Albert Msando: Bashiru sio mla Rushwa

Tukiachana na ya Msando, Tuliofanya kazi na huyu mzee sote tunashangazwa na tuhuma za yeye kuhusika na ukwapuaji wa pesa "huko kunakosemekana". To the best of my knowldedge huyu mzee sio fisadi wala mwizi, Maisha yake binafsi, familia yake Mpaka shule anazosomesha watoto wake, siuoni huo ufisadi wa Dr. Bashiru.

Binafsi nampinga yeye kupewa nafasi ya KM sababu haifahamu siasa ya CCM, alichukuliwa sana na "aina ya siasa za hayati" na matokeo yake wakaumiza watu wengi, kama angekuwa KM imara anayekifahamu chama kuna vitu angeweza kumshauri Hayati, au asikubaliane nae katika baadhi ya mambo. Yaliyotokea yamesababisha chama kimepata ushindi huo lakini credibility imeshuka sana, almost to zero. Hakukuwa na sababu yoyote ya msingi kuingilia siasa za majimbo, wangeachwa wabunge wapambane na hali zao na wenzao huko, Lililofanyika linanifanya niamini kuwa Hayati na Bashiru walikuwa na lao jambo.

Lakini tuhuma za wizi kwa Dr. Bashiru binafsi sitaki kuchukuliwa na upepo mpaka pale zitakapothibitishwa. Haya ni maoni yangu binafsi.
 
Acha kutetea upuuzi, kakwapua baada ya mzee baba kusepa🙏
 
Kweli penye uchafu tofauti mchina hubuni na kutengeneza brush ya kipekee ya kuusafisha uchafu huo bila kutumia nguvu nyingi!
Msando rejea hotuba ya CDF kule Chato, isikikize huku ukiwa na soda baridi unainywa taratibu, Kisha Rudi hapa huenda ukaikana hii post yako!
Moyo wa mtu hausemewi dogo!
 
Binti, moyo wa mtu kichaka! Umdhaniaye ndiye, kumbe siye! Pesa ni sabuni ya roho, Nani asiyezitaka? Kama kina Trump na ubilionea wake alihongwa na akachukua, kina Perez huko Israel wamehongwa huku account zao zimejaa matarakimu zaidi ya 12, Nani wa kuzikataa ambazo hujazitolea jasho?
 

Yani huna uliloacha. Umesema kweli kabisa. Huyu ashike nafasi ya uRais.. tutalia na kusaga meno. Mara mia ya Jiwe. Halafu wala hakuelekea kuwa hivi, sijui kitu gani kilimkuta.!
 
Kwa hiyo ukishamwamini wewe na magu ndo unataka na sisi wote tumwamini, hizi akili za wapi hizi?
Akili za kutafuta uteuzi hizo, Msando anahangaika sana apate uteuzi
 
Kutoka na mayala leo wkt anaojiwa nadw kiswahili alisema kuwa dkt huyo alikuwa anaandaliwa kuja kuwa rais baada ya jiwe kungatuka
Ndiyo maana gang lao wapo hoi bin taaban kisiasa
 
Hapo alipokuwa tayari alishajiona bonge la star
 
Alafu tazama media anazochagua kwenda kufanya interview
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…