Ali kiba afunguka baadhi ya wasanii kumfuata Director wake

Lord Diplock MR

JF-Expert Member
Mar 16, 2015
1,393
3,234
Alikiba afunguka wasanii walio mfuata Director wake

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Alikiba amefunguka kuhusu baadhi ya wasanii kumpigia simu Director wa wimbo wa Toto kwa ajili ya kuyataka material ya wimbo huo.
Kiba amesema hayo wakati anafanya mahojiano na kipindi cha Playlist kinachoruka Timesfm baada ya kuulizwa, kuwa kuna baadhi ya wasanii walisemekana kumpigia simu director wa Toto ni kweli?
” Ni kweli kuna watu walimpigia simu Director ni kitu cha ajabu sana na sikufurahishwa nacho, kwanza sio mara ya kwanza kuna director niliwahi kugombana nae na tukaacha kufanya kazi naye kisa aliwapa watu fulani material ya wimbo wangu” alijibu Alikiba
” Wanachukua nyimbo zangu wanasikiliza sijui wanataka nini na najua kuna sehemu fulani wamechukua wimbo wangu fulani na hiki kitu kinaniumiza sana sipendezwi nacho kabisa, nampongeza sana Manwalter kwani hajawahi kumpa mtu yoyote wimbo wa mtu mwingine aisikilize yuko profesional sana, kwani hawezi kutoa material ya mtu hata umpe nini” aliongezea kusema.
 
Wimbo wa Toto sijasikia hata bodaboda waupige huo au umetoka jioni ya leo
 
Wimbo wa Toto sijasikia hata bodaboda waupige huo au umetoka jioni ya leo

Inamaana mama angu mpaka upande bodaboda ndio upate nafasi ya kusikiliza mziki!!!!

Ni pm,kwangu nina sabufa,natumia earphone nasimu ya tekno,tv yangu ina king'amuzi moja kwa moja kwaiyo wasafi tv na clouds unaona muda wowote,nina memory card ya 2gb nimejaza ngoma zangu za singeri,nikiiweka kwenye ile sabufa majirani wote wananifata na kunipigia magoti huku wakilia ooh pliizi mkorintoo donti kili azi wiss big sound.
 
Hiyo ndo gia ya kutongoza au?
 
Nyimbo mara nyingi ni mali ya Producer.
Sema ma- producer wa bongo ni wauza beats, wengi hawafahamu wimbo ni mali yao, siyo ya Mwimbaji.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom