Mangi flani hivi
JF-Expert Member
- Jan 2, 2016
- 2,026
- 3,104
Salaam,
Kwanza niseme kuwa hili ni jiwe la gizani, na yeyote litakayemtwanga atulie kimya.
Kipindi cha nyuma kidogo kulikuwa na harakati nyingi sana za kuwasema na kuwakebehi akina mama mkwe Wazazi wa mume. Walisemakana wana gubu, wana fitina, wivu, Maneno na kila aina ya ubaya. Zikatungwa nyimbo, maigizo, vitabu, mashahiri na kila aina ya sanaa ili tu kumkomesha mama wa mume ailete kiherehere.
Wanaume tulivyokuwa na moyo wa huruma, tukakubaliana na hayo maneno, na sisi tukaja na kauli mbiu kibao za kuwazuia mama zetu wasilete balaa kwenye ndoa zetu. Mara ooooh! Mama akija kwako asikae Muda mrefu, mara ooooh! Msaidie mama yako akiwa hukohuko kwake nakadhalika. Tukasahau kabisa kuwa tunafunga mlango mmoja tunafungua mwingine hatari zaidi.
SASA:
Mimi nilidhani hiki kikombe nakipitia mwenyewe ni mpaka nilipopokea SMS toka kwa mangi mwenzangu akiniomba niende kwake nikamkomboe maana Kama ni Maneno ameyasikia yote.
Nilipofika nilimkuta kakaa getini Shati lipo begani amevaa malapa. Tulipofika mahali tukakaa ndo akanielezea balaa la mama wa Mke wake na Maneno anayoyasema hapo nyumbani kwake. Kama utani nikamuuliza kwanini huwaambii wazee wako au baba mkwe?? Sababu aliyonipa ilinifanya nigundue kuwa wanaume tutakufa sana na tai shingoni kwenye hizi ndoa, kwa kujifanya ngunguri.
Nihitimishe kwa kusema nyie mama wazaa wake zetu, kaeni na waume zenu mle pensheni. Acheni kuingilia ndoa za watoto wenu, ndio maana wengine wanajikuta wameliwa na wakwe zao.
Wakwe mmekuwa kama mabibi afya mnakuja kwa watoto wenu Kama mnakagua vyoo vya stendi. Sitavumilia tena.
Ya kwangu sitayasema hapa. Naomba wewe mkwe wangu, ujirekebishe upesi, ukija tena kwangu na uzeleheba wako huo utachezea mabapa mbele ya mwanao. Pumbavu.
Na nyie wasanii geukeni sasa muwaseme na hawa wamama waliotuzalia hivi vizazaa.