Msalaba una maana kubwa Kwa wote wenye Imani katika kristo Yesu.
Ni Ishara kuwa Mungu alikuja katika mwili akafa akazikwa na kufufuka siku ya tatu.
Ikumbukwe pia kuwa Ibada Kwa wakristo ni katika Roho na Kweli.
Msalaba ni katika Imani, Si katika kuuvaa shingoni au kininginiza ndani ya gari. Kufanya hivyo ni kufanya Ibada ya sanamu Kwa kujua au kutojua.
Shetani ni Mwizi na baba wa copy na paste, alama ya Bikari watumiayo Freemason amecopy na kupaste alama ya Mungu iliyoko Mbinguni.
Alichokifanya ni kuigeuza juu chini na kuifanya ni alama yake Ili aabudiwe.
Waaminio haturuhusiwi kuvaa michoro na alama zozote katika miili yetu, ndomana hata nguo tunatakiwa kuvaa RANGI Moja, mambo mengi Bado hatujafikia utimilifu, lakini tunakoelekea tutarudi kama Kanisa la kwanza.
Mungu awabariki nyote.
Amen
Siri zilizomo Kanisani ambazo zinamzuwiya Kiongozi kuwafundisha watu ukweli na nidhamu ya woga iliyojengwa ndani ya Wafuasi inamfanya mtu akubali jambo bila kulielewa kabisa akiuliza husomewa vipande vya aya za biblia na kupewa tafsiri potofu, lazima akubaliane na Kiongozi wake. Ukimwambia ukweli yuko tayari kupigana na kuuwa mtu, hata hivyo lazima ukweli tuuseme tu kwa kumuogopa Mungu.
Mataya 10:26-27
Waraka huu nitaongelea alama mojawapo kuu na kongwe ya mojawapo ya dini yenye wafuasi wengi. Nitajitahidi kuonyesha chanzo hata uwongo unaozunguka uwepo, ujio, matumizi na maana nzima ya alama hii ya
MSALABA.
Kama zilivyo alama mbali mbali, msalaba ni alama kuu (
religious symbol) na muhimu ya dini ya kikristo. Wakristo wengi ukiondoa wale wa Mashahidi Jehova Msalaba kwao ni alama muhimu sana katika imani zao. Kwani inaaminiwa kuwa Bwana Yesu aliwahi kutundikwa na kufa msalabani. Alama hii ni sawa na bendera ya nchi kwa ukristo. Hivyo ni alama muhimu na yenye thamani kubwa.
Matumizi ya misalaba na aina nyingine za masanamu zilipigwa marufuku na kuonekana kuwa ni upagani, lakini mnamo mwaka ca. 675-ca.749 mtakatifu
Yohana Damascene akakubali kwamba yafaa matumizi ya masanamu na aina nyingine za alama zinazo wakilisha ukristo,kwa maana ya kusulubiwa kwa Yesu pamoja na watakatifu wengine kutumika kwa kufundishia. Kikao cha mara ya pili cha Nicea 787 kikarejesha rasmi matumizi ya alama na taswira. Mnamo mwaka 814 - 43 matumizi ya masanamu na alama zingine ziliondolewa makanisani kwa kuona kuwa watu walishaanza kuziabudu. Adhabu kali ziliwafika zikiwemo kuuawa kwa wale wote walikuwa wakitumia masanamu na alama zingine zilizokuwepo wakati ule. Matumizi haya ya misalaba na masanamu yalikuja kurejeshwa tena kati mwaka 759-826 na mtakatifu
Theodore.
Masanamu yanayohusishwa zaidi katika ibada hizo ni pamoja na sanamu la mungu-mtu Yesu wa Kikristo akiwa amebebwa na mama yake (Madona) ambaye amepewa cheo cha umama wa mungu. Yaani Theotokos (“
Mother of God ca.185-ca.254”), na kwenye sanamu lingine akiwa amekufa msalabani, sanamu la "Bikira Maria", sanamu la malaika na masanamu mengine mengi ya watakatifu wa Kikristo waliokufa!
Kama maandiko ya Biblia tukufu yafundishavyo, ibada hii (ya sanamu) ifanywayo na Wakristo, kiasili imetokana na watu wa mataifa (wapagani). Uthibitisho wa hilo tunaupata katika maandiko yafuatayo:
"
Bali walijichanganya na mataifa, wakajifunza matendo yao.Wakazitumikia sanamu zao, Nazo zikawa mtego kwao".
(Zab 106:35-36).
Kwa uchache, maandiko hayo juu yanathibitisha wazi kuwa waasisi na wahusika wakuu wa ibada hiyo (ya sanamu) ni watu wa mataifa, yaani wapagani.
Sambamba na ukweli huo, Biblia haikuacha pia kubainisha jinsi Yehovah alivyowakemea wanadamu tangu mapema kujaribu kuchonga (kufanya) na kuabudu sanamu, kama ifuatavyo:
"
Usijifanyie sanamu ya kuchonga, mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, au kilicho chini duniani. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, nawapatiliza wana uovu wa baba zao; hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao".
(Kumb 5:8-9).
Mwandishi ya kikatholiki
Adolphe-Napoleon Didron ambaye pia ni mtaalamu wa mambo ya kale (archaeologist) anasema: “
The cross has received a worship similar, if not equal, to that of Christ; this sacred wood is adored almost equally with God Himself.” Some say that the cross makes them feel closer to God when they pray. Others use it as an amulet, thinking that it protects them from evil. But should Christians use the cross as an object of veneration?
Je Alama hii inastahiki kupata heshima na umuhimu huu? Hilo ndilo swali kuu la kushughulika nalo.
Ushahidi wa kwanza kuwa msalaba una chimbuko na maana kwenye dini za awali za kipagani unapatika kwenye katiba yenyewe ya ukristo yaani biblia wanayoiita wao takatifu. Soma waebrania 12:2 kwa ufafanuzi zaidi.
Pia kuonyesha ujio na uwepo wa msalaba na mkanganyiko wa jamii ya waumini inayoifuata biblia, waweza kusoma 1wakorintho1:17-18 ambapo mitume wanatukuza tendo lililofanyika kwenye msalaba na siyo msalaba kama ilivyo sasa.
Kabla ya kwenda mbali lazima tukiri kuwa uchambuzi wetu utaonyesha jinsi msalaba ulivyokuwepo kama alama ya dini za kipagani hata kabla ya kuzaliwa kwa Bwana Yesu mwenyewe. Tutajaribu kufanya hivyo ili kuonyesha upagani ulivyopaganisha ukristo huku na ukristo ukikiristisha upagani na kufanya ndoa ya mashaka inayoendelea hadi leo.
Katika kamusi ya
Expository of new tastment words, yaani kamusi fafanuzi ya maneno ya agano jipya, inasema kuwa
msalaba kama alama ya kipagani ilianzia kule Ukaldayo (ambapo pia ndiko chimbuko la Ibrahimu). Kamusi hii inasema kuwa wapagani wa eneo hili waliitumia alama ya msalaba kama heshima yao kwa muungu wao wa kipagani aliyeitwa Tammuz ambaye kimsingi ni Nimrodi muwindaji na mwanzilishi wa himaya ya Babeli (Babylonian) iliyolaaniwa kuliko hata firauni.
Tammuz kwa ufupi aliitwa «
Tau» akitumia alama ya
T kama alama yake kuu au sahihi tuseme. Alama hii ya T kama ishara ya Tammuz pia ilitumika si ukaldayo tu bali hata Misri na asia wakati ule ikizingatiwa kuwa Tammuz aliweza kuabudia karibia maeneo hayo yote wakati wa himaya yake. Ezekiel 8:12-16,
Msalaba pia unaweza kupatikana katika jamii za Kimisri za kipagani za hapo mwanzo. Ushahidi huu unapatikana kule kwenye jengo la
Amenopolis IV kule Tabes nchini Misri. Msalaba huu unajulikana maarufu kama «
Msalaba wa Misri au Msalaba wa tau. Hii ni kutokana na baadhi ya kazi za wanahistoria maarufu wa zama zile. Msalaba huu ulikuwa na mduara upande wa kichwani ukiashiria alama ya Tammuz akiwa kama muungu jua hapo baadaye.
Pia katika maeneo ya
Ufoenike, China na Mexico inapatikana dhana nzima ya matumizi ya kidini ya msalaba kama alama yao kuu. Ikumbukwe kuwa yote hii ni kabla ya kuzaliwa kwa Yesu hivyo kabla ya ukristo.
Jamiii nyingine unapopatikana msalaba kama alama shufaa ni maeneo kuanzia nchi ya
Niger ya sasa hadi mto Nile. Kwani ngao za mashujaa wa eneo hili zilichorwa alama hii kama ishara ya utaua na ukuu. Vile vile kwenye dini ya Uhindu unajulikana kama
The swastika, wagiriki wao wana msalaba unao itwa
crux gammata, composed of four Greek uppercase gammas (
Γ),
Ushahidi madhubuti waweza kupatikana pia nchini Mexico ambako msalaba maarufu wa
Palengue unapatikana. Kwa anayetaka ushahidi zaidi juu ya hili aweza kusoma kwenye
“T
he catholic encyclopidia“ ambayo licha ya kuuita msalaba wa Palengue inauita msalaba wa kabla ya ukrist wa Palengue.
Msalaba huu nchini uliitwa pia
Tota ama baba kama ambavyo baadaye uliitwa kwenye biblia. Soma Yeremia 2:27 hii imebainika kuwa upotofu mkubwa kuanzia lugha hata matumizi ya neno baba kumaanisha msalaba.
Nchini Misri inapatikana pia michoro au picha ya Muungu Amon akiwa ameshikilia msalaba wa Tau.
Pia kwenye hekalu la
serapis kule Alexandria lilibeba alama ya msalaba.
Hata kwenye vita baina aya Alexander Mkuu (
Alexander the great), na waajemi, waajemi walibeba msalaba kama alama yao ya ushindi. Pia hapa ikumbukwe kuwa utumizi wa alama ya msalaba kwenye vita ilianzishwa na akina
Nebkadneza na wenzake kama alama ya ushindi.
Kwa ufupi angalau msomaji anaweza kuona utamaduni huu wa kuutukuza na kuutumia msalaba ulikotoka kuwa ni kwenye dini za kipagani za kale. Hiki ndicho tulichomaanisha tuliposema kuwa upagani umepaganisha ukristo na ukristo umekristisha upagani na kufanya ndoa kuu ya uwongo na mashaka.
Hebu tuhame twende nchini Italia ambako ndiko chimbuko hasa la ukristo chini ya himaya ya kiroma. Mwaka 46 kabla ya kuzaliwa Yesu, kunapatikana sarafu za muungu jupiter zikiwa na alama ya msalaba ambao kwa wapagani wa kiitaliano ulitumika kama hirizi au sihiri kama unavyotumiwa na baadhi ya madhehebu ya kikristo kwa sasa.
Hata ukiangalia sarafu aliyoletewa Yesu alipe kodi ilikuwa na Maandishi
Partem max yaani baba mkuu ambaye alikuwa ni kaizari, ilikuwa na alama ya msalaba. Hilo leo siyo mjadala wetu hivyo tutalitumia kwenye ushahidi huu tu.
Hata kule Ugiriki ulichorwa msalaba kwenye vibanio na nembo ukiwa ni alama ya mfalme wao aliyefanana sana na
Tammuz.
Tusiwachoshe na rejea na ubukuzi na uchokonozi. Hebu tujiulize swali rahisi. Je msalaba hadi hapa ni alama ya Kimungu au kimiungu? je inaingia akilini hadi leo mtu kuendelea kuutukuza na kuuvaa shingoni ikiwa ni kama kinga au hirizi kwake? je kama mtu atategemea kulindwa na msalaba huyo Mungu atafanya kazi gani!?
Je inaingia akilini kuendelea kuutumia msalaba kwenye mahekalu ya Mungu, nyumba zetu, makaburi yetu, kuuchora kwenye vipaji vya uso kila mtu aingiapo kanisani na mengine kama hayo? Je ni nani mwehu huyo awezaye kuivaa shingoni bastola au kisu kilichotumika kumuua mpendwa wake kama kinga au japo kumbu kumbu tu? kama hata akili nyepesi ingetumika basi bastola ingeogopewa kiasi cha kutisha kwani ndiyo iliyouchukua uhai wa mpendwa wako. Je ni nini mantiki ya wakristo kuvalishwa kongwa bila wenyewe kujua asli?
Je inaingia akilini kwa mtu ambaye amejua maana na chimbuko la msalaba kuendelea kuivaa hiyo kongwa na alama ya laana? kazi kwenu. Je anayefanya hivyo anaendelea kuwa mkristo wa kweli au mpagani wa kawaida tu hata akijiita mkristo?
Hatulengi kudhalilisha imani za wenzetu wala kuwaonyesha kama majuha lakini ni ujuha kutumia alama ya kipagani ambao kimsingi ndiye adui mkubwa wa dini. Tunaandika haya kwa kuzingatia ushauri wa bure lakini wa maana. Yesu Alisema kuwa mkiitafuta kweli itawaweka huru kweli kweli. Kama hivyo ndivyo kwanini nasi tusiwaweke huru kweli kweli ?
Kwa taarifa yako msomaji msalaba umekuwa nongwa hasa kwa wakatoliki. Kwani huchora alama ya msalaba kila waingiapo kanisani, kunywa au kula, wakati wa kulala wakati wa kuamka n.k Pia msalaba huchorwa kwenye mwili wa mtu tangu siku ya kuzaliwa (kubatizwa) hadi kuzikwa huku kaburi lake likiubeba milele !
Kwa waroma msalaba uko kila mahali. Kwenye meza, makanisa, hata tumbo la kanisa limejengwa kwa ishara ya msalaba, hata kwenye vikombe wanavyotumia kanisani hufunikwa kwa kitambaa chenye alama ya msalaba. Kwa taarifa yako ni kwamba padre hufanya alama ya msalaba mara 16 wakati akiendesha misa huku akiongeza mara 30 za kuibariki altare!
Kama kweli msalaba ni alama ya laana na ya kipagani huku ni kufanya nini kama siyo kuwalaani waumini hata madhabahu yao. Je hapa kunaweza kuepukika kwa mabalaa na majanga yanayolikumba kanisa kama vile ulawiti na uzinzi wa mapadre wake?
Imekuwa ni jadi kwa mkristo kujilaani kwa kila afanyalo. Hali wala hanywi bila kujitia alama hii ya laana.
Hata tukiambwa kuwa msalaba unatumiwa kama alama ya kusulubiwa kwa Yesu ambaye ni alama ya ukombozi wa kinjozi, bado haiingii akilini kwani zana na nyenzo hii ilianza kutumika kabla ya kuzaliwa na kusulubiwa kwake.
Je ni wapi ukiachi siku ya kusulubiwa ulipoona Yesu na wanafunzi wake wakiongozana na msalaba kwenye shughuli zao za kueneza injili?
Tuhitimishe. Huko Misri, Ugiriki , Syria na Karthago, Palestina na Roma msalaba pia ulitumika kuwaadhibia wahalifu waliokuwa wametenda maovu makubwa kama alama ya kulaaniwa kwao.
Kimsingi msalaba na matumizi yake vimepotoshwa sana kama ilivyo kwa dhana kuu ya ubaba. Soma Matayo 23:9-11. tukiache magube ya kanisa, hili liko wazi kuwa msalaba hauna uhusiano na ukristo wala dini aliyoileta Yesu. Huenda tukikubali kusema kuwa Ukristo siyo dini aliyoleta Yesu twaweza kuyakumbatia na kuyakubali matumizi ya msalaba kwa raha bila ubishi.
Lakini si kosa la kanisa. Kwani kama hadi leo halijamjua Yesu mwenyewe litajuaje upogo na najisi ya msalaba kwa kazi ya Mungu?
Tuhitimishe kwa kumnukuu Bwana
J. D. Parsons katika kitabu chake kiitwacho T
he Non-Christian Cross anaelezea kuwa:
“
There is not a single sentence in any of the numerous writings forming the New Testament, which, in the original Greek, bears even indirect evidence to the effect that the stauros used in the case of Jesus was other than an ordinary stauros; much less to the effect that it consisted, not of one piece of timber, but of two pieces nailed together in the form of a cross.”
Nakaribisha hoja juu ya kuyavinjari haya tunayoletewa. Huu ndiyo wakati muafaka wa kuhoji na kuhoji na kuhoji hadi kweli ipatikane ili ituweke huru kweli kweli.