HUYU HAMISS77, NI KATI YA WAPOTOSHAJI WAKUBWA.....
Ni sawa na kuambia watu kuwa; CCM maana yake ni Chama Cha Mambuzi na sio CHAMA CHA MAPINDUZI au kusema FFU ni fanya fujo Uone na sio Field Force Unit nk nk
yaani anachukua habari sahihi; anaifanyia tafsiri anayotaka....AKIJUA WATU WOTE NI WAJINGA WA KUMUAMINI......Shame on him!!!
HUYU; KAMA AMESOMA BIBLIA/AGANO LA KALE, IWEJE HAJUI HABARI ZA ISHMAEL NA MAMA YAKE AMBAZO ZIME ELEZWA VIZURI, SAWA SAWA NA KWA WAISLAM? ANAKUJA HAPA KUTULETEA HADITHI FEKI ZA KITAPELI eti Ishmael alipeleka mjini Maka kukiwa na msikiti, Wakati Biblia inatuambia kabisa, kuwa waliachwa jangwani na hapakuwa na kitu chochote..... Shame on him!!!
UTAONA KABISA ANAKWEPA HIZI HABARI KWA SABABU NDIPO MSINGI WA UISLAM ULIPO (AL-KAABA nk nk)
NAAMINI HATA YESU HAWEZI KUKUBALI WAPOTOSHAJI KAMA HAWA, ETI NI WAFUASI WAKE?
AENDELEE TU NA HUU UPOTOSHAJI SIKU ZA MWISHO, YESU AMKATAE NDIO ATAJUA HAJUI!!!
Wewe Bado mdogo sana kwa hii mijadala ,kwanza hujui historia,hujui uislamu,hujui biblia
Hujui Geography location ya mashariki ya kati
Kwanza kabisa, tulia.
Hakuna anayekwepa habari za Ishmael na Hajar.
Sisi tunasoma maandiko yalivyo, si kuyaongeza wala kuyapunguza.
Biblia inasema wazi
“akapotea katika jangwa la Beer-sheba.”
(Mwanzo 21:14)
Hapo ndipo Hajar na Ishmael walienda. Si Mecca. Si Saudi Arabia. Ni Beer-sheba eneo la kusini mwa Kanaani.
Biblia pia inasema
“
Mungu akafungua macho yake, akaona kisima cha maji.”
(Mwanzo 21:19)
Biblia haisemi
Zamzam
Mecca
Kaaba
Msikiti
Hija
Jiwe jeusi
Sasa swali la msingi ni hili
Kama hadithi ni “sawa sawa” kwa Wakristo na Waislamu, kwa nini vitu hivi vyote havipo kabisa kwenye Agano la Kale?
Hapo ndipo tatizo linaanza.
Wewe unasema
“Biblia inasema waliwekwa jangwani na hapakuwa na kitu.”
Ndiyo, ni kweli. Lakini jangwani la wapi?
Biblia imeweka jina,Beer-sheba.
Kwa nini unakataa jina hilo halafu unataka kulibadilisha kuwa Mecca?
Ukisoma Mwanzo 16 na 21 kwa uangalifu utaona
Ishmael alizaliwa Kanaani
Alikulia Kanaani
Alifukuzwa akiwa kijana (si mtoto anayenyonya)
Akaenda jangwa la Beer-sheba
Akaishi “jangwa la Parani” (Mwanzo 21:21)
Parani ipo Sinai / Negev, si Mecca.
Sasa hoja yako inajikanganya. Unasema hakuna msikiti wala kitu chochote sawa kabisa.
Lakini hadithi ya Bukhari ndiyo inayotaja
“mahali pa juu kabisa kwenye msikiti karibu na Kaaba”
Swali
Msikiti gani wakati Uislamu haukuwepo?😂😂
Kaaba gani wakati hakuna ushahidi wa kihistoria wa karne ya Ibrahimu huko Mecca?😂😂
Hapa ndipo unaona wazi kuwa hizo ni simulizi za baadaye, si historia ya karne ya Ibrahimu.
Na kuhusu kusema
“Ndipo msingi wa Uislamu ulipo”
Hapo umesema ukweli bila kujua.
Ndiyo, msingi wa Uislamu umefungwa kwenye hadithi ya kuhusisha Kaaba na Ibrahimu.
Lakini tatizo ni hili
Hakuna maandiko ya Kiyahudi.
Hakuna maandiko ya Kikristo.
Hakuna ushahidi wa akiolojia.
Hakuna rekodi ya kale ya Kiarabu ya kabla ya Uislamu
inayosema Ibrahimu alifika Mecca.
Historia ya Ibrahimu imeandikwa na Wayahudi karne nyingi kabla ya Muhammad.
Kama kweli alifika Mecca, kwa nini hakuna hata mstari mmoja katika Torati?
Hapa si suala la kupiga kelele au kusema “Yesu atamkataa fulani.”
Yesu mwenyewe alisema:
“Utaijua kweli, nayo kweli itawaweka huru.” (Yohana 8:32)
Kweli haiogopi uchunguzi.
Na ukweli ni huu, Biblia inamuweka Ibrahimu Kanaani.
Uislamu unampeleka Mecca. Moja lazima iwe sahihi na maandiko ya kale ndiyo yana uzito wa kihistoria.
Sasa swali ni hili
Ni nani aliyekuja kwanza kihistoria?
Torati au Muhammad?