TRA na unafiki kuhusu wanufaika na ufisadi wa Escrow

Goliath mfalamagoha

JF-Expert Member
Aug 3, 2012
602
2,505
MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA (TRA) NA UNAFIKI KUHUSU WANUFAIKA WA UFISADI WA ESCROW




Ndugu wananchi wenzangu, mnakumbuka sakata la ufisadi wa escrow uliotekerezwa na viongozi wa umma na kutetewa na wabunge wa CCM na ikulu kuwa haikuwa fedha ya umma.

CHIMBUKO LA ESCROW

Escrow chimbuko lake ni mkataba wa uzalishaji wa umeme dhalura kati ya Tanesco (Shirika la umma) na IPTL uliosainiwa kudumu kwa kipindi cha miaka 20 (1995 hadi 2015)

IPTL ilimirikiwa na Mechmar Engineering ya Malaysia kwa hisa 70% na VIP Engineering ya Tz kwa hisa 30%.

Katika mkataba huo, makubaliano yalikuwa uamuzi wa mwisho wa usuluhishi wa mgogoro utafikiwa na baraza la usuluhishi wa migogoro ya uwekezaji duniani ICSID.

Kumbukeni IPTL haikuweza kukamirisha mradi wa dharula, badala yake ikakamirisha mwaka 1998. Hilo lilikuwa kosa lenye uwezo wa Tanesco kuvunja mkataba.(ila haukuvunjwa, kwanini? Kwa masirahi ya nani?) Tafakari...bila shaka mkono wa mafisadi watawala.

Mwaka 1998 IPTL ililalamikiwa na Tanesco (Shirika la Umma) katika Mahakama ya ICSID kuwa IPTL ilidanganya wakati wa kusaini mkataba na kukuza gharama za uwekezaji, ikaperekea kukuza gharama za uzalishaji umeme.

Mwaka 2001 uamuzi wa ICSID ukatoka ukieleza kuwa ni kweli IPTL ilikuza gharama za uwekezaji kwa kiasi cha Dola 27 Milioni. Hili ni kosa kosa kubwa sana kwa Taifa letu masikini. Hivyo mkataba huo ulikuwa ni "void" na ungevunjwa on the spot kama ingekuwa serikali makini yenye watendaji makini.

Ajabu haijulikani selikari kama ililalamika na kulipwa fidia ya kosa hilo maana hakuna taarifa yoyote kuhusu hilo. Hiyo inaonesha kuna wanufaika wa mkataba huo wa kinyonyaji kwa Taifa letu masikini.

Mwaka 2002 IPTL ilianza kuiuzia Tanesco umeme ila 2004 Tanesco iligundua kuwa IPTL ilidanganya kuhusu mtaji wake.

Ikumbukwe kwa mujibu wa maelezo ya wabunge wa upinzani, IPTL ilidanganya wakati wa kuwa kuomba kandarasi kuwa ilikuwa na 30% ya mtaji sawa na dola 36 Milion na ilikopa 76% ya mtaji.

Baada ya ukaguzi ilibainika kuwa IPTL haikuwa na 36 Milioni bali ilikuwa na dola 50 sawa na Tsh.50,000/- tu wakati huo dola 1=1000/-Tshs.

(Hili ni kosa ktk madili ya mikataba ya kibiashara na ni sifa ya kusababisha IPTL kupoteza sifa ya kutokakulipwa)

Kutokana na kosa hilo Tanesco ikadai gharama ya umeme ishuke kwasababu bei wakati wa kusaini mkataba ilizingatia mataji Dola 36 Milion badala ya Dola 50 tu. Mgogoro kuhusu kushusha gharama za umeme uliendelea hadi 2006.

Mwaka 2006 serikali na Tanesco wakashinikiza kufunguliwa akaunti maalumu(Escrow) ili malipo yawekwe humo hadi mgogoro utakapoisha ili bei sahihi ikiafikiwa ndipo kila upande upate stahiki yake.

Kwahiyo;

ZINGATIA

1. ICSID iliafiki kuwa IPTL ilikuza gharama za mtaji zilizotumika kupata bei ya kununulia umeme.

2. Pesa zilizowekwa kwenye akaunti maalumu ya Escrow hazikutakiwa kutolewa kabla ya uamuzi kufikiwa.

3. Sio sahihi kuwa pesa yote ktk akaunti ya Escrow kuwa ilikuwa ya IPTL ilihali dai la Tanesco la IPTL kudanganya kuhusu mtaji wa uwekezaji halikuwa limeamuliwa na ICSID.

4.Pesa iliyowekwa na Tanesco ktk akaunti ya escrow ilikuwa fedha ya umma kwasababu Tanesco ni shirika la umma.

5. Uamuzi wa kutoa hizo fedha za umma ktk ulitakiwa kuamliwa na ICSID na sio kikundi kidogo cha watu kama ilivyokuwa.

TWENDE MBELE ZAIDI

Mwaka 2008 IPTL ilidhindwa kujiendesha ikawekwa katika utaratibu wa kupokea uwezeshaji wa uzalishaji kutoka RITA ikisimamia gharama za uendeshaji wa Tanesco.

Sept.2013 Mahakama Kuu ilitoa uamuzi wa kesi ya VIP iliyodai IPTL iondolewe chini ya RITA na mali zake zihamishiwe kwa PAP na hivyo PAP wakapewa rights za IPTL.

Ikumbukwe kuwa 2005 IPTL huko Malaysia iliiuzia Standard Chartered Madeni yake na ikawekwa mufilisi.

Feb.2014 ICSID ikatoa uamuzi kuwa IPTL inatoza bei kubwa za uzalishaji umeme na kamuru pande zote zifanye hesabu upya ndani ya siku 90 zilizoiasha Mei 2014.

Kwa mujibu wa hukumu hiyo ingesaidia ni kiasi gani IPTL iliibia umma wa Tz kupita Tanesco toka 2002 hadi 2013.

MAAJABU

1. Ndani ya siku 90 Tanesco na serikali hawakufanyia kazi uamuzi wa Mahakama ya ICSID uliyoipa Tanesco (shirika la umma) ushindi dhidi ya IPTL.

2. PAP ililipwa fedha za Escrow akaunti kwa hukumu ya kesi ya mwanahisa mdogo bila consent ya mwanahisa mkubwa Mechmar.

3. Ikumbukwe kuwa deni la IPTL lilihamua Standard Chartered na limetolewa bila mdai halisi kuhusishwa.

4. PAP inayodai kununua hisa za Mechmar 2010 isingeliwezekana wakati IPTL ilikuwa mnufaika wa RITA 2008 hadi 2013.

5. Mechmar iliyokuwa na 70% y hisa IPTL ilipinga kwa barua kupitia wakili wake iliyoelekezwa gazeti la The Citizen kuwa haikuuza hisa zake kama inavyodaiwa na serikali/Tanesco.

6.Hakuna ushahidi wa hati ya malipo ulioneshwa na PAP kununua hisa za Mechmar ktk IPTL.

Hapo ni kwa ufupi kwa mujibu wa kumbukumbu za maelezo ya Wabunge hasa Kafulila na Tundu Lissu.

UNAFIKI WA TRA

TRA katika gazeti la Mtanzania la 03 April,16 liliandika kuwa Anna Tibaijuka aliyepewa 1.62 Bil Tshs ameamuliwa kulipa 500 Milion ikiwa ni kodi ya mgao alioupata kutokana na fedha zilizochotwa katika akaunti ya escrow.

TAFSIRI YAKE NI NINI?

1.Fedha za escrow ni fedha za umma sio haikuwa zawadi.

2.Uamuzi wa serikali kuwa hizo fedha hazikuwa za umma sio kweli.

Swali.

1. Je, miongoni mwa wanufaika wa mgao wa fedha za escrow ni za Tibaijuka tu ndizo zinatakiwa kulipiwa kodi?

2. Tibaijuka anadai hiyo pesa alipewa kwa ajili ya mchango wa harusi na mambo mengine ya kifamilia kutoka kwa rafiki yake Rugemalila, TRA kudai kodi kunaashiria imehakikisha kuwa maelezo ya Anna T. ni uongo na hizo ni fedha za umma ndio maana wanazifuatilia. Kwanini za wengine walionufsika na mgao TRA haituelezi kwanin haiwatozi kodi?

3. Je, kwanini TRA hawatoi tamko kuhusu msimamo wao waziwazi kuhusu fedha za escrow kuwa ni za umma au la?

4. TRA inatoza kodi kwa mapato halali?

Jibu kama ni ndiyo, je wanufaika wa mgao wa Escrow walifanyia kazi gani PAP?

5. Je, TRA wanaweza kutuambia kwanini wao wako exempted kuripa ushuru?

Au zao haramu?

*Chenge 1.6 Bil
*Rugemalila 75 Bil.
*Ngereja 40.2 M
*D.Yona 40.2 M
*Enos Bukuku 161.7M
*Jaji Luhangisa 404.2M
*P.Kimiti 40.2M
Baadhi tu.
*Prof.Muhongo 1.6 Bilioni

Je, hao walilipwa makaratasi?

6. Jumla ya mgao uliotolewa na VIP Bw.Rugemalila ni 79.726 Bilion

ILA

Fedha iliyochotwa ktk akaunti ya Escrow ni zaidi ya 320 Bilion.

Ukifanya hesabu

320Bil - 79.726Bil
=229.274 Bil.Tshs

Je, TRA mbona haitulezi mnufaika mkuu wa malipo ya fedha 229.274Bil.Tshs za escrow
*Ni nani?
*Yuko wapi?
*Alilipwa na nani?
*Atalipa kiasi gani?
Je, ni malipo halali? Kwa kazi gani?

Nasema huu ni unafiki wa TRA kujitia upofu na kutuona Watanzania tuu mazuzu.iewadanganye ccm wenzao ndio size yao.

Sasa Magufuri ameshindwa kuchukua hatua ktk huu uhuni?

Kumbukeni Standard Chartered iliyonunua madeni ya Mechmar inadai Tanesco USD 258.7 sawa na 438.6 Bil.Tshs Ex.rate y 1:1700

SCB inadai na riba juu ya inayoperekea kiasi hicho deni la SCB kipande hadi zaidi ya Bil.700

Haya yote yanatokana na mikataba ya siri na TRA inatufanya sisi wajinga eti tuwaone serious kudai Tibaijuka kodi ya 500M

Kiukweli, mtu anayeunga mkono ya CCM daima naamini haipendi hii nchi,ana asili ya wizi,unafiki,anakubali rushwa na mbinafsi kupitiliza.

Magufuri bado ameipakata IPTL na madeni yake batili.

CCM haiwezi kufuta ufisadi. Huyo mnufaika mkuu wa Escrow wa 229 Bilion amekumbatiwa na mfumo wa CCM ale peke yake ila madikini muuza nyanya, tikitimaji,dagaa,mamantilie na wengine masikini hohehahe wanatiwa kitanzi cha kodi na TRA ila hao wezi TRA inawaficha. CCM inatesa Watz kupita maelezo na mbaya imewajaza ujinga kwa kuwanyima elimu hata kutambua jema na baya wanashindwa.

Hayo maneno ya kutumbua majipu kusikoendana na matendo ni danganyatoto....Majipu ni ccm na ccm ni jipu kuu.

Serikali ya Magufuri kuendelea kuipakata IPTL na wezi walionufaika na mgao na wengine kupewa vyeo vya uwaziri ndio mjue kuwa CCM imefunga ndoa na wezi na haiwezi kubadiri mfumo unaosababisha kufuta wizi serikalini.

Jiulize hali ya ukosefu wa ajira,mfumuko wa bei,ukosefu wa huduma bora za maji,afya,elimu n.k kisha unaone mtu mzims akitokwa macho anatetea chama chakavu lichojaa wezi, na kimeshindwa kufanikisha kutatua kero hata 1 kwa miaka 50.

Kuna watu wapuuzi sana wanaona fahari kushangiria porojo za kutumbua majipu pasipokuwa na uwazi wa hatua zichukuliwazo kwa wahujumu uchumi.

Yaani ukiona mtu anafurahia kumkamata aliyebaka mpenzi au mke wake utajua kiasi cha ujinga wake.

Utajua kiwango cha upumbavu kwa mtu anayeshangilia kumwona mwizi aliyeiba ng'ombe wake na kuwachinja kisha huyo mwizi kuachiwa....huo ni uzuzu.

Ukimuuliza mwana ccm kuwa ni nani aliyeisha adhibiwa kihalali na kulingana na makosa aliyoyatendea umma ni nani? Wanasema tumpe muda....sasa unachoshangilia ni nini kama sio ujinga?

Ukiwa na madarasa ya elimu hadi PhD, U-Prof. then ukawa mwana ccm lazima akili ina mute kufanya kazi logically.

Endeleeni kuisoma namba, mmeichagua wenywe, mmpenda kitu kidogo wenyewe, CCM ni ile ile.
 
Back
Top Bottom