Pipi mboga
Member
- Apr 18, 2016
- 5
- 0
Mzee Yussuf ni miongoni mwa wasanii ambao hawaamini kama Diamond na Ali Kiba wana beef kutokana na wawili hao kutokutana pamoja na kuonyesha tofauti zao.
Akizungumza Jumamosi hii, Mzee Yussuf amesema beef ya Diamond na Ali Kiba zinakuzwa na mashabiki lakini sio beef kweli.
“Mimi Ali Kiba na Diamond sidhani kama wana beef kweli,” alisema Mzee Yussuf. “Bado siamini kwa sababu ni watu ambao hawakutani tukaona kama kweli ni beef kweli zikapigwa ngumi watu tukaona,”
Aliongeza, “Kwenye taarab kuna beef za kweli, watu wanazipiga kweli. Mimi naamini wanaume hawanuniani,”
Katika hatua nyingine Mzee Yussuf amesema anajipanga na wasanii wenzake kuanzisha umoja wa wasanii wa taarab ili na wao waweze kupeleka kero zao kwa pamoja.
Habari kutoka Udaku News