Akubaliwa kirahisi

Akubaliwa kirahisi

Viol

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Posts
25,419
Reaction score
18,368
Jamaa alimtongoza msichana ambaye alikuwa anasali naye kanisa moja,msichana akamwambia nipe mda wa kusali ili mungu anionyeshee kama we ndo mme wangu wa ndoa,jamaa akampa mda wa mwezi moja,mwezi ulipoisha akamfuata ili apewe jibu,msichana akajibu kwamba mungu hakunionyesha kwamba we ndo mme wangu.Jamaa akamwambia basi nipe na mimi mwezi mmoja nisali ili nihakikishe kweli kama mungu alinidanganya,najua mungu atafanya kitu cha pekee ili uone mi ndo mme wako.basi msichana akampa jamaa mda wa kusali.Kwa vile msichana alikuwa anaishi kwenye nyumba ya nyasi jamaa siku moja usiku wa manane akaenda nyumbani kwa huyu binti,akapanda juu ya nyumba na kufunua nyasi halafu akamwulika demu machoni kwa tochi huku akisema,''Selina mi ni malaika wa bwana,nimetumwa kwako na mungu kuwa Zakaria ndo mme wako halali wa ndo,mungu amesikia kilio cha zakaria,usiufanye moyo wako kuwa mgumu mana ghadabu ya mungu itawaka juu yako''......halafu jamaa akaondoka zake.Kulipokucha asubuhi msichana alimtafuta jamaa na kumwambia naomba nisamehe,Malaika amekuja kuniambia we ndo mme wangu,nimekubali ombi lako.
 
Ngoja wenye dini zao waje.....mie namalizia nguruwe wangu hapa!
 
Kweli wanaume ni wabishi si mchezo
 
mwe mwe mwe mweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee! usijesababisha wengine wakashikwa juu ya paa kwa style ya yule jamaa wa tabata.
 
nitafanyaje kosa hilo nami nakuja mwenyewe kumwakilisha kwakuwa hutaki kuelewa somo mwaka unakaribia kukatika.

hahahaha! Kuanzia leo somo nimelielewa nisije nikashindwa kulala kwa uoga.lol
 
Back
Top Bottom