kufikiri na kupambanua mambo hasa inapokuja kwenye masuala yanayotoa mustakabari wan chi hii. Na dokta slaa si wa kwanza kuziona kasoro hizo, maana hata waangalizi wa jumuiya ya umoja wa ulaya wametilia shaka mchakato mzima wa uhesabuji kura, ambao unatoa mwanya kwa CCM kuchakachua matokeo. Na kama wewe unadhani suala ni kunyamaza kimya, consider yourself a failier, and not only that but a stupid looser kwa sababu unaongea kitu usichokijua, na hata sheria za nchi hujui zina zungumziaje kuhusu matokeo ya uraisi. Watu kama wewe kwa zama hizi wanahesabika kama maadui wa taifa letu, ambalo limeporwa na wana ccm wachache, na wakadhani wana dhaman ya kututawala milele. Wanachokitaka CCM ni maandamano ya nchi nzima ikibidi. Maana hata kura zetu wamezichakachua.
Wote (au wengi) tumesikia alichosema.
Ameomba kura zisitishwe kutangazwa.
Mimi ningeongeza kuwa, matokeo yajumlishwe upya kwa kutumia namba za mwanzo zilizopatikana katika kila kituo na kusainiwa na mawakala wa vyama vyote.
Mafisadi wa ccm mmeanza kubadili mambo (kama kawaida yenu) na kudai kuwa Slaa anataka damu ya watanzania imwagike. Swali rahisi kwenu, kuna uhusiano gani kati ya kusitisha zoezi la kutangaza matokeo na damu kumwagika?
Kama kweli ccm mmeshinda, kwa nini msikubali kura zijumlishwe upya (sio kuhesabiwa upya)?
Nimefuatilia kwa makini sana uchaguzi wa mwaka huu. Nimevutiwa sana kwa jinsi shamra shamra na msisimko mkubwa sana. Hakika Tanzania tumekomaa kisiasa na tunaelekea kwema.
Tatizo langu linakuja pale mmoja wa wagombea, hapa namaanisha Dr. Slaa kuanza kwa maksudi kabisa kutaka kuanzisha fujo zisizo na maana. Kwa jinsi alivyozipanga points zake kwa kusema kura za urais zisimamishwe na si kura za ubunge nadhani kila mmoja anafahamu kuwa alikuwa anakwepa kuudhi washirika wake walioshinda ubunge. Kwa maana hii tunatambua kuwa janja yake kubwa ni kutaka serikali ya kitaifa iundwe. Mimi nakubaliana na hiyo point, ila approach aliyotumia kwa kweli inanipa wasi wasi kama kweli ana busara na ni mtu aliyekomaa kisiasa.
Kama Kiongozi mkubwa si busara kuanza kuchochea ghasia. Hicho kitendo kimenikera sana na sikutarajia kwa kiongozi niliyempa points nyingi sana kabla.
Tusimame kama Watanzania. Kama kuna shida na matokeo, tusubiri kwanza then twende mahakamani.
Waislamu oyeeeee, waikristu nendeni mkandamane kanisani tutaonana 2015.
:ban:Waislamu oyeeeee, waikristu nendeni mkandamane kanisani tutaonana 2015.
Waislamu oyeeeee, waikristu nendeni mkandamane kanisani tutaonana 2015.
Taratibu na sheria mbovu zinazotawala muundo wa uchaguzi wa Bongo ndo zinazomfanya mgombea kama Dr slaa kutamka aliyotamka. Ilivyo ni kwamba tume itakapo tangaza matokeo na Rais kutangazwa na kuapishwa hakuna namna iliyopo sheriani ya kupinga matokeo. Hivyo ni vema na bora kwa mgombea wa urais pale anapogundua kasoro za wazi zinazomkandamiza au kumnyima haki kutamka mapema ili utaratibu ufanyike na tume kutafuta ufumbuzi kabla ya kutangaza matokeo.
Mfano mzuri ni chaguzi zilizotangulia huku Unguja. Alipotangazwa Salimini, Karume, na wengine ilikuwa ndo mwisho wa kulalamikia matokeo. hivyo ni bora ukalilia utatuzi wa utata wa wizi wa kura na uchakachuaji ufanyike mapema na tume ili kupata majibu ya kuridhisha kabla ya kutangaza matokeo.
kuna kasoro kubwa zilizojionyesha wazi wazi bila kificho, hii ni pamoja na kupotea kwa kura ndani ya masanduku, kukamatwa kwa wahesab kura wakiwa na shahaa bandia, kutolingana kwa idadi ya wapiga kura za ubunge na urais, kura kuwa nyingi kuliko idadi ya waliojiandikisha.
Ni bora kurekebisha matatizo haya ambayo yamekuwa sugu ktk chaguzi za Taifa letu sasa na kuingiza madarakani viongozi waliochaguliwa kwa ridhaa ya wananchi ili kujenga demokrasia ya haki na usawa, kuliko kumwona Dr Slaa akilalamikia ubovu na kasoro na kuishia kumkosoa na kusema kuwa umefuatilia kwa makini uchaguzi unavyoendeshwa.
Siku zote demokrasia ya kweli hutawaliwa na haki na utawala wa sheria kwa ridhaa ya wavuja jasho ambao ndo wananchi.
Mwanjelwa said:Tatizo langu linakuja pale mmoja wa wagombea, hapa namaanisha Dr. Slaa kuanza kwa maksudi kabisa kutaka kuanzisha fujo zisizo na maana. Kwa jinsi alivyozipanga points zake kwa kusema kura za urais zisimamishwe na si kura za ubunge nadhani kila mmoja anafahamu kuwa alikuwa anakwepa kuudhi washirika wake walioshinda ubunge. Kwa maana hii tunatambua kuwa janja yake kubwa ni kutaka serikali ya kitaifa iundwe. Mimi nakubaliana na hiyo point, ila approach aliyotumia kwa kweli inanipa wasi wasi kama kweli ana busara na ni mtu aliyekomaa kisiasa.
Kama Kiongozi mkubwa si busara kuanza kuchochea ghasia. Hicho kitendo kimenikera sana na sikutarajia kwa kiongozi niliyempa points nyingi sana kabla.
Tusimame kama Watanzania. Kama kuna shida na matokeo, tusubiri kwanza then twende mahakamani.
Mwanjelwa said:Ninachochelea ni ile kauli ya uchochezi
CCM OYEE said:Waislamu oyeeeee, waikristu nendeni mkandamane kanisani tutaonana 2015.
"Ukikuta mahali mawazo ya vijana na wazee yanafanana, ujue hapo pamedumaa" - J. S.Warioba.mabeja said:Huyo Slaa amepoteza dira. Ameona Maalimu Seif ameula na yeye anataka apate umakamu kwa kulazimisha. Asubiri katiba ibadilishwe kwanza ndiyo atapata umakamu. Asitutishie na watanzania hatuko kwenye kumwaga damu. Labda damu yake ndiyo imwagike!!
Nimewapata wote hapo nitawajibu kwa pamoja.
Labda kama mtaniona sijui kama mmoja wenu alivyosema au ni namna ya kudai haki, vyovyote vile. Lakini, haikuwa busara hata kidogo kwa mtu wa kiwango chake kuongea kitu alichooongea. Hata kama unagombea roho yako isitoke, huwezi lazimisha roho za wengine pia zitoke!. Ni kiwango cha chini kabisa cha busara kwa mtu kama Dr. Slaa kuongea namna ile. Mnaonipinga hapo juu, je mmeweza elewa kwanini Slaa hajaongelea kuhusu Ubunge wakati kwenye Ubunge ndiyo kuna malalamiko zaidi kuliko Urais? NImemsikia BBC jioni akisisitizia matokeo ya Urais tu, kwanini isiwe Ubunge na Udiwani? Sikutarajia, hamna mtu alitarajia. Nilichodhani mimi, angetuambia sisi wafuasi, tusubiri matokeo kwanza na baada ya hapo twende mahakamani.
Hapa ndipo tumefika watu wanasema TOGETHER we stand, Divided it is time to GO.
wewe kilaza ni nini kiwango cha busara? busara yako wewe mjinga haiwezi hata kidogo kui-chalenge busara ya werevu,
kama umesoma katiba ungekuwa unajua kuwa tume imepewa mamlaka ya kupitiliza kwa maana ikisha mtangaza mshindi wa urais hakuna kupinga kwa namna yeyote, ndio maana Dr. anapinga before kutangaza ili kwenda sambamba na matakwa ya sheria.
ubunge unaruhusiwa kupinga mahakamani wakati wowote, pia kwa taarifa yako sheria imetungwa kuelekeza mahakama kusikiliza haraka kezi za uchaguzi(ubunge) ccm inatumia mijitu mijinga kama wewe inayodhani ina busara kumbe haina tofauti na mav..., hebu onyesha utofauti wako na nyani basi!!!!!!!!!!!
Kuhakiki kura kila mtu anaunga mkono, kama ni lazima, anyway. Hapa tunaongelea kauli zake za kinazi. Kauli za kichochezi. Kauli ambazo mdomoni mwa mtu wa aina yake, kisiasa, kijamii na kidini, hazikutarajiwa.