mkumbwa junior
JF-Expert Member
- Oct 22, 2014
- 831
- 1,595
Watanzania mnapenda sana udaku na uongo uongo. Mtu kasajili kampuni kihalali, kaomba tenda kihalali, kaipata kihalali, kalipa kodi halali kaingia mkataba halali kautendea haki mkataba wake mpaka upande wa pili ukaridhika na kaondoka kihalali kwa pasipoti na documents zote, mbele ya uwanja wa ndege ulio chini ya jeshi, polisi, uhamiaji na maafisa wa usalama kibao. Sasa hii hadithi katoroka inaanzia wapi? Tafakari. Sio kila jipu ni la kutumbua na hata mtumbuaji anajua. Huu mchezo hauhitaji hasira wala jazba.