Album ya Alicia Keys 'ALICIA' inatarajiwa kutoka kesho, Septemba 18

Forgotten

JF-Expert Member
Jul 20, 2018
653
1,000
Ijumaa ya tarehe 18 mwezi huu wa 9 inatarajiwa kutoka Album ya mwanamuziki nguli kutoka nchini marekani, Alicia Keys. Album hii itakuwa ni Studio Album ya 7 kutoka kwa mwanamuziki Alicia Keys katika carrer yake ya muziki. Album yake ya kwanza ilikwenda kwa jina 'Songs in A Minor' iliyoachiwa mwaka 2001.

Album hii ilivyotoka ilifanya vizuri na kushika namba 1 katika 'US Billboard 200' pia album hii ilifanikiwa kibiashara kwa kuuza nakala zaidi ya milioni 16 duniani na ikamfanya Alicia Keys kuwa best-selling new artist na best-selling R&B artist of 2001.

Album ya pili ilikwenda kwa jina la 'The Diary of Alicia Keys' iliyoachiwa mwaka 2003 na kuuza nakala milioni 8 duniani. Baada ya album hizi mbili zilifuatiwa na; As I Am (2007), The Element of Freedom (2009), Girl on Fire (2012), Here (2016) na inayotarajiwa kutoka hapo kesho, September 18, 2020 'ALICIA'

Alicia Keys - ALICIA.jpg


Album hii imekuwa ikizungumziwa sana mitandaoni, hasa kwa hapa nyumbani Tanzania ikiwa na jina kubwa ndani kutoka Africa na Mashariki yake. Jina la Diamond Platnumz ni moja ya majina yaliyoshirikishwa katika Album hii. Ni jina pekee kutoka Africa kuhusika katika album hii. Uwepo wa Diamond Platnumz ni ishara nzuri kwa muziki wa Bongo Flava, sina hakika kama imetumika ladha halisi ya Bongo Flava katika wimbo alioshirikishwa Diamond Platnumz ila naamini lugha ya Kiswahili italibeba jina la Bongo Flava. Kwenye album hii Diamond Platnumz amehusika katika track no. 4 inayokwenda kwa jina la 'Wasted Energy' kitu kizuri zaidi ni hii track kuwa katika namba za juu kabisa, hii itaiweka nyimbo hiyo karibu na usikilizaji katika Digital Platforms (Apple Music, Spotify) ambako track hupangwa kwa namba.

Fun facts kuhusu wimbo wa 'Wasted Energy'

1. Ndiyo wimbo ya pili kwa urefu (dakika) katika album.
Baada ya 'Time Machine' yenye dakika 4:30 inayofuata ni 'Wasted Energy' ikiwa na dakika 4:19.

2. Wimbo wa kwanza wa msanii kutoka marekani kumshirika msanii wa Bongo Flava.

3. Wimbo wa kwanza kuwa katika album ya mwanamuziki wa marekani akiwa ameshirikishwa msanii wa Bongo Flava.

Album hii inasubiriwa na mashabiki wengi wa Diamond Platnumz na wachache wapenzi wa Bongo Flava, kinachosubiriwa hasa ni wimbo huu wa 'Wasted Energy' kwa ukubwa wa Alicia Keys na Diamond Platnumz kwa Africa na Mashariki yake nautabiria wimbo huu kufanya vizuri katika Digital Platforms hasa YouTube; Watanzania hawahawa wanaofurika katika YouTube ya Diamond Platnumz naamini siku hiyo wataipamba comment section kwa lugha adhimu ya Kiswahili.

Diamond Platnumz anazidi kuupa heshima muziki wa Bongo Flava na collaboration hii na Alicia Keys ni hatua nzuri kufungua milango katika soko la muziki Marekani, inaweza isiwe mapema kusikika katika Playlist za DJ' wa Marekani lakini itamtambulisha katika soko hilo linaloshika nafasi ya kwanza kwa muziki duniani.

Alicia Keys amewahi kutamba na ngoma kama;

-If I Ain't Got You

-Girl on Fire
(Inferno Version) ft Nicki Minaj

-Blended Family feat. A$AP Rocky

-No One

-Fallin'

-In Common (Moja ya ngoma kali ninazozikubali kutoka kwa Alicia Keys)

Alicia Keys ameshinda jumla ya tuzo 152, Nominations zaidi ya 200. Ni mshindi wa tuzo ya Grammy kwa mara 15 huku akiwa nominated mara 29. Ukiachana na hayo Alicia Keys ana jumla ya followers Million 82.4 katika mitandao yake ya kijamii ya Instagram, Facebook na Twitter. Wafuasi wote hawa 82.4M wamechanganyika na mastaa wakubwa wa muziki duniani pamoja na sekta nyingine, wakiwemo; Ariana Grande, Nicki Minaj, Amandla Stenberg, Jessica Alba, Kehlani, Serena Williams, Serayah, Stephen Curry, Jordin Sparks, Dua Lipa, Chance The Rapper, 21 Savage, Camila Cabello, Cristiano Ronaldo, Tory Lanez, Marshmello, Shawn Mendes, The Rock, Post Malone, Aliya Janell, Meek Mill, Kevin Hart.

Nikiandika mastaa wote waliom-follow uzi utajaa huu, kiukweli wanaodhani Diamond Platnumz kapata shavu la kitoto wajitafakari mara mbilimbili. Alicia Keys ni moja wa wanamuziki wenye ushawishi mkubwa katika jamii Duniani. Hongera DIAMOND PLATNUMZ (Mfalme wa Bongo Flava)

UPDATES:

Ngoma ya 'Wasted Energy' nimeisikiliza, kiukweli ni ngoma kali sana. Japokuwa Diamond Platnumz ameimba kipande kidogo tu ila amefanya unyama sana, nimemsikia yule Diamond Platnumz wa 'Kamwambie' humu ndani ametulia sana. Nafasi aliyopewa kaitumia vizuri sana; Pongezi nyingi kwake ametisha sana pia kwa kutumia lugha adhimu ya Kiswahili.

Screenshot_20200917-144411.png


REFERENCE:

Unknown Author (2020) Alicia (album). [Online] Available at: Wikipedia (Accessed September 17, 2020)

Unknown Author (2020) Alicia Keys discography. [Online] Available at: Wikipedia (Accessed September 17, 2020)

Unknown Author (2020) List of awards and nominations received by Alicia Keys. [Online] Available at: Wikipedia (Accessed September 17, 2020)

Michelle Ruoff (2020) Top 10 Alicia Keys Songs. [Online] Available at: Broadcast and Listen to Internet Radio (Accessed September 17, 2020)

Imeandaliwa na: Forgotten
 

Hziyech22

JF-Expert Member
Jun 8, 2019
6,763
2,000
Nimesikia huyo wimbo aliyomshirikisha Diamond imeimbwa style fulani ya rege diamond ameua Sana alafu kaimba kiswahili ameimba Kama nyimbo zake za Zamani ila Alicia key kamfanyia umafia diamond kampa kipande kidogo Cha kuimba 🤣🤣
 

shiu yang

JF-Expert Member
Sep 16, 2016
3,242
2,000
Nimesikia huyo wimbo aliyomshirikisha Diamond imeimbwa style fulani ya rege diamond ameua Sana alafu kaimba kiswahili ameimba Kama nyimbo zake za Zamani ila Alicia key kamfanyia umafia diamond kampa kipande kidogo Cha kuimba
Uko wap mkuu udrop hapa
 

Forgotten

JF-Expert Member
Jul 20, 2018
653
1,000
OFFICIAL: Album ya 'ALICIA' kutoka kwa Alicia Keys imetoka na ngoma aliyomshirikisha Diamond Platnumz imekuwa na mwanzo mzuri kwani mpaka sasa ina views 20K katika mtandao wa YouTube ikiongoza kutazamwa zaidi ya nyimbo zote zili-upload-iwa leo katika channel ya Alicia Keys.
Screenshot_20200918-093354.jpg
 

Citizen B

JF-Expert Member
May 13, 2019
4,476
2,000
OFFICIAL: Album ya 'ALICIA' kutoka kwa Alicia Keys imetoka na ngoma aliyomshirikisha Diamond Platnumz imekuwa na mwanzo mzuri kwani mpaka sasa ina views 20K katika mtandao wa YouTube ikiongoza kutazamwa zaidi ya nyimbo zote zili-upload-iwa leo katika channel ya Alicia Keys. View attachment 1573120

Huyu bimaza bado anaimba tu? Mbona keshapotea kwenye game kitambo
Alaf mondi mbona anapenda kufanya kazi na watu waliofulia marekani?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom