Akomae au niendelee kumtafutia kazi?.

Akomae au niendelee kumtafutia kazi?.

Johnny Bravo

Senior Member
Joined
Dec 4, 2013
Posts
107
Reaction score
46
Ndugu yangu amemaliza chuo na amepata kazi mshahara hauzid 300k.

Je tuendelee kutafuta kazi au atulie kwanza hapohapo maana sehemu nyingi

tulizo enda wanadai ana vyeti vizuri ila hana experience kazini.
 
Yeye hawezi kujitafutia kazi mwenyewe mpaka nyie mumtafutie?
 
Muache apate ujuzi hapo japo miaka miwili! Lakini kama unaweza pata kimemo basi mtafutie kazi nyingine.
 
Mkuu, nisaidie kujibu maswali haya kisha nitatoa ushauri:

-Wanampa ofa nyingine kama breakfast, lunch na chumba cha kulala?
-Yupo mkoa gani (Gharama za maisha zimetofautiana kutokana na maisha)?
-Atakua anakaa kwa ndugu au wazazi au ndio anaanza kujitegemea rasmi?
-Eneo la kufanyia kazi na anapo kaa, panahitaji usafiri (daladala) kwenda na kurudi kila siku?

Njoo jibu haya maswali mambo tuyaweke fresh.
 
kaka fanya cost-benefit analysis.
kama akifanya hapo hapotez chochote muache hapo na hata kama mshahara unaishia kwenye nauli na kula.
uzoefu kwanza
 
  • Thanks
Reactions: HMS
Akomae tu atajiupgrade mwenyewe huko kazini kwa ufanisi wake wa kazi.....kazi zenyewe ngumu siku hizi
 
  • Thanks
Reactions: HMS
ndugu yangu amemaliza chuo na amepata kazi mshahara hauzid 300k.

Je tuendelee kutafuta kazi au atulie kwanza hapohapo maana sehemu nyingi

tulizo enda wanadai ana vyeti vizuri ila hana experience kazini.

hili nalo ni la kuomba ushauri kweli? Nina mashaka kuwa wewe na ndugu yako wote hamjitambui.
 
  • Thanks
Reactions: HMS
Mwambie aache hiyo kazi halafu mshinde pamoja nyumbani hiyo 300k ataendelea kulipwa si amefunga mkataba?
 
  • Thanks
Reactions: HMS
Yeye hawezi kujitafutia kazi mwenyewe mpaka nyie mumtafutie?

co kila mtu anatafuta mwenyw kazi..wengine wanatafutiwaa na wenyw wanatafuta pia.ukipata ndugu wa hivi wanokujali raha sana
 
  • Thanks
Reactions: HMS
Kazi gani analipwa pesa kidogo hivyo, maana mimi housemaid wetu tunamlipa laki tatu !
 
Mkuu, nisaidie kujibu maswali haya kisha nitatoa ushauri:

-Wanampa ofa nyingine kama breakfast, lunch na chumba cha kulala?
Hapana
-Yupo mkoa gani (Gharama za maisha zimetofautiana kutokana na maisha)?
DSM
-Atakua anakaa kwa ndugu au wazazi au ndio anaanza kujitegemea rasmi?
Inabidi ajitegemee
-Eneo la kufanyia kazi na anapo kaa, panahitaji usafiri (daladala) kwenda na kurudi kila siku?
Nauli 2000

Njoo jibu haya maswali mambo tuyaweke fresh.

Yawek mtu wangu
 
watu tunatafuta hata kazi ya laki mbili nn laki tatu!!! akomae tu akiwa kazini anapata experience... endelea lakini kumtafutia!!!
 
Muache akomae hapo2 akili ifunguke kwa huo mshahara naona wanamfundisha wizi pia ivi achangamke na deal yyt hapo ofisini
 
Mwambie akae nyumbani kwanza kazi nzuri zitamfuata asihofu.. hiyo ya laki tatau mwambie aipige chini wadau wengine waichukue.
 
Mwambie afanye hiyo ya laki tatu huku anatafuta nyingine yenye maslahi zaidi. Siku hizi kupata kazi ni shida graduate wapo wengi
 
Back
Top Bottom