ALERT!! BEWARE OF MAFISADI's NEW MOVE | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ALERT!! BEWARE OF MAFISADI's NEW MOVE

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bongolander, Mar 16, 2009.

 1. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Wana JF, najua hii si habari mpya kwenu. Lakini ningependa kuwafahamisha wale wanaotembelea JF mara moja moja, inaonekana hivi sasa kuna desperate attempts kutoka kwenye upande wa mafisadi, za kuleta distraction na kuonesha kuwa kuna mgongano kwenye kambi ya watanzania safi wanaofunua maovu ya mafisadi.

  Alama zote za msumari wa mwisho kwenye jeneza zinaonekana, na mafisadi sasa wanatumia njia ya kuleta confusion na distraction ili ku-divert attention ya issue nzima ya ufisadi, na kuleta kitu kama mkoroganyo na kutoelewana ndani ya CCM, ndani ya upinzani na hata kujaribu kufanya umeme badala ya ufisadi kuwa ndio issue.

  Juzijuzi tumeanza kusikia sauti za wadhaifu na wajinga kutoka ndani ya CCM kujaribu kuwasemea mafisadi, na tumeanza kunusa kitu kama kupenya kwa rupia ndani ya upinzani, na kitu kama kupenya kwa rupia ndani ya media na media kuanza kuwa kama kipofu. Hali hii ambayo haitafanikiwa, inaonesha kuwa kuna desperate move ya mafisadi kuelea 2010 na kujaribu kufika Kisutu.

  Tusikubali distraction, tatizo letu ni ufisadi, Hilo ndio linatufanya tuishi kwa taabu na tuonekane kama nchi ya wajinga, na tuonekane kama watu cheap ambao tunaweza kununulika kirahisi.

  TUSIPOTOSHWE, na tuwakumbushe wengine kuwa hii ni janja tu.
   
 2. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mkuu Bongolander......kuna point ya muhimu sana katika post yako! Ni kweli kabisa na attention na fights vinataka kuhamia kny mambo ya ajabuajabu ambayo mimi pia naamini si mambo ya kipaumbele kny mijadala na mapambano yetu!

  Badala ya kukomalia wanaotuhumiwa kufisadi nchi yetu kupelekwa mahakamani na waliopelekwa tayari kesi zao sifanyike mapema, naona watu wankuja na hoja za eti, CHADEMA yagawanyika, CCM yameguka, or CUF sijui imefanya hiki na kile...of course kwangu mimi hizi naziona kama ni maigizo kuelekea 2010! Tusipokuwa makini tutajikuta tunapoteza muda mwingi kujadili hizi ''issues'' zinazopenyezwa na mafisadi ilikutupotezea attention ya mijadala mahususi na tutakuja kustuka 2010 mafisadi wanatupiga mweleka kwa kuingia /kurudi bungeni kwa ''KISHINDO'' kama walivyozoea kuita wao wenyewe!

  Naungana na Bongolander kuwaomba wadau wasipoteza mwelekeo katika kujadili ajenda za mushimu hasa wakati huu tunapoelekea kny uchaguzi wa serikali za mitaa 2009 na ule mkuu 2010.
   
 3. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  why hit around the bush?

  mnajua tatizo la mindset za wanaofrequent JF ni ushabiki wa kisiasa Period! formula ya majadiliano humu imekaa hivi:

  CCM wote ni Mafisadi

  JK hajali chochote

  FREEMAN MBOWE ni Mungu mtu hivyo huwezi kumcriticise na ukifanya hivyo unaambiwa jadili issues

  REGINALD MENGI (same as above) japo media zake hazina objectivity yoyote ile

  CUF hawa ni ruksa kuwa criticize

  NEWS: hakuna kipya zaidi ya ku kocopy and paste yale yale yaliyoandikwa kwenye udaku asubuhi

  SCANDALS: hizi kama zinamhusu kipenzi cha JF basi lazima ziwe sources

  "CONTROVERSIAL" THREADS: be advised kuwa hivi huwa zinahamishwa ili zisiwa offend wahusika

  LEAKED DOCS...siku hizi hazimo tena....unless once in a while

  halafu mntasema kuna conspiracy ya Mafisadi!
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  tatizo ni kuwa wapo mafisadi ambao nao wanajifanya kuwapiga vita mafisadi
   
 5. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #5
  Mar 16, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Sina cha kuongezea.
  Asante GT...
   
 6. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #6
  Mar 16, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mkuu,

  Vipi kundi la pili ambalo kila kitu linalia ufisadi hata pale wanapokuwa challenged kwenye mambo ya ukweli?

  Ukiwambia mbona hutimizi ahadi zako ulizoahidi? Oohh! umetumwa na mafisadi.

  Mbona hapa mambo yako yanaonyesha yana utata? Oohhh! umetumwa na mafisadi.

  Ufisadi sasa umegeuka mtaji wa kisiasa.

  Unataka Watanzania wote tuamini tatizo la Tanzania ni ufisadi tu? Sio kweli mkuu, Tanzania ina matatizo mengi ambayo lazima yapiganiwe kwa pamoja. Ufisadi ni tatizo moja tu katika matatizo makubwa kama kumi hivi.

  Leo hii hata ufisadi ukome kwa asilimia 100, bado Tanzania itaendelea kuwa maskini. In fact wakati wa Nyerere pamoja na kutokuwa na ufisadi bado nchi yetu ilikuwa maskini.

  Tusiwe na akili finyu ya kufikiri matatizo yetu yanasababishwa na jambo moja. Tuangaze huku na kule na kupambana na matatizo yote kwa pamoja.

  Jambo muhimu kuliko yote liwe kuwasaidia wananchi wetu kupambana na adui wetu wakuu ambao ni ujinga, maradhi na umaskini. Vita dhidi ya ufisadi iwe ni silaha mojawapo tu katika kutimiza hilo lengo.

  Pia ufisadi hauna chama, dini wala ukoo. Tuna mafisadi kutoka kila angle na kila jamii ya Tanzania ikiwemo JF. Kuna watu wanatoka kuandika vijembe hapa kisha wanaenda kunyanyasa Watanzania humo kwenye maofisi yao ambayo wamepewa madaraka ya kutuhudimia wananchi. Kama tunapambana na ufisadi kwa kufuata itikadi za siasa au dini, sisi wenyewe tunageuka na kuwa waendelezaji wa huo ufisadi.
   
 7. I

  Ijabu Issa Member

  #7
  Mar 16, 2009
  Joined: Apr 29, 2008
  Messages: 56
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu, umeongea mazito ya kuzingatia. Nilishtushwa sana jana na simplicity ya baadhi ya wanaJF kukumbatia kwa urahisi na haraka bila kujiuliza maswali taarifa za kichochezi zinazoibuliwa na Mtanzania, jarida la propaganda la fisadi Rostam Aziz, kuhusu mtu muhimu sana katika mapambano dhidi ya ufisadi, Dk. Mwakyembe. Ati "Dk. Mwakyembe aumbuliwa!" Kisa ni nini? Gazeti linasema Dk. Mwakyembe na wenzake wanane wana kampuni ya umeme! So what?

  Ukisoma the whole story, unagundua kampeni ya kumsafisha Lowassa kuwa alionewa na Dk. Mwakyembe ambaye, kwa maoni ya gazeti hilo la Rostam, pia ni fisadi kwa kuwa amediriki kuwa na kampuni ya umeme! Rubbish! Kwa kuwa Dk. Mwakyembe na wenzake wamediriki kuwa na kampuni, basi ni halali kwa Serikali kununua mtambo chakavu wa kampuni ya Rostam Aziz, DOWANS! Nonsense! Kinachonisikitisha sana ni baadhi yetu kuwa carried away na cheap propaganda kama hizo na kupoteza the big picture. Kinachonisikitisha zaidi ni kuona wanasiasa tuliowaamini, akina Zitto Kabwe, na magazeti muhimu kama Tanzania Daima, kukumbatia mafisadi at zero hour kwa kisingizio cha kijinga ati "national interest"! Hivi kweli Zitto anaziona national interests kwenye biashara za Rostam, Somaiya, Shubash Patel, Yusuf Manji na siyo kwenye misimamo madhubuti ya akina Samuel Sitta, Ole Sendeka, Dk. Mwakyembe, Anne Kilango, Selelii?

  CHADEMA wana serious problem kama CCM, ya kuwa na mamluki ndani ya chama. Wanasiasa makini ndani ya CHADEMA kama Dk. Slaa, John Mnyika, Halima Mdee, Ndesamburo, Arfi n.k wamwangalie kwa makini Zitto na ashki yake ya kupenda pesa kupindukia. Sijafurahishwa na taarifa kutoka BRELA kuwa kijana huyo, badala ya kuungana na wezake kwenye Operesheni Sangara au kuwa jimboni kwake ambako hajaonekana kwa muda mrefu, alikuwa Dar on Rostam's assignment akihaha kutafuta nyaraka BRELA ati kummaliza DK. Mwakyembe! Sisi wengine tunasema, anajimaliza mwenyewe!

  Nakushukuru Mkuu, Bongolander, kulileta hili hapa. Nimeangalia magazeti ya leo na kukuta kuwa story waliyoianzisha Rostam na Zitto kwa lengo la kumbomoa Dk. Mwakyembe, haijaitikiwa na magazeti mengine. Aidha, taarifa ya jana ya Tanzania Daima kuwa Dowans Tanzania Ltd inamilikiwa na Brigedia Mstaafu wa Jeshi la Oman kwa jina la Sulaiman Mohammed Yahya Al Adawi, zimezua maswali mengi ya msingi ambayo huenda yakaua kabisa credibility ya Tanzania Daima:
  (i) Kama Al Adawi ndo mmiliki wa Dowans Tanzania Ltd, mbona MEMARTS za kampuni hiyo zilizoko BRELA hazina jina hilo wala sahihi yake?
  (ii) Mbali na Dowans Tanzania Ltd, ni nani mmiliki wa Dowans Holdings SA iliyorithi rasmi mkataba wa Richmond?
  (iii) Baadhi yetu tumewasiliana na Al Adawi kwa anuani ya barua pepe hii: hana.radhi.6700_1@commerce.gov.bh na tumegundua mengi yasiyoweza elezeka hapa. Tanzania Daima walitumia barua pepe ipi?
  (iv) Upo uvumi kuwa barua pepe hiyo iliyofanyiwakazi na Tanzania Daima iliandikwa na Rostam Aziz mwenyewe. Ikiwa huu ni uvumi tu, mwaga hiyo barua pepe hapa!
  (v) Mwaka juzi, kwenye ulingo huu huu wa JF, (tarehe 2 Juni, 2007 saa 8.47 mchana) Field Marshall ES alituleza kuwa mmoja wa wamiliki wa hisa za Dowans Holdings SA ni Suleiman Mohammed Yahya Al Adawi, raia wa Falme za Kiarabu. Kwa Tanzania Daima Jumapili kudai kuwa "Siri ya Dowans yafichuka" na kumtaja Al Adawi, ilikuwa na maana gani wakati wana JF tunajua hilo toka mwaka 2007?
  (vi) Tanzania Daima ina uhakika kuwa huyo jamaa kweli ni bilionea, ni Jenerali mstaafu na kwamba ni raia wa Oman au gazeti lilielezwa tu kuandika wasichokijua?
   
 8. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #8
  Mar 16, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Ijabu Issa, naomba kama utaweza kuhamisha comments zako kuhusu mmiliki wa Oman katika thread niliyoanzisha kuhusu AlAdawi ili data zote ziwe sehemu moja kuhusu huyu jamaa wa Oman.
  Ila mkuu naomba nikupe tano zote maana hata mimi ili nipa wasiwasi kile ki-article cha Tanzania Daima.
   
 9. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #9
  Mar 16, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280

  Mkuu ndio kusema tupo kwenye vicious cycle tayari!
   
 10. M

  Mkereme JF-Expert Member

  #10
  Mar 16, 2009
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 251
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Poleni sana Wanakijiji. Tatizo kubwa hapa ni kwamba pamoja na kusemwa kote ndoa ya akina Lowasa .Kikwete na Rostam and Co.LTD ni ya KIKRISTO haina talaka mpaka kifo kiwatenganishe. Ufisadi walianzisha day one baada ya Marehemu Julius Kambarage Nyerere kuwaumbua kwenye mchakato wa uchaguzi 1995 mwenye kubisha aendelee tu. Tanzania Daima hawana hata aibu kuleta hadithi hapa. As I said wa-Tz asilimia 85 hawapendi kusoma I mean hawajui kusoma they simply rely on the word of mouth. Tangu ianzishwe UPE elimu has been going down at cosmic speed na bado mtaona. CCM iko siku watajibu nina usongo kweli kama Mkapa na Kikwete waliridhia eneo la Chuo Kikuu pale mlimani pajengwe maduka badala ya maktaba na maabara plus hostels then maana ya uwekezaji CCM wote Alfu kwa kijiti sina muda wa kupoteza na watu hawa, Nahene !!!!
   
 11. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #11
  Mar 16, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu unachosema sio uongo, na kuna uwezekano mkubwa kuwa ujunga huu wa sisi kutosoma na kupenda kusikia ya kuongewa ndio umetufikisha hapa. Lakini kwa kuwa kuna wanaosikia basi wewe na wengine inabidi mtoe mchango kwa kuwafanya wengine wasikie. Kila mtu anatakiwa ku-play part kwenye vita hii kwa analoweza.
  Siku zote wanaopenda kuhodhi madaraka ya dola wanatumia njia ya kuwafanya wengine wajinga(kuwapa elimu ya kujua na kusoma tu) ili waendelee kuwarubuni.
   
 12. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #12
  Mar 16, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,187
  Trophy Points: 280
  Wengine hili tuliligundua mapema - kuna mgongano tena si kidogo. Wazungu husema "you cant eat your cake and have it" Kwenye chama kilichooza kama CCM, huwezi kubaki humo na ukaendelea kujiita msafi, period. Kwamba kuna wapiganaji wa kweli ndani yake, wanakaa na mafisadi kwenye vikao, wanakula lao, wanalala nao na wanakubaliana na kushirikiana nao, ni tusi kubwa kwa wapiganaji wote wa kweli.

  Iliyoshikwa pabaya ni CCM na inatumia kila aina ya silaha kujilinda. Wote wale tunaowashuku kwa ufisadi, salama yao iko ndani ya CCM na siyo nje ya CCM. Ufisadi wote uliofanyika kwa namna moja ama nyingine umewezekana kwa baraka na manufaa ya CCM na viongozi wake. Juzi wabunge wa CCM wameombwa kutanguliza maslahi ya chama badala ya taifa - ni shujaa gani ndani ya CCM amethubutu kupingana na hoja hii ?

  Hao wanaoitwa wadhaifu(?) na wajinga ambao wamejaribu kuisemea CCM, wamechukuliwa hatua gani kichama ? Sana sana tumeshuhudia waoga na wanafiki waliojaribu kupiga kelele wakikunja mikia kutokana na rungu la chama na hoja zao kuzimwa. Unakumbuka vikao vya wabunge wa CCM ? Je ni kwa sababu wanapenyezewa rupia ? tukubali tusikubali mafisadi ndani ya CCM wana nguvu kubwa na ni wajanja sana - ndio maana wanapeta humo.

  Mtaji mkubwa wa CCM ni ujinga wetu na umasikini wetu na vyote vimesababishwa na kulelewa na fisadi CCM. Tunaishi kwa taabu na hivyo rahisi kununuliwa - wakati mafisadi wamekamata mpini, wanyonge tumeshika makali. Ni aibu kuwa wakati tunaanza kuamka na kuhoji mambo mbali mbali, kuna wanaotaka tumeze mzima mzima mbinu za laghai kwenye mapambano. Nani alijua kuwa Mh. Zitto angeweza kuchukua msimamo kama alochukua, sembuse tunaowaona mashujaa ndani ya bonde la kashfa.

  Hakika tusipotoshwe, lakini na nani ? Bahati nzuri ni kuwa kumbu kumbu ndani ya JF zipo na unahitaji muda kidogo upitie post mbali mbali, utashangaa na misimamo iliyotolewa kwa nyakati tofauti. Utetezi unatolewa kwa watu, chama au serikali kwa kutanguliza zaidi itikadi na maslahi binafsi. Ni wachache wanaotanguliza maslahi ya taifa na kuwa tayari kumkoma nyani yeyote yule bila kujali jinsia, dini, rangi, itikadi, wadhifa au umri - lakini wapo.
   
 13. M

  Mwan mpambanaji JF-Expert Member

  #13
  Mar 16, 2009
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 468
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Nashindwa kujua kama Taifa tunaenda wapi,,ni kweli Mkuu Bongolander unayoyasema na naunga mkono 100%,ila tatizo letu ni kubaki tukilalamika badala ya kuchukua hatua za kuwakataa kwenye uongozi wetu wote yeyote yule anayehisiwa kuwa fisadi au kuwa na harufu ya ufisadi.Sina hakika ila inawezekana hata hapa JF wenye shahada za kupigia kura ni wachache,ila kwa kulalamika wapo wengi,sasa lazima tufike mahali tuanze kuchukua hatua,na hili liwe swala la mtu mmoja mmoja,lazima kila mmoja wetu awajibike tuwaondoe katika sanduku la kura,vinginevyo jitihada zozote bila matendo ni kama kilio cha samaki."Inawezekana timiza wajibu wako"
   
 14. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #14
  Mar 16, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kaka inaelekea unajua sana kazi ya propaganda.

  Ni wazi hapa unaendeleza strategy ya kuua ndege wawili kwa jiwe moja. Yaani kumjeruh/kummaliza kisiasa Zitto kama kiungo muhimu cha kupambana na UFISADI ndani ya kambi ya UPINZANI na wakati huohuo kujitahidi kulinda uhalali wa CCM miongoni mwa jamii kwa kuwatumia hawa unaojaribu kuwaonyesha kama ndio vinara wa MAPAMBANO dhidi ya UFISADI wakati inajulikana wazi kuwa karibuni wote wana historia ya KUJENGA,KUTETEA na KULINDA mfumo FISADI na ndio maana wanaongelea yake tu waliyoruhusiwa na sio yale mengine kama KAGODA, NSSF, PPF, DEEP GREEN na mengine mengi ambayo wanahusika nayo moja kwa moja.

  Hapa naongelea hao unaodai kuwa wana MSIMAMO MADHUBUTI akina Samuel Sitta(aliyekuwa kinara wa utekelezaji wa sera za UBINAFSISHAJI na UCHUKUAJI mlizoita UWEKEZAJI), Ole Sendeka(bingwa wa kupokea MGAO wa TANZANITE kutoka kwa Tanzaniteone na kuhonga wazee wa kimasai kuwapambanisha katka siasa za kikoo ili kulinda maslahi ya CCM), Dk. Mwakyembe(Utetezi wa MAUAJI ya Unguja na Pemba ya January 27 na UMAMLUKI wake kisiasa ukiachilia sifa aliyekuwa nayo plae MLIMANI), Anne Kilango (hapa naweka heshima kwa FMES), Selelii(Huyu sina noma naye na naamini ana nia njema miongoni mwa kundi lake) kama ulivyowataja na kusahau wengine kama yule FISADI wa kimaadili na kiuchumi KIMARO na Mzee Shelukindo aliyekuwa mratibu mkuu wa sera za UBINAFSISHAJI kama Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu na baadaye mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma iliyokuwa ikibariki UWEZESHAJI WA MFUMO FISADI.

  Unajaribu kwa ufanisi mkubwa kumuunganisha Zitto na kina Rostam, Somaiya, Shubash Patel, Yusuf Manji. Hivi ukiondoa hili la mjadala wa manunuzi ya mitambo ya DOWANS ambayo mnadai kuwa Zitto alikuwa napigia debe ni wapi ambapo Zitto amehusika na biashara za kina Somaiya, Shubash Patel, Yusuf Manji? Hivi sio Zitto aluyekuwa mstari wa mbele kupigia kelele wizi wa NSSF na Manji? Hivi sio serikali na CCM ndio wanufaikaji mkubwa wa misaada/rushwa za kina Rostam, Subhash Patel na Yusuf Manji. Ama unataka kuwasahaulisha watanzania kuwa ni Katibu Mkuu wa CCM ndiye aliyekuwa akimpigia debe waziwazi hili teja lenu MANJI kuwa mbunge wa Kigamboni? Ni lini hawa jamaa wamewahi kumfadhili Zitto na sio huo mfumo FISADI mnaoufanyia kazi hapa.

  Unataka kutumia huu mnaona kuwa ni mwanya kwenu kuwagombanisha CHADEMA. Using the naming and shaming strategy mliyozoea. Eti leo Mzee Ndesamburo yule mliyekuwa mkimwita sultan wa maslahi ya wachaga CHADEMA na kumtumia kuhalalisha propaganda ya kuwa CHADEMA ni chama cha wachaga sasa leo ameshakuwa mtetezi wa maslahi ya watanzania. Tayari mmeshakimbilia kutumia nafasi hii kama ilvyokuwa wakati ule wa UTEUZI WA KAMATI YA MADINI na baadaye masuala na kifo cha Marehemu CHACHA WANGWE kuwapambanisha CHADEMA. Mnashindwa kulearn kuwa watanzania na hata CHADEMA wameshakomaa na siasa za Tanzania kiasi ya kuwa imara kung'amua propaganda hizi za kulinda MFUMO FISADI mliosadifu, kuulinda na kuutetea kwa janjajanja zenu ambazo zinaonyesha kugonga mwamba kila kukicha. Eti leo unajidai kuwa ulikuwa ukimwamini Zitto kwa lipi? Kuhatarisha mfumo wa KIFASADI mnaoulinda na kuukuwadia kila kukicha?

  Kuhusu utetezi wako kwa Mwakyembe. Mimi hapa kila mara nimekuwa nikiongelea hulka ya UMAMLUKI wa Kisiasa wa Mwakyembe katika kulinda na kutetea MFUMO FISADI na pia hatari za watanzania kulishwa kasa la MASIHA FEKI. Mwakyembe alitumia mwanya wa Wanakamati wa Kamati ya Mahesabu ya Mashirika ya Umma kupokea POSHO haramu za TANESCO kuhalalisha propaganda yake kuwa msimamo wa kamati na hata Zitto kuwa unatokana na POSHO ama hongo hiyo huku akijua wazi msimamo wa Zitto dhidi ya utamaduni huo haramu wa POSHO katika kamati za bunge. Wakati huohuo Mwakyembe hajawahi kusimama iwe ndani ya Kamati yake ya Madini na Nishati na wala bungeni kupinga utamaduni huo. Hajaweza kusema kama yeye binafsi ama Kamati yake ambayo yeye ni makamo mwenyekiti wameacha kupokea POSHO hizo kwa makampuni ama mashirika wanayokutana nayo. Sasa limekuja swala la umiliki wake wa kampuni ya nishati. Hapa ndipo tunaposema tuwe makini na MASIHA FEKI hawa na usanii wao ulokubuhu. Yeye kama Mbunge alipaswa kisheria kuweka bayana umiliki wake katika kampuni hiyo ama sekta ya nishati kila mara anapokuwa akijadili ama kushughulikia suala lolote linalohusu sekta ya nishati. Yeye kama Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Madini na Nishati alipaswa kutaarifu rasmi bunge/kamati yake kuhusu umuliki wake katika bisahara yeyeote inayohusiana na sekta ya Madini ama Nishati. Je alifanya hivyo?

  Sasa badala ya kutueleza hapa kama Mwakyembe alitimiza wajibu wake kisheria na kwa mujibu wa taratibu za kimaadili wewe unakimbilia kumhusisha Zitto na Tanzania Daima katika jitihada za kumsafisha Lowassa. Zitto amsafishe lowassa ili iweje wakati aliwahi kupambana na Lowassa na wenziwe kutokana na mpango wao wa kumaliza waliokuwa wakiufanya pale nyumbani kwa Lowassa Dodoma wakati Lowassa akiwa bado Waziri mkuu. Iweje leo iwe sawa kwa Mwakyembe kutumia mapungufu ya kamati za bunge ili kujaribu kuhalalisha propaganda yake ya kuwa msimamo wa kamati ya mahesabu ya mashirika ya umma na zitto kama mwenyekiti unatokana na hongo ya POSHO lakini ikawa haramu kwa Zitto kujaribu kuonyesha USANII na UMASIHA FEKI wa Mwakyembe na kundi lake katika suala zima la MAPAMBANO dhidi ya UFISADI kama kweli Zitto anahusika na hilo.

  omarilyas
   
  Last edited: Mar 16, 2009
 15. L

  LazaroSMtindi Senior Member

  #15
  Mar 16, 2009
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 101
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  more or less udaku!!!
   
 16. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #16
  Mar 16, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Well it can be UDAKU to those who want to fool Tanzanians while in real truth they are very much part of the CORRUPT SYSTEM they have built and guard all this time but not for those Tanzanians who really want MABADILIKO MAKINI na sio this cheap USANII..

  Can you further explain how my views on these MASIHA FEKI na usanii wao ambao msimamo wa Kamati ya Mahesabu ya Mashirika ya Umm na Mwenyekiti wake Zitto unahatarisha kuwaanika hadharani are more or less udaku as you put here?

  omarilyas
   
Loading...