Albert Msando: Bashiru sio mla Rushwa


Kwenye wizi pana walakini kwa kweli. Ila aina ya uongozi wake ndio iliyomchafua sana. Ubabe ubabe.. Najiuliza sipati jibu - alikumbwa na nini Dr masikini?!! Maana ni kama madaraka yalimlevya. Yeye na yule jamaa mwingine wa ‘viete’. Waliendesha chama kama wanaswaga ng’ombe jamani!

Hapo kwenye ‘pengine walikuwa na jambo lao’, panafikirisha sana. Labda ni Mungu tu ndio ametuokoa na hilo jambo lao. Maana tusingeweza kulizuia. Au ni kweli ‘tunausalama’ mzuri sana kama wachache wasemavyo, kwamba imezuiliwa jambo hilo lisiikumbe nchi (japo siamini kama hao watu wanaweza kulisaidia taifa kiasi hicho, maana na wao walishakuwa watu wa kuabudu). Pole yake Dr.
 
Hata majobless wanafurahia Bashiru kuwa mbunge, hivi ubunge siku hizi haulipi? Mbona watu wanafanya as though Bashiru hana kitu tena. Hao hao watarudi mwezi ujao kushinikiza wabunge wakatwe hela.
Kwa nafasi aliyokuwa nayo Bashiru ni kubwa sana na ya heshima na pia ni daraja fupi sana kupanda ngazi
 
Ogopa sana kitu kinachoitwa nyakati, kinachobadili watu si tabia ni nyakati, yaani muda utaamua tabia yako iwe namna gani? Kwa yale yanayotajwa dhidi yake kwanini ni yeye tuu na si wengine?
 
Pole sana kwa best wako kukutwa na hayo yaliyomkuta na sasa sifa zake zoote zimeporomoka kama mchanga
 
Msando aliunga juhudi hivyo akili zake alisha zikabidhi kwa chakubanga
 
Wengi wenu mnaomsema Dr. Bashiru vibaya! Ni wale ambao mlikuwa mmejimilikisha mali za chama kinyemela. Mlifanya mali za chama kuwa vitega uchumi vyenu. Baada ya Bashiru kuwakazia na kukataa rushwa zenu! Sasa mmeanza kumtusi! Lakini mti wenye matunda ndiyo unaopigwa mawe.
 
Tunaomjua vizuri Dk. Bashiru tunajua kwanini Hayati JPM alimpenda na kwanini baadhi ya watu wamefurahia kutengwa kwake. Ni muda tu utajibu kama ilivyokuwa kwa Mzee Mangula!
 
Binafsi hata mimi nakuunga mkono Mr arbert msando, Bashiru ktk utendaji wake wa kazi, hafungwi na masaa, kuna kipindi alikuwa anatembelea ofsini mwetu na ratiba ilikuwa afike saa saa 9 alasiri, kwa sababu ya majukumu akawa amechelewa lakini akapiga simu kuwa ni lazima afike hata km ni saa 6 usiku, kweli alifika saa 3 usiku na alitimiza kila alichotarajia kufanya.

Lakini kama matani, akasema tunainuka kwenda kwenye mradi mwingine saa 11 asubuhi, hivyo tuwe tayari na kweli ilipofika saa 10;30, akapiga simu tayari yeye akiwa amejiandaa, na tulilala saa 6 usiku, kwa hiyo Msando mie nakubaliana na wewe,
 
Kwa hiyo akilala masaa mawili ndio anakuwa sio Mwizi? Hii habari ya kulala masaa mawili inahusika vipi hapa?
Pathetic
 
Kwa hiyo akilala masaa mawili ndio anakuwa sio Mwizi? Hii habari ya kulala masaa mawili inahusika vipi hapa?
Pathetic
Naona mnaandika tu mwizi mwizi, wengine jizi! Lakini hakuna hata mmoja wenu aliyetaja na kuzibitisha huo wizi aliufanya lini na ofisi ipi???. Hebu tutajieni ofisi hata moja aliyopiga hizo hela.
 
Chawa wa bashiru na msando[emoji1787]mtajitokeza tu [emoji1787] time will tell
Jamaa aliwatemesha mali za chama ndo kisa cha chuki zote hizi.
Lakini Bashiru sio sawa na wewe , aliisha toka huko kwenye UPUMBAVU NA ULOFA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…