Al Shabaab wapata kichapo Mogadishu

Al Shabaab wapata kichapo Mogadishu

Nazjaz

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2011
Posts
7,802
Reaction score
9,280
Kikundi cha wapiganaji wa Kiislamu wa
Somalia, al Shabaab, kinasema kuwa
kimeondoka katika vituo vyake kadha ndani
ya mji mkuu, Mogadishu.
Wakaazi wameiambia BBC kwamba waliona
misafara ya wapiganaji ikiondoka katika mji
huo.
Kuhama huko kunafuatia mapigano makali
jana usiku.
Kikosi cha Umoja wa Mataifa kinachoisaidia
serikali ya Somalia kimekuwa kikipigana na
al Shabaab mjini Mogadishu katika siku za
karibuni; ili kuweza kufikisha msaada wa
chakula kwa wale walioathirika na ukame
nchini Somalia.
Haijulikani kama wapiganaji hao
wameondoka kabisa.
Msemaji wa serikali alielezea huo kuwa
"ushindi wa dhahabu" kwa watu wa
Somalia.
Lakini al Shabaab, ambayo inadhibiti
sehemu kubwa ya kusini mwa nchi, ilisema
wameondoka kufwatana na mikakati yao na
iliahidi kufanya shambulio la kulipiza.
Baadhi ya wadadisi wanafikiri al Shabaab
imepungukiwa na fedha kwa sababu
wafadhili wao wa Arabuni
wamewapunguzia msaada tangu al
Shabaab kudhoofika kijeshi.
Wadadisi wanasema al Shabaab imewahi
kuwahamisha wapiganaji wake mjini
Mogadishu siku za nyuma, lakini safari hii
inaonesha kuondoka kwao ni ushindi
mkubwa kwa serikali.
 
Inaelekea una ndoto kuwa iko siku utasikia Alshabaab imekufa na Somalia iko salama chini ya African Union ikiongozwa na Uganda na Burundi.Hili milele halitotokea.
Njaa ikiisha wanarudi mjini.Hivi sasa pia huko waliko hawakamatiki.
Jiulize taifa kubwa kama America linakufa pole pole kwa kiu yake ya kutaka kuuwa uislamu Iraq na Afghanistan itakuwa Burundi na Uganda!.
Jana tu Askari shujaa wanaoitwa seels 30 wameuliwa Afghanistan.
 
Wameondoka kwa sababu ya njaa au wamepigwa??
 
Inaelekea una ndoto kuwa iko siku utasikia Alshabaab imekufa na Somalia iko salama chini ya African Union ikiongozwa na Uganda na Burundi.Hili milele halitotokea.
Njaa ikiisha wanarudi mjini.Hivi sasa pia huko waliko hawakamatiki.
Jiulize taifa kubwa kama America linakufa pole pole kwa kiu yake ya kutaka kuuwa uislamu Iraq na Afghanistan itakuwa Burundi na Uganda!.
Jana tu Askari shujaa wanaoitwa seels 30 wameuliwa Afghanistan.

watu wengine sijui mnafikiria na akili za wapi,
kwa hiyo unaona uganda na burundi hawafanyi lolote,naona melewa dini, wauwaji ndio unawaita mshujaa, unafaidi nini kufurahia vifo vya wamarekani
kama Mungu wenu angekuwa anasikia basi angekuwa ashawaangamiza wamarekani, dua zenu mbaya ni baraka kwao.
 
nani kakudanganya?
 
Jana tu Askari shujaa wanaoitwa
seels 30 wameuliwa Afghanistan.

unajua mambo mengi kweli mkuu
 
Afadhali tena waondolewe kabisa ili misaada ya kibinadamu iweze kuwafikia wanawake na watoto ambao ndio kundi kubwa linaloharika
watu wengine sijui mnafikiria na akili za wapi,
kwa hiyo unaona uganda na burundi hawafanyi lolote,naona melewa dini, wauwaji ndio unawaita mshujaa, unafaidi nini kufurahia vifo vya wamarekani
kama Mungu wenu angekuwa anasikia basi angekuwa ashawaangamiza wamarekani, dua zenu mbaya ni baraka kwao.
 
Ami,
ningekuwa nakujua tukikutana usiku nakukimbia aisee. Hiyo post yako tu inatosha kunikimbiza.
 
Back
Top Bottom