Alaumiwe nani kati yao hawa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Alaumiwe nani kati yao hawa

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Billie, Oct 10, 2011.

 1. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #1
  Oct 10, 2011
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,333
  Likes Received: 2,328
  Trophy Points: 280
  Roger alikuwa anamfundisha dada yng na pia alikuwa na uhusiano nae.Ila Roger alisifika kwa akili nyingi pale shule ya secondary Pugu high school walijuana na dada kwa kuwa alikuwa anasoma pale form 3(enzi zile Pugu palikuwa kuna mtaala wa shule za tasisi) ila Roger alikuwa form six.Alizoeleka kuja nyumbani mara kwa mara na mimi nikiwa rafiki yake mkubwa coz huwa akija lazima aje na zawadi yangu.WALI AHADIANA KUONA ila Roger alifaulu na kuchaguliwa Makerere University (Uganda) na dada akabaki pale Pugu ili amalize form four yake kibaya zaidi hawakuwa na simu kama unavyojua simu enzi zile zilikuwa zinamilikiwa na watu wenye uwezo wa juu.ILA nilipata kumsoma dada yangu vile hali yake haikuwa sawa kutokana na Roger kuwa mbali nae .Miaka minne mbele Roger alirudi kutoka Uganda na akaja mpaka shule ya msingi niliyokuwa nasoma kwa kuwa pale tulipokuwa tumepanga tulihama baada ya Mama kujenga nyumba yetu(single parent family) ndipo nikapanda kwenye gari alilokuwa amekuja nalo baada ya kuniombea ruhusa pale shuleni kwa vile nilikuwa mdogo enz zile nilijikuta kumsahau kidogo kwa vile alikuwa amenenepa kiasi chake.Basi njiani tulikumbushana na akaniuliza swali "nimekuja kumuona dada yako na mama hivi wapo"?nikamjibu "wapo"Akaongeza swali lingine dada yako kaolewa? Mi nikajibu "hapana ila anaishi kwake na mmewe".Roger akatamka "SHIT"na akagonga usukani wa gari na honi ikalia.Ila hakukoma kuuliza " Ana mtoto?"mi nikajibu "hapana ila ana mimba kubwa"Ghafla akapiga breki na kusikitika sana.
  Tukafika nyumban bahati nzuri dada alikuwa yupo pale home kwa ajili ya uangalizi wa ujauzito wake wa kwanza(kwa mama) Gari lilipaki na hatimaye tukashuka mama alikuwa wa kwanza kutuona na hatimaye dada yangu ila cha kushangaza Dada na Roger walikimbiliana na kukumbatiana kwa furaha hadi machozi yakawatoka.Walikataa kukaa sebulen na kuniagiza viti ili wakae nje.Mama cha kushangaza akabun kasafari ili kuwapa nafasi wazungumze Nilichokiona ni kuwa walikuwa wanaliliana tuu kwa kuwa mi nilikuwa nawachungulia pale nje kupitia dirisha la chumba chetu na namimi nikajikuta namkumbuka rasmi Roger kutokana na zawadi zake ambazo zingne nilikuwa nazo kama Uniform za mpira(jes),na mkebe wa vifaa vya shule.
  Tuishie hapa na ntaendelea ila nataka kujua nani alaumiwe ikiwa dada anasema alisubiri kutokana na kutokuwa na mawasiliano kulimtisha ndo akajikuta ndani ya mikono ya mume mwingine na Roger yeye anasema alipatwa na tatizo la kifedha ndio maana ikamladhimu kubaki kwa rafiki yake Mganda huku wanafanya tenda mbalimbali ikiwemo ualimu ndo maana hakuweza kurudi hadi pale alipomaliza degree yake na pia anasema ameshatuma barua 3 kwa anuani ya Pugu high schooa dada hakuzipata hizo barua.

  TUENDELEEENI JAMANI:Kwanza naomba samahani kwa kuikatisha maana haikuwa kusudio langu betri iliisha coz natumia simu kupost hii story.
  Nilitoka dirishan nakabadili nguo zangu na kwenda kufunua ma Hot pot kucheki wameniwekea nini Nikala nikaenda kucheza(maisha ya uswahili coz sikuwa get kali) Basi kurudi kutoka kwenye mpira sikumkuta mgeni wala dada mama ila nilikuta nimeachiwa Sh elfu 20 za kibongo ila mama alizizuia nakusema ngoja Nikuwekee ntakuwa nakupa kidogo kidogo .Ila mida iliyoyoma hadi ikafika saa 2 usiku sikumuona dada kurudi kwa kuwa niliambiwa kapanda gari na kaenda kumsindikiza mgeni.PUNDE SI PUNDE hazikupita dak 5 nikaona mwanga mkali wa gari ukimulika kuelekea nyumba yetu ilikuwa gari ile ile ya Roger akamshusha dada na akaniulizia mimi dada aliingia ndani na kuniita.Nikaenda mpaka kwenye gari nikatoa shukrani kwa ule mzigo akanisifia sana kuwa mi nilikuwa mtoto mzuri kwan walimu walinisifia sana na kumuonesha faili la maendeleo yangu pale skuli.Na alianza kunijaza moyo kuwa nisome sana hata kama kwetu hakuna uwezo na kunipa vijihabari vya shida alizopitia yeye wakati anasoma na kuapa kuwa hatavumilia kuona zile shida zikinurudia mimi kifupi akanipromise kunisuport kifedha.JAMAA AKAONDOKA ILA SASA kila weekend alikuwa anakuja na gari na kumwaga zawadi na kusindikizwa na dada kama kawa kurudi saa 2 hadi 3 na mbaya zaidi tripu hiz zingine dada alikuja ananukia arufu ya pombe na ulegevu fulani hivi wa kilevi.Kuna siku kama 2 hivi Mme wa dada na Rodger walishawahi kugongana ila walisalimiana na kukaushiana tuu.Baada ya tukio hilo mmewe dada akaibuka na issue ya kutaka kumuoa dada(kubaliki ndoa kwa wakatoliki wanajua hili) ila dada alipinga kwa hoja yake kuwa hawezi kufunga ndoa na TUMBO KUBWA vile kulitokea mvutano mkubwa sana kwenye hili hadi mme wa dada akaona kashindwa kwenye hili, miez kadhaa mbele dada akajifungua mtoto wa kiume na mmewe akarudisha ombi lake la kutaka kumuoa ila dada akakana na akatoa sababu ya kuwa mwili wake haukukaa vizuri baada ya kujifungua so akamuomba mumewe ammpe muda atakapo hitaji ndoa atamuambia yeye mwenyewe.LIKAIBUKA lingine la namba inapiga mara kwa mara kwa dada na kumfanya mmewe apandishe jazba na kuleta mashtaka kwa mama.Akidai kuwa anakuta nakala za sms za kutumiwa voucher nyingi kama elfu 20 au 25 mara kwa mara
   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  Oct 10, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,867
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  acha nipite, ntarudi
   
 3. S

  Siimay Member

  #3
  Oct 10, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna wa kumalaumu mwenzake hapo ila kama tu walipeana ahadi pindi walipobaini kuwa mmoja anakwenda masomoni kusoma..
   
 4. lutamyo

  lutamyo JF-Expert Member

  #4
  Oct 10, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 633
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Naona hadith tam ngoja ikolee
   
 5. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #5
  Oct 10, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  He Part2 inakuja duh kweli filamu za kibongo wizi mtupu.
   
 6. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #6
  Oct 10, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,640
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Waache wenyewe.
   
 7. ENZO

  ENZO JF-Expert Member

  #7
  Oct 10, 2011
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,057
  Likes Received: 552
  Trophy Points: 280
  Siwezi kuchangia mana story umeikatisha kati kati .........
   
 8. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #8
  Oct 10, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 736
  Trophy Points: 280
  Lawama za nini sasa...wote wanastahili pongezi.
   
 9. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #9
  Oct 10, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,499
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160
  Hapo kuna dalili ya mmojawao (kidume) kupigwa kibuti, Mana ake mmmh!!!:shock:
   
 10. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #10
  Oct 10, 2011
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,333
  Likes Received: 2,328
  Trophy Points: 280
  kivipi?
   
 11. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #11
  Oct 10, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  malizi story kwanza ndo na mimi nitakuja kutoa mawazo yangu kuwa nani alaumiwe
   
 12. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #12
  Oct 10, 2011
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,333
  Likes Received: 2,328
  Trophy Points: 280
  Likwan hii stori ni ya ukweli na ninaendeleza coz betri ya simu ilikwisha ndo maana nikaikatiza na nilikwenda kumtembelea dada(mhusika wa hii stori)
   
 13. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #13
  Oct 10, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  daah hebu check na shigongo ndugu uuze hii kitu
   
 14. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #14
  Oct 11, 2011
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,333
  Likes Received: 2,328
  Trophy Points: 280
  INAENDELEA HAPA samahani uwezo wa simu unanizuia kumalizia pale nilipoishia ngoja niimalizie hapa...
  Kwa kifupi ni kuwa Roger na dada mimi nahisi wanaendelea mpaka leo na kuna ugomvi mzito sana kati ya mmewe na dada yangu maana ilifikia kipindi dada alirudi nyumbani akakaa kama miaka 3 kisa ugomvi huu.Na nilimsikia dada akimuomba ushauri shoga yake ambaye ni mtoto wa Aunt ampe ushauri kwa kuwa Amehaidiwa kujengewa nyumba na kutafutiwa kazi na life itaendelea vizuri tu na "Roger".Mmewe alimfuata nyumbani na kumuomba msamaha kuwa amsamehe kwa kumhisi vibaya na arudi nyumbani waendeleze maisha na nakumbuka kilikaliwa kikao ili warudiane ndipo busara za wakubwa zikawarudisha.SASA TAMBUA VITU VIfuatavyo Mme wa dada ana uwezo wa wastani yeye na wenzake wameunda ka kampuni ka mambo ya Finishing za nyumba nyumba kina deal na kupaka rangi,ceiling board za kisasa(gypsum) na vingnevyo.Na roger ni mfanya kazi mkubwa serikalini pia ana miradi mingi kawekeza maeneo mbalimbali nchini,ILA dada yangu goli kipa yaani ni wa nyumbani ila ni Mzuri sana hata natamani kuwatumia picha yake muione ila sababu za kiusalama zinanikataza.
  KWA SASA ANAISHI NA MUMEWE NA HAWAJAFUNGA NDOA NA MGOGORO UNATULIA KIDOGO NA UNAIBUKA TENA PALE TU ROGER AKIJA DAR KWA SABABU ANAFANYA KAZI MKOA MWINGINE NJE YA DAR ES SALAAM.
  Hivyo nakaribisha ushauri,maoni ila mi nimeshindwa kuamua lolote nimeona bora niwashirikishe na nyie wenzangu.
   
 15. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #15
  Oct 11, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
 16. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #16
  Oct 11, 2011
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,333
  Likes Received: 2,328
  Trophy Points: 280
  Nimeshamalizia hapo chini na juu nimeiendeleza so karibu sana.
   
 17. MADAM T

  MADAM T JF-Expert Member

  #17
  Oct 11, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 3,655
  Likes Received: 937
  Trophy Points: 280
  Kwani huyo Roger yeye hajaoa?
   
 18. Tulizo

  Tulizo JF-Expert Member

  #18
  Oct 11, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 849
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Namuonea Huruma dada yako Kwani hatokuwa mke Wa huyo mumewe wala Roger. Amepoteza confidence ya wanawake. Inaelekea kuna kitu kinamsumbua Kama siyo uchumi ni ulimbukeni, huyo Roger ana dalili zote za mpita Njia.
   
 19. A

  Ashangedere Senior Member

  #19
  Oct 11, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haya mambo yapo jamani halafu yanauma sana, kama haijawahi kukutokea tema mate chini isikutokee. Yani unajikuta umekata tamaa ya kuwa na love of your life coz mmepotezana, so unaenda kwa alternative number mbili, baadae ndio anaibuka kutoka huko alipotokea, kaoa na wewe umeoa. Binafsi ilishanitokea na inanifanya niishi maisha ya mawazo wakati mwingine, na yy pia lakini tunajaribu kukaa mbali na kukubali hali halisi.
   
 20. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #20
  Oct 11, 2011
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,333
  Likes Received: 2,328
  Trophy Points: 280
  kwa mujibu wa maelezo ya dada anasema Bado hajaoa kwa kuwa kavurugukiwa na tukio hili na anang'ang'ania kuwa dada ndiye chaguo lake tangu zamani.
   
Loading...