Mkuu Junius pamoja na nafasi inayoonekana kwa Dr Mohamed Al-Baradei,Lakini Ukweli wa mambo ni kwamba Mtoto wa pili wa Rais Hosni Mubarak,Ndiye ana nafasi kubwa,na karibuni Taasisi zote za Uarabuni na Ulaya zinazojihusisha na mambo ya siasa zinampa nafasi .Mtoto huyo Gamal Mubarak ana umri wa miaka 47 na anafanya kazi kama investment Banker huko London (UK) na nyumbani Misri ana wadhifa wa Katibu Mkuu Msaidizi wa chama kinachotawala Nchini Misri kijulikanacho kama National Democratic Party (NDP).
Nafasi ya Gamal ilionekana wazi baada ya baba yake kumchagua Dr.Ahmed Nazif,kuwa Waziri Mkuu Julai/2004,Dr Nazif alishawahi kuzungumza katika hadhara (American University in Cairo) kuwa "Gamal ana nafasi kubwa kuja kuwa Rais wa Misri".Dr Nazif ni Rafiki Mkubwa wa watoto wa Rais Mubarak (Alaa na Gamal)
Gamala anakubalika pia na Mataifa ya Magharibi yakiongozwa na Marekani,amekwishawahi kufanya ziara Nchini Marekani mwaka 2003 na 2006,katika Ziara hizo alikutana na Viongozi wakuu wa serikali ya Marekani akiwamo Dick Cheney,Collin Powell,Condolezza Rice na Donald Rumsfeld.Ukimuacha Gamal watu wengine wanaozungumziwa Nchini Misri kwamba wana nafasi ya kuongoza Nchi hiyo ni waziri wa Ulinzi na Mkuu wa Usalama wa Taifa Nchini humo,lakini wote wawili wana umri mkubwa,wapo katika umri wa miaka 70+
Rais Hosni Mubarak mwenye umri wa miaka 81 bado hajasema kama hatogombea tena katika uchaguzi utakaofanyika 2011.lakini watu wengi wanasema Rais Mubarak ameonyesha nia ya kustaafu.Mubarak amekuwa Rais wa Misri toka mwaka 1981 baada ya kifo cha Rais Anwar Sadat.