Alhamisi nitafunguka-Lwakatare

Alhamisi nitafunguka-Lwakatare

Status
Not open for further replies.

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Wilfred Lwakatare amesema atatoa ya moyoni siku ya Alhamisi.

Akizungumza na waandishi wa habari wa ndani na nje ya nchi mara baada ya kupata dhamana aliomba subira kwa watanzania kwani anayo siri nzito moyoni.

Lwakatare alisema anawaomba waandishi wa habari watulie kwani anatarajiwa kuzungumza kwanza na viongozi wake wakuu wa chama na jopo la wanasheria wake nguli ndipo azungumze na dunia.

Wakati hayo yakiendelea mtandao wa You Tube unamuonyesha Naibu Katibu Mkuu CCM Mwigulu Nchemba akitamba kwenye kampeni za udiwani Arusha kwamba ndiye aliyegharamia vifaa vyote vilivyotumika kumrekodi Lwakatare na hatimaye mateso yote yaliyomfika Lwakatare.

Viongozi wakuu wa Chadema tayari wameelezea furaha yao baada ya Lwakatare kupata dhamana.Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe yuko Dodoma katika vikao vya bunge wakati Katibu Mkuu Dr Wilbroad Slaa yuko kwenye ziara ya kichama barani Ulaya.Katika salamu zake jana alizozitoa akiwa Ujerumani Dr Slaa alimpa pole Lwakatare na hapo hapo kuelezea furaha yake na ya watanzania wanaoishi Ujerumani kwa Lwakatare kupata dhamana na kuweza kuungana na familia yake tena baada ya mateso ya miezi mitatu.

Source:Tanzania Daima.

Updates...

Kutokana na ushauri kutoka kwa wanachama wa Chadema mkutano wa leo umeahirishwa.Hii ni kutokana na bajeti ya serikali inayotarajiwa kusomwa leo Dodoma.Hii ni kuwapa watu fursa ya kuelekeza macho na masikio Dodoma.
 
Kama ametoka mahabusu atulie tu na familia yake. Kuropoka kutamfanya apate majanga mapya kabisa.
 
Jela inamsubiri na kwa muda huu ambao yupo nje kwa dhamana ningewashauri wananchi kuchukua tahadhari ili wasing'olewe kucha na kumwagiwa tindikali.
 
Think vice versa bro,hizo tuhuma ni za Mwigulu SAVIMBI na Amekiri huku akitamba kwa kumtembeza mhanga wake wa Tindikali.
 
Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Wilfred Lwakatare amesema atatoa ya moyoni siku ya Alhamisi.

Akizungumza na waandishi wa habari wa ndani na nje ya nchi mara baada ya kupata dhamana aliomba subira kwa watanzania kwani anayo siri nzito moyoni.

Lwakatare alisema anawaomba waandishi wa habari watulie kwani anatarajiwa kuzungumza kwanza na viongozi wake wakuu wa chama na jopo la wanasheria wake nguli ndipo azungumze na dunia.

Wakati hayo yakiendelea mtandao wa You Tube unamuonyesha Naibu Katibu Mkuu CCM Mwigulu Nchemba akitamba kwenye kampeni za udiwani Arusha kwamba ndiye aliyegharamia vifaa vyote vilivyotumika kumrekodi Lwakatare na hatimaye mateso yote yaliyomfika Lwakatare.

Source:Tanzania Daima.

mkuu kumbe chanzo cha habari tanzania daima kwa heri mkuu.
 
Jela inamsubiri na kwa muda huu ambao yupo nje kwa dhamana ningewashauri wananchi kuchukua tahadhari ili wasing'olewe kucha na kumwagiwa tindikali.
majeshi ya Lwakatare ndio yalimuua Mwangosi?
 
Jela inamsubiri na kwa muda huu ambao yupo nje kwa dhamana ningewashauri wananchi kuchukua tahadhari ili wasing'olewe kucha na kumwagiwa tindikali.

hujitambui wewe,Mwigulu kapata Aibu sasa anaomba msamaha
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom