Ali Kiba atikisa Tabora na Unforgettable Tour

Ali Kiba atikisa Tabora na Unforgettable Tour

ormystatus

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2019
Posts
262
Reaction score
464
Msanii Alikiba amefanya tamasha lake la Alikiba Unforgettable Tour, ambalo ni sehemu ya kuazimisha miaka yake 17 kwenye muziki, na ameanza Tabora usiku wa kuamkia leo Desemba 1, 2019 kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.

Alikiba akiwa na wasanii wote wa Kings Music walipanda jukwaani na kuachia burudani kwa kuimba ngoma moja baada ya nyingine, ambapo Alikiba alipanda na Cinderella na kumaliza na ngoma yake mpya inayofanya vizuri kwa sasa ‘Mshumaa’.
ALIKIBAAAAA.jpg

Baaada ya kupiga show kwa takribani masaa mawili alimkaribisha msanii Abdu Kiba, ambaye naye alipiga show kali kisha akawainua wasanii wa Kings Music Cheed, Killy na K2GA, ambao walipigiwa shangwe kubwa na wakazi wa Tabora waliofurika uwanjani.
ABDUUA.jpg

Baadaye Alikiba alirejea jukwaani tena akamtambulisha msanii mpya wa Kings Music Tommy Flavour, kisha akaweka wazi kuwa ngoma ya Tommy inayokuja humo ndani ameshirikishwa yeye.
KINGS%2012.jpg

Alikiba Unforgettable Tour inapewa nguvu na East Africa Television na East Africa Radio, ambapo mbali na tamasha, Alikiba anafanya shughuli mbalimbali za kurejesha kwa jamii ikiwemo kutoa vifaa tiba pamoja na mahitaji kwa wagonjwa kwenye hospitali ya mkoa wa Tabora.

Chanzo: Bongo5
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] unforgettable tour
 
Hilo jukwaa sasa 😀😀

Safi lakini mdogo mdogo tu nae atafika.
 
Naona watu walitaka waone kama lile lililoporomosha mtu Shinyanga.
Anyway, alicjoganya ni kizuri hasa hicho cha kurejesha kwenye jamii(haijalishi ni kiasi gani)
 
jina la tour na uhalisia wa tour ni mbingu na ardhi, mwambieni aendelee kujifunza zaidi atafika tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom