Ali Kiba ni msanii anayekuzwa kuliko uwezo wake (Overrated)

Babu wa Kambo

JF-Expert Member
May 2, 2016
559
808
Huwa najaribu kusikiliza na kutazama kazi mbalimbali za wasanii hapa Bongo lakini nimegundua kabisa kuna wasanii wengi wanaokuzwa kuliko uwezo wao, na mmojawapo ni Ali Kiba

Huyu bwana mdogo nadhani pengine jina lake lilikuzwa tu kuliko uwezo wake hasa kipindi kile Diamond kaja juu kimuziki, sasa watu walivyo na wivu kimaendeleo wakatafuta njia ya kumshusha wakashindwa, wakatafuta mmabadala wakakosa, mwisho wa yote wakaona wampe jina Ali Kiba kwa matumaini kuwa pengine umaarufu aliojijengea enzi zile ungesaidia kumzima Diamond, japo nayo sijaona impact yake zaidi ya kuzidi kumpaisha dogo Baba Tiffah

Kiukweli ukifuatilia vizuri kazi za Kiba utagundua kazi nyingi ubunifu ni ZERO, hasa siku hizi ndo kabisaa, sasa sijui ni kelele za mashabiki wake ndo zinampoteza, ni papara, au ni kukosa seriousness ama pengine ni "nature" yake tu kwamba si mmbunifu.

Kazi zake kiukweli zinaboa, maana unaweza ukasikia katoa AUDIO nzuri ikija VIDEO boko kabisa inauzima hadi umaarufu wa Audio. In short dogo ni wa kawaida na hapaswi hata kushindanishwa na wakongwe wenzake kama akina Marlow.

Msimpoteze kwa kelele zenu za kumpa jina kubwa asilokuwa nalo, anahitaji menejimenti nzuri, atulie asiwe na papara, awe serious na atulie aangalie kazi za wenzake ndipo pengine anaweza akafanya vizuri, mshaurini hayo, ndiyo ya msingi, kwa kumvimbisha kichwa hamumsaidii
 
Aiseee kuna mijitu sijui ikoje!
Unachotaka kusema wewe ni nini?
Ali Kiba kwa kipaji chake kile unaanzaje kusema 'anakuzwa'?
Mwenyewe alishasema hashindani na mtu maana muziki anaufanya kwa njia zake mwenyewe, muziki wake haufanani na wanaofanya wengine.
Hivi hilo nalo ni la kutia shaka?
Jinga sana.
Tunaomuelewa Kiba na aina yake ya muziki tupo, humuelewi shut up.
 
Waambie hao vibaraka wa domo ndo maana , hao ndo watu wasojua muziki mzuri ni nini wanafuata mkumbo ,
 
Huwa najaribu kusikiliza na kutazama kazi mbalimbali za wasanii hapa Bongo lakini nimegundua kabisa kuna wasanii wengi wanaokuzwa kuliko uwezo wao, na mmojawapo ni Ali Kiba

Huyu bwana mdogo nadhani pengine jina lake lilikuzwa tu kuliko uwezo wake hasa kipindi kile Diamond kaja juu kimuziki, sasa watu walivyo na wivu kimaendeleo wakatafuta njia ya kumshusha wakashindwa, wakatafuta mmabadala wakakosa, mwisho wa yote wakaona wampe jina Ali Kiba kwa matumaini kuwa pengine umaarufu aliojijengea enzi zile ungesaidia kumzima Diamond, japo nayo sijaona impact yake zaidi ya kuzidi kumpaisha dogo Baba Tiffah

Kiukweli ukifuatilia vizuri kazi za Kiba utagundua kazi nyingi ubunifu ni ZERO, hasa siku hizi ndo kabisaa, sasa sijui ni kelele za mashabiki wake ndo zinampoteza, ni papara, au ni kukosa seriousness ama pengine ni "nature" yake tu kwamba si mmbunifu.

Kazi zake kiukweli zinaboa, maana unaweza ukasikia katoa AUDIO nzuri ikija VIDEO boko kabisa inauzima hadi umaarufu wa Audio. In short dogo ni wa kawaida na hapaswi hata kushindanishwa na wakongwe wenzake kama akina Marlow.

Msimpoteze kwa kelele zenu za kumpa jina kubwa asilokuwa nalo, anahitaji menejimenti nzuri, atulie asiwe na papara, awe serious na atulie aangalie kazi za wenzake ndipo pengine anaweza akafanya vizuri, mshaurini hayo, ndiyo ya msingi, kwa kumvimbisha kichwa hamumsaidii
HUYU DOGO HATA KWENYE 20 BORA BONGO HAYUMO SIJUI KWA NINI ANABEBWA BEBWA
 
Ndugu mtoa maada, mtu hakatazwi kuwaza ila anakatazwa kuongea coz si kila utakachoongea ni muhimu vingine ni pumba kama unazozitoa. Alikiba mwenyew kasema hashindani na mtu ( nyie ndio mnaochochea high zisizo na maana kwa wasanii) kila msanii anaplay part yake katika muziki, kwa wapenda maendelea tunachoka sasa always mond na kiba utafikiri wanabifu vile. Mda mwingine kama hamna vya kuongea muwe mnakaa kimya tu
 
Back
Top Bottom