Hashpower7113
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 1,354
- 2,144
Hii inaweza kuwa habari njema sana kwa wanywaji wa pombe! Inafahamika kwamba ili ulewe, lazima unywe kinywaji chenye kilevi ukipendacho, inaweza kuwa ni pombe za kienyeji, bia au pombe kali lakini mwisho wa siku malengo ya mnywaji ni kulewa.
Zipo kero nyingi zinazoweza kumkumba mnywaji katika starehe yake ya kulewa, kubwa ikiwa ni pamoja na kulazimika kupiga ‘chupa’ kibao ili kichwa kichangamke. Lakini pia, kwa vilevi kama bia, mnywaji atalazimika kuwa anainuka mara kwa mara kwa ajili ya kwenda kujisaidia haja ndogo!
Wengine hulazimika kukaa muda mrefu baa ili angalau wafikie kiwango cha kulewa wanachokihitaji.
Kero zinazowakumba wanywaji wawapo kwenye starehe yao ni nyingi na hiyo ikamsukuma Profesa wa Kirusi, Evgeny Moskalev kuingia maabara na kuumiza kichwa kutafuta njia inayoweza kumfanya mtu akalewa bila kupitia kwenye kero za ulevi.
Alichokifanya Moskalev, ni kuanza kufanya majaribio ya kukausha pombe aina ya vodka kupata ungaunga, ambao baadaye aliutumia kutengeneza vidonge.
Katika majaribio yake, Moskalev aligundua kwamba kumbe inawezekana mtu akalewa ‘chakari’ kwa kutumia vidonge vilivyotengenezwa kwa kuikausha vodka na kupata ungaunga. Utafiti wake ulionesha kwamba mtu anayekunywa vodka, na yule atakayetumia kidonge kwa kiwango kilekile, watalewa sawa.
Baada ya kufanikiwa kwa majaribio yake kwa kutumia vodka, Moskalev aliendelea na majaribio kwenye aina nyingine za pombe kuanzia kwenye whiski, ‘waini’, bia na pombe kali na kote teknolojia yake ilionesha mafanikio makubwa.
“Unatakiwa kujua ni kilevi kiasi gani kinatosha kukuleweshwa, kwenye kila kinywaji chenye kilevi huwa kunaandikwa asilimia ya kilevi kwa hiyo unajipima kisha unachukua vidonge vyenye kiwango unachokitaka. Ukinywa unalewa haraka, bila usumbufu wowote,” alikaririwa Moskalev wakati akihojiwa na Gazeti la Times of India.
Mara tu baada ya Moskalev kufanya utafiti huo, wanasayansi wengine kadhaa nao walikuja na utafiti unaofanana na huo na miongoni mwao ni David Nutt wa Kampuni ya British Tech Company Imperial Innovations ambaye yeye alikuja na utafiti mwingine kwamba alcohol pills, ni bora kuliko pombe kwa sababu uyeyushwaji wake mwilini, hauendi kuathiri figo au maini, kwa hivyo kuwa na faida kubwa ya kuzuia saratani miongoni mwa walevi.
Pia akaja na matokeo mengine kwamba alcohol pills hazimuachi mtumiaji na mning’inio (hang overs) wala haziwezi kumsababishia mtumiaji matatizo ya mchafuko wa tumbo unaotokana na pombe (alcohol poisoning).
Utafiti huo uliibua mjadala mkubwa miongoni mwa wanasayansi ambapo wengine wengi waliingia kazini kujaribu kuthibitisha kama kilichosemwa na Moskalev na Nutt ni kweli.
Mpaka sasa, matokeo ya tafiti zote zilizofanywa, yanaonesha alcohol pills ni mbadala mzuri wa pombe na zitakapoanza kutumika, zitamaliza kabisa matatizo ya vifo vinavyosababishwa na ulevi wa kupindukia, kuharibika kwa figo na maini kwa sababu ya ulevi, kupatwa na saratani za aina mbalimbali kutokana na unywaji wa pombe uliopitiliza na kadhalika.
Kingine kinachosisimua ni kwamba, alcohol pills zitakuwa zinauzwa na dawa nyingine za anti-alcohol pills, ambazo zenyewe zinafanya kazi kinyume na alcohol pills.
Yaani kama umekunywa vidonge na umelewa chakari, lakini ukapigiwa simu kwamba unatakiwa kurudi kazini haraka, unakunywa anti-alcohol pills na ndani ya muda mfupi tu, pombe zote zinakutoka! Unarudi kuwa mzima kabisa. Yajayo yanasisimua sana.
Kinachosubiriwa kwa sasa ni mamlaka za vyakula na madawa kuziidhinisha dawa hizi kisha zianze kuuzwa duniani kote.