Alhad aitaka Serikali kuingilia kati katazo la NEMC adhana, kengele kupigwa dakika mbili

comte

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
8,222
5,946
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum ameiomba Serikali iingilie kati kauli iliyotolewa na Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC), hivi karibuni ya kutaka kengele na adhana katika nyumba za ibada zisizidi dakika mbili kwa kuwa zinachangia uchafuzi wa mazingira kwa kelele.

Akizungumza leo Julai 9, katika Kongamano la siku maalum ya amani katika Maonyesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam, Sheikh Salum amesema ujumbe huo ni wa utovu wa nidhamu na unaweza kuchafua amani iliyopo nchini.

Sheikh Salum ambaye pia ni Mwenyekiti wa Amani mkoa wa Dar es Salaam, amesema kama sheria hiyo kweli ipo basi ibadilishwe kwakuwa inaweza kuchangia watu kukosa uhuru wa kuabudu.

“Kengele au adhana ikilia hata zaidi ya saa kumi si kelele ni moja ya kuabudu Mungu na hili lilikuwapo tangu enzi hizo,” amesema Salum.
 
Kuna makelele yanakera sana hasa ya wale wazee wetu wanaogumia swalaa swalaaaa sasa ni saa kumi kamiliii.

Hizi kelele zinakera sana kwa sababu zinaamsha watu nyakati ambazo bado kuamka.

Kama sisi waislamu tuna adhana mbili usiku.lakini hapo hapo mzee likochopwike anataka kushika maiki aanze kusumbua watu "swalaaaaa sasa ni saa kumi kamiliiiii" ...si upige adhana tu umalize?

Kama kelele hizi za akina mzee likochopwike ambazo ni zao tu kwa hashuo zao basi hizo naona kweli zonakera aisee.

Lakini hata kama wakizuwia adhana basi wazuwie na ile miziki inayopita mabarabarani kutangaza mambo yao ya biashara na mapromosheni mbali mbali.kwa sababu nayo ni kelele pia.

Lakini iwe itakavyo kuwa wasifikie hatua ya kuzuwia ibada,hi hatua waliyofikia ni wao kuzuwia wito wa kwenye ibada.lakini wafanye watakavyofanya wasifikie hatua ya kutuzuwia ibada zenyewe hapo watakuwa wamevuka mipaka kabisa.

Kwa sababu nafikiria ya kuwa hawajakataza adhana bali WAMEKATAZA ADHANA KWA KUTUMIA VIPAZA SAUTI AMBAYO VINAIPAZA SAUTI KUWA JUU,HIVYO WATU WANAUWEZO WA KUADHINI BILA VIPAZA SAUTI NA BADO IKAWA HAKUNA KILICHO HARIBIKA.
 
Pumbavu zake hilo ndiyo ameliona baya. Ya kutekwa watu, kupotezwa kuuawa mbona hajayasemea. Ya Lisu mbona hakutoa kauli. Pumbavu
Kauli mbona zilitoka. Au hujui kuna watu wapo Segerea 6yrs kabla ya hao waliotekwa huku hakuna tamko lolote hadi sasa.
 
Yaani huwa inakera sana ..mimi nimewahi kuishi jirani na nyumba hiyo ya ibada aise ni kero kubwa mnoo mpaka mtu una shtuka usingizini
Kuna makelele yanakera sana hasa ya wale wazee wetu wanaogumia swalaa swalaaaa sasa ni saa kumi kamiliii.

Hizi kelele zinakera sana kwa sababu zinaamsha watu nyakati ambazo bado kuamka.

Kama sisi waislamu tuna adhana mbili usiku.lakini hapo hapo mzee likochopwike anataka kushika maiki aanze kusumbua watu "swalaaaaa sasa ni saa kumi kamiliiiii" ...si upige adhana tu umalize?

Kama kelele hizi za akina mzee likochopwike ambazo ni zao tu kwa hashuo zao basi hizo naona kweli zonakera aisee.

Lakini hata kama wakizuwia adhana basi wazuwie na ile miziki inayopita mabarabarani kutangaza mambo yao ya biashara na mapromosheni mbali mbali.kwa sababu nayo ni kelele pia.

Lakini iwe itakavyo kuwa wasifikie hatua ya kuzuwia ibada,hi hatua waliyofikia ni wao kuzuwia wito wa kwenye ibada.lakini wafanye watakavyofanya wasifikie hatua ya kutuzuwia ibada zenyewe hapo watakuwa wamevuka mipaka kabisa.
 
Miaka ya nyuma nilikaa karibu na msikiti aisee nilikoma makelele ilikuwa ni kero, sasa hivi pia nakaa karibu na msikiti Cha kushangaza sioni kero sauti hainikeri, hainifanyi niamke kama nimelala, nikiwa macho naisikia lkn haina makelele. Sijui tofauti ni nini
 
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum ameiomba Serikali iingilie kati kauli iliyotolewa na Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC), hivi karibuni ya kutaka kengele na adhana katika nyumba za ibada zisizidi dakika mbili kwa kuwa zinachangia uchafuzi wa mazingira kwa kelele.

Akizungumza leo Julai 9, katika Kongamano la siku maalum ya amani katika Maonyesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam, Sheikh Salum amesema ujumbe huo ni wa utovu wa nidhamu na unaweza kuchafua amani iliyopo nchini.

Sheikh Salum ambaye pia ni Mwenyekiti wa Amani mkoa wa Dar es Salaam, amesema kama sheria hiyo kweli ipo basi ibadilishwe kwakuwa inaweza kuchangia watu kukosa uhuru wa kuabudu.

“Kengele au adhana ikilia hata zaidi ya saa kumi si kelele ni moja ya kuabudu Mungu na hili lilikuwapo tangu enzi hizo,” amesema Salum.
Ati sheikh ha ha haaaa, Masufi bana
 
Swalaaa swalaaa amka ukaswali kabla ya kuswaliwa....sasa ni saa kumi kamili..wananikera
 
Hatutaki makelele
Pombe zenyewe siku hzi tunakunywa hku kukiwa kimya
We alhad tulia tu

Ova
 
Back
Top Bottom