Alaji alaji alaji watuu weeeeeeeweeeeee dom | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Alaji alaji alaji watuu weeeeeeeweeeeee dom

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Apr 12, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Apr 12, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,358
  Likes Received: 5,656
  Trophy Points: 280
  CCM washangilia kuondoka Makamba  *Wala na kunywa Dodoma kujipongeza

  Mwandishi Wetu

  WAFANYAKAZI wa CCM Makao Makuu Dodoma wamejipongeza kwa kula na kunywa kwa kile wanachosema ni kufurahia kuondolewa ofisini kwa
  aliyekuwa Katibu Mkuu, Bw. Yusufu Makamba jambo walilokuwa wanalisubiria kwa muda mrefu.

  Baadhi ya wafanyakazi hao waliokutwa na Majira katika maeneo mbalimbali ya starehe mjini Dodoma wakizungumza bila kutaka majina yao yaandikwe gazetini, walisema kwamba furaha yao hiyo imenogeshwa zaidi na kuondolewa kwa sekretarieti nzima ambayo ilikuwa mzigo mkubwa, sio kwa chama tu bali pia kwa watumishi wa chama.

  Walisema uwajibikaji wa watumishi ulipungua kutokana na maamuzi binafsi ya Bw. Makamba ambayo kila mara yalitolewa bila kuzingatia taratibu za utumishi na ajira. Kwamba baadhi ya watumishi walihamishwa kibabe kwa amri yake kwa sababu binafsi.

  "Kuondoka kwa uongozi wa Makamba kwetu ni sawa na kuzaliwa upya, ndio maana tuko hapa tukiburudika kwa furaha na kupongezana. Kuondoka kwao haikuwa kazi ndogo kwani tayari baadhi ya wajumbe walishapewa kiasi kikubwa cha pesa ili kukwamisha na kuhujumu uamuzi wa kuwaondoa madarakani," alisema mmoja wa wafanyakazi hao.

  Mwingine alisema, "Ni kweli chama kimepoteza mvuto kwa wananchi kiasi kwamba hata sisi watumishi tunapata shida na aibu kila tunapoumbuliwa na kukejeliwa na wananchi mitaani. Hatuna la kusema wananchi wanapokilalamikia chama, lakini viongozi kwa sababu za uswahiba wao usio na kikomo wanakauka au kutoa matamko ya ajabu dhidi ya wanachama na wananchi kwa ujumla."

  Walisema ni matarajiio yao kwamba sasa baada ya kujiuzulu kwa wajumbe wa Kamati Kuu, chama kitakuwa na sura mpya na safu makini ya uongozi, ambayo pamoja na mambo mengine itajenga mshikamano na kuelekeza nguvu na kasi zaidi katika kupambana na ufisadi jambo ambalo ndio maradhi yanayodhoofisha afya ya CCM.

  Aidha kwa nyakati tofauti watumishi hao walishauri kwamba uamuzi mgumu uliochukuliwa na chama usiishie kupanguana katika nafasi za uongozi tu, bali utazame na kuwamulika hata wale wanaoendeleza makundi yanayokigawa chama kwa lengo la kutafuta uongozi wa juu, kwani wanakwaza juhudi za utekelezaji wa ahadi na ilani ya chama.

  Pia walikumbushia kurejewa kwa dhamira ya rais ya kutenganisha mambo ya siasa na biashara. Tumeona wafanyabiashara walivyotuvuruga, hivyo sasa ni muda mwafaka kujitoa mikononi mwao na kurejea kwa wananchi wakulima na wafanyakazi ambao ndio wenye chama, alidokeza mwingine.

  [​IMG]
  :
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Apr 12, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  majizi makubwa hayaa...hayana lolote
   
 3. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Au makamba alikuwa aanabana!
   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  Apr 12, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,358
  Likes Received: 5,656
  Trophy Points: 280
  Umeonaaaa eeeeeeeeeeeeeeeehhhhhhhh!!!!!!!!!!!!!!!
   
 5. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #5
  Apr 12, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  the way i see the problema in that party was not Makamba alone. ni kama ametolewa kama mbuzi wa kafara. shida kubwa ni ufisadi ndani ya chama hicho. cdm wako wapi kueneza sumu ya mabadiliko vjjn? hawatavuna kitu 2015 kama hawafanyi kazi sawasawa vjjn ambako ndo umma mkubwa wa watz uliko. Ile taa ya mchana iliyowashwa na vjana songea imefika wapi sasa? inaendeleaje? I saw it as a good move.
   
Loading...