Albert Chalamila: Mabasi 99 yataingia Agosti 15, mengine 250 yataingia Oktoba 1, 2025

Albert Chalamila: Mabasi 99 yataingia Agosti 15, mengine 250 yataingia Oktoba 1, 2025

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,783
Reaction score
14,975
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema kuwa ifikapo tarehe 15 Agosti 2025, mabasi 99 yataanza rasmi kutoa huduma ya usafiri katika barabara ya Mbagala.

Aidha, kufikia tarehe 1 Oktoba 2025, mabasi mengine 250 yanatarajiwa kuanza safari kati ya kituo cha Mbezi Kimara hadi Gerezani, ikiwa ni sehemu ya maboresho ya mfumo wa usafiri wa umma jijini Dar es Salaam.

Pia soma:
Kwa hadha inayoendelea kwa wakazi wa kimara ni vizuri daladala zikarusiwa kupita kwenye njia ya mwendokasi wakati uvumbuzi ukitafutwa
 
Serikali jenga tu miundombinu tu ya reli na barabara,kazi ya mabasi haitaki akili kubwa kama serikali inavyofikiria
Mpe leo Abood wa Morogoro kazi ya kununua na kuendesha mradi wa mwendo kasi wala usingemuona Chalamila anafoka leo.

Kwa mradi wa mabasi Mama wanakudanganya hawawezi kabisa.
Mabasi ya Kichina hayafai inatakiwa Scania ndio yatadumu.
Ya Kichina ni kwa watu binafsi si kwa serikali.

Nyerere aliingizwa kichwa kichwa na machawa kuitaifisha DMT yaani Dar es salaam Motors Transport ya Makaburu.
Pammoja na akili nyingi ya Nyerere na juhudi zake hadi anastaafu hapakuwepo UDA,wala KAMATA. Si hiyo tu Nyerere kwa kuchonga mdomo alikuwa anapewa BURE mabasi ya Leyland na Uingereza, pammoja na Benz ya West Germany hadi kujengewa karakana kubwa kubwa bado alipata wash. out.
Kama haitoshi akapewa mabasi ya Isuzu kibao kutoka Japan lakini sikio la kufa.

Akaigawa DMT kuzaa UDA na KAMATA bado haikuzaa matunda,akaanzisha shirika la NIT,bado alifungwa magoli tatu bila.
Kama haitoshi kaanzisha Chuo cha usafirishaji hakuna hafueni ilipatikana.
Kasema labda mabasi ni madogo akatinga mpaka Hungary akaleta mabasi kama train.Makubwa yakijulikana kama Ikarus Kumbakumba marefu yana mwendo kasi lakini hadi Nyerere anangatuka usafiri wa umma ulikuwa ume kufa kabisa.

Mama achana na mipango feki,baada ya miaka mitatu au minne yale makopo ya Kichina asili 60 yatakuwa marehemu kabisa.
Kwani mnataka kurudia makosa kila mara?
 
Huku mbagala hatutakubali UJINGA kama mnaofanya kimara wa kuwachomesha mahindi abiria vituoni huku tutawapopoa mawe kwelikweli, Sisi hatuna huo ustaarabu wa kupanda Kwa foleni Sisi kila MTU ni machinga
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema kuwa ifikapo tarehe 15 Agosti 2025, mabasi 99 yataanza rasmi kutoa huduma ya usafiri katika barabara ya Mbagala.

Aidha, kufikia tarehe 1 Oktoba 2025, mabasi mengine 250 yanatarajiwa kuanza safari kati ya kituo cha Mbezi Kimara hadi Gerezani, ikiwa ni sehemu ya maboresho ya mfumo wa usafiri wa umma jijini Dar es Salaam.

Pia soma:
Kwa hadha inayoendelea kwa wakazi wa kimara ni vizuri daladala zikarusiwa kupita kwenye njia ya mwendokasi wakati uvumbuzi ukitafutwa
Hao waandeshao mabasi wa binafsi na serikali ifikapo oct 2025 wataleta mapinduzi makubwa sana
 
Back
Top Bottom