Huyo mdada ana mtu ambaye hao rafiki zake ametambulishwa kwao na wewe unakuwa kama mshika pembe na anakupotezea ili rafiki zake wasikujue. Au anaona aibu kuwa na mtu kama wewe, huenda marafiki zake wanapokutana huwa wana wapenzi wao wa aina Fulani so anaona aibu kuwa nawe mbele yao. Mie iliwahi kunitokea hiyo kwa mke wangu wangu niliye naye sasa na ilifika kipindi nikajitoa kabisa na kumuondoa moyoni na kumpiga chini ndipo alipogundua kuwa nilikuwa na upendo wa kweli kwake ila hatua ilikuwa na athari kubwa kwetu maana alitamani kurudi na akarudi wakati mie nimetoka tayari. Kuwa makini kwa maamuzi huenda wakati mwingine sio kwamba anakusaliti au la! bali ni kutojielewa na kutofautisha marafiki na mahusiano. Kiufupi bado anakupenda sana ila marafiki wamemshika akili na atakuja kushituka wakati na wewe umetafuta wa kuwa naye pindi hao marafiki zake wanapokuja iringa.
Hao marafiki zake wanafanya Kazi gani mpaka wawe na uwezo wa kuja Iringa kula raha Kila baada ya miezi miwili?
Huenda huwa wanaletwa na watu wao huko Iringa na hao watu wao wana fedha hivyo gf wako anaona aibu kuwa na wewe pindi awapo na rafiki zake sababu wewe huna kitu au anahisi huna hadhi kama hao wapenzi wa rafiki zake
Next time wakija nenda nao huko kwenye bata halafu utajua mbichi na mbivu
Huyo anza kuwanae makini toka hivi sasa kwa dalili izo anaonesha anashawishika kilaisi sana so inawezekana siku moja akakuacha kwenye wakat mgumu sana kuliko huu unaouwona sasa.
Ongea na mpenzi wako umueleze seriously hiki kitu hupendi kama ana akili na anathamini mahusiano yenu atabadilika. Huu ndo mda wa kumjua ukishamuoa itakuwa ngumu ku-undo. Ukiona pamoja na kumueleza mara mbili tatu bado hajali ujue hata huko kwenye kifungo cha maisha mkishaingia atakuwa hamsikilizani. And remember, "There is Always Plan B"
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.