Albert Einstein na Charles Darwin.......

Albert Einstein na Charles Darwin.......

If it wasn't for the genetic problems that might result from it (chances za recessive genes kujitokeza) I don't see why people shouldn't marry their cousins. Kumbuka zamani hapakua na kitu dating. So if you want to marry someone you know basi ni cousin.
Pharaohs married their blood sisters only to keep the 'goldy' bloodline pure from huma imperfection. One of them ended up beibg born with a spinal malformation ndio wakaelewa kuna hatari ya ndugu kuoana.
On the personality disorders sio scientists tu. It is believed that we all have some disorder (more or less) tofauti ni kiwango gani diaorder yetu inakubalika au inashangaza jamii zetu (foulcaut). Scientists (and more increasingly famous artists) wanaonekana kuathirika zaidi just because they are under the spotlights.
 
Basi nahisi wewe umekua around madr na maprof hadi mkaweza kuelewana.

Lakini kuna maeneo hamna maelewano, raia tunaona dr kachanganyikiwa na yeye anashangaa how ignorant a human being can be?

Mradi tu tunakinzana kimawazo.

Ni wapi huko ambapo hakuna maelewano? Maana Ikungu maprof walikuwa wanajichanganya tu na raia na wanaelewana kabisa. Tena wengine bila hata kuambiwa yule ni prof so and so huwezi hata kujua.

Maprof ni watu wa kawaida tu na wala siyo majiniasi.
 
Ni wapi huko ambapo hakuna maelewano? Maana Ikungu maprof walikuwa wanajichanganya tu na raia na wanaelewana kabisa. Tena wengine bila hata kuambiwa yule ni prof so and so huwezi hata kujua.

Maprof ni watu wa kawaida tu na wala siyo majiniasi.

Kwani majiniasi wako vipi????
 
kwa sababu wanawajua kwa ukaribu sana na pia kuoa binamu nadhani ni jadi ya baadhi ya makabila.
 
Mkuu The Boss, kuna wakati niliwahi kuweka uzi hapa kuhusu wanasayansi hawa na vituko vyao nikihoji kama walikuwa ni vichaa au hamnazo...?

Kwa mfano Albert Einstein ni mwanasayansi alieweza kuelezea kwa undani kuhusu uwiano mwingi wa masuala ya sayansi. Yeye alifurahia sana kuwa na nyumba ndogo. Hiyo nyumba yake ndogo alikuwa ni binamu yake na aliishi nae kwa takribani miaka mitano kabla hajamuacha mkewe wa ndoa ambaye alizaa nae watoto kadhaa kabla ya kufunga nae ndoa, na kuioa hiyo nyumba ndogo.

Charles Darwin huyu ningependa kumuita mzee wa utata, huyu nae ni mwanasayansi aliyezungumzia kuhusu mabadiliko ya viumbe (Evolution). Alikuwa akiishi peke yake kwa muda mrefu bila ya kuoa kwa sababu alikuwa akijiuliza faida ya kuoa na kuishi bila kuoa kabisa. Mwansayansi huyu nae alikuwa na vituko vingi, kwani kuna wakati alisema, “Kwa kiasi fulani mke ni bora kuliko mbwa, lakini ni kupoteza muda wako tu kuwa nae” Hata hivyo alikuja kuoa baada ya kuwa na uhusianao wa muda mrefu na mwanamke huyo aliyemuoa.

Sigmund Freud, Huyu ameweza kueleza vizuri kuhusu saikolojia na ufahamu, kwa ujumla alikuwa ni mtu mzuri, lakini alikuwa na mzozo na rafiki yake, kutokana na tabia zake za kushindwa kudhibiti hisia zake za kutojitosha, na hivyo kutaka kuabudiwa na kunyeyekewa.

Isaac Newton ambaye aliweza kukokotoa na kutoa kanuni za mwendo zijulikanazo kama Newton laws of motion, na kanuni ya nguvu za mvutano za dunia, alilelewa na bibi yake, baada ya baba yake kufariki na mama yake kuolewa na mwanamume mwingine, ambaye Newton hakumpenda kabisa. Newton alikuwa na tabia ya kupenda ugomvi na mizozo isiyo na umuhimu na wanachuo wenzake na hata marafiki zake, pia alishawahi kulelewa kwenye vituo vyenye kutoa ushauri nasaha. Kumbuka hapa namzungumzia mtu ambaye ugunduzi wake kwenye Fizikia haujavunjwa hadi leo.

Marie Curie ambaye aligundua Radioactivity, aliishi na mume wake kwenye nyumba iliyokuwa na vitu vichache na vilivyozagaa kwa sababu alichukia sana kazi za ndani, sijui wakati huo kulikuwa hakuna watumishi wa ndani (House Girls)? Wakati wakifanya shughuli zao za uchunguzi kuhusu radioactivity walikuwa wakiishi katika kibanda chao kilichokuwa na matundu, kiasi ambacho hata mvua ikinyesha maji yaliweza kuingia ndani. Hawakuwa na fedha nyingi na mara nyingi walitumia fedha kidogo walizonazo kununua kahawa na kunywa kwa furaha, huku wakiota katika jiko lao la stovu. Marie Curie nae alijishindia tunzo mbili za Nobeli.

Paul Erdos mmoja wa wanahisabati katika karne ya 20, ambaye amesaidia sana katika kutengeneza Kompyuta, huyu naye hakuwa ametulia sana. Hakuishi maisha ya kifahari, karibu maisha yake yote yalikuwa ya kifukara, kwani alitegemea misaada ya chakula na nguo kutoka kwa marafiki wema. Hakupenda kujilimbikizia mali ingawa angeweza kama angetaka.

Je sasa umeweza kushawishika kwamba watu wenye vipaji maalum (Geniuses), huenda ni watu ambao kwenye upande wa pili wa maisha yaani katika kujenga maisha yao, hawana uwezo? Lakini Je sio kwamba watu wanapokuwa na uwezo mkubwa kiakili hatimaye mambo mengine kama vile fedha na ufahari vinakosa maana kwao? Nadhani hili ndilo la msingi.

Kwa upande wa mahusiano wanasayansi hawa walikuwa hamnazo kweli.........!
Akili nyng huondoa maarifa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom