Akina Dada wa kibongo Acheni Hizo.

Haya mambo ya chat room hayafai, na huwezi kupata mwenza online. Niliwahi kuwa na friend wa kike niliyekuwa nachati naye online, siku moja akaniuliza nipo pande gani za dunia, nikamwambia nipo Sumbawanga na siku hiyo ikawa ya mwisho kuchat naye.

Katavi,

Nakumbuka ulituaga kuwa unaenda kijijini kusherekea Noeli na mwaka mpya. Umerudi lini? Mbona hukutupa ripoti ya yaliyojiri? Jeshini tulifundishwa kuwa baada ya kufanya operation yoyote lazima mpiganaji atoe "ripoti ya maganda na risasi". Hebu basi tupe ya kwako. Risasi zimetumika au umerudisha zote?
 
Mkuu,

Labda wengine tumepitwa na wakati. Sipati jawabu kwa nini mtu amtafute mwenza online. Kwani walio "in line" au kwenye kwenye macho yake hawaoni? Hapa kuna udhaifu fulani watu wa namna hii wanajaribu kuuficha. Kama mtu anakitu anachokificha basi lazima atasema uongo tu! Hakuna kitu cha bei nafuu. Kwa hiyo ni poa tu wakidanyana kwa sababu wote wanatafuta njia ya mkato!

Lakini, kwa maoni yangu (tupende tusipende), pesa kwenye mapenzi ni kitu cha lazima. Suala la msingi ni kujaribu kuangalia matamanio yako na jinsi ya kuyatimiza katika mahusiano bila kusababisha usumbufu kwa mwenzio.
hapo nimekugongea senks mpwa,money should be involved in love,siongelei pesa za kuhonga etc,ila ni pesa za kuwawezesha kumove hapa na pale na kubadilisha mazingira na huyo mwenzi wako ,kama huna pesa baba duuuuh!
 
Mwezi uliopita nilikua benki moja ya kanda ya ziwa, ebana usimpimie mtu kivile.
Vijana wadogo wadogo wanaingia na mifuko ya rambo na KUWEKA (si kuchukua apo) mahela mpaka nilichanganyikiwa.
Nyie akina dada msiwadharau wa mikoani, kuna watu wanamiliki Lexas benki na hawasemi, mnakosaga bahati ivi ivi.

TEh LEXUS bank....?! Aliweke barabara ashuhudie mademu wakiomba lifti kwa foleni!
 
Mimi huwa nafawanyia research hawa viumbe kwenye mitandao mbalimbali ya urafiki na uchumba.

Mwanzoni tunachati fresh tu, linapokuja swala la kutaja sehemu nilipo, ndo hapo ninapowachezeaga akili hawa dada zetu.

Mara nyingi nikiwaambia niko mamtoni nachukua nondoz au napiga mgalala/box, basi maongozi yanakwenda vizuri mpaka kufikia mikakati ya kupanga engejimenti na harusi.

Asilimia kubwa pia huendelea kuchati nami, iwapo nitawaambia niko Dar, na niko kwenye ofisi flan kubwa hapa mjini.

Usilongwe ukawaambia ukweli hawa viumbe, kuwa uko Tandahimba,Ukwale au mikoani huko hasa ya pembezoni, hupotea ghafla na namba za simu hubadilishwa.

Hivi nyie akina dada, fedha na kazi ni kitu gani hasa mpaka mvipapatikie kiasi hicho?

Hivi huwezi ukaanza maisha na mwenza wako kwa kulalia mkeka kwanza?

Hamuoni fahari kuanza maisha from the grass root na mwenza wako?

Hivi mke wa Obama alijua mmewe atakua rais, ndo akamkubali fasta?

Baba hii hoja sawia kabisa.

Lakini kupenda mteremko ni kadhia ya kawaida kwa wadada wengi sio tu wa kibongo. Popote duniani ukienda mara nyingi mapenzi yale ya dhati ni adimu kwelikweli kuyashuhudia ktk maisha halisi.

Tukumbuke kuwa tunaishi zama hizi za kila kitu kimebadilika. Vitu artificial ndio reality, cha msingi ni kuelewa mapema ishu ikoje na kuikabili.
 
hapo nimekugongea senks mpwa,money should be involved in love,siongelei pesa za kuhonga etc,ila ni pesa za kuwawezesha kumove hapa na pale na kubadilisha mazingira na huyo mwenzi wako ,kama huna pesa baba duuuuh!

Ahsante Zegere, ila umesahau kubofya kitufe cha senks. Hii ya maneno haiingii kwenye rekodi!!

Pesa ni mwisho wa maneno ndugu yangu. Ni Kigoma mwisho wa reli!! Hebu nenda sehemu uchungulie couples mbili zinapiga story. Moja inatesa na machips kuku, ice cream etc na nyingine inapambana na ugali mrenda au wali maharage kwa mama ntilie. Hawa watu watakuwa kwenye dunia mbili tofauti na nadhani hata nervous systems zao zitakuwa zinafanya kazi tofauti kabisa!

Wanaume wengi tunapenda kulalamika tu. Kama huna hela basi tafute size yako badala ya kutafuta mtoto wa geti kali halafu utake kumpa mlo mmoja kwa siku tena chakula chenyewe ni ugali na kauzu wa Mwanza! Mapenzi ya hivyo ni ya kufikirika. Lazima mwili ushibe kwanza kabla ya saikolojia kukaa sawa kwa ajili ya mambo ya mapenzi. Mungu awabariki nyote mnaohangaika kutafuta wenzi ila msilazimishe mambo.
 
This is not fair....I have seen a live example kutoka kwa kaka zetu wa bongo pia. Everyone is opportunist, so it works both ways.

No complains:)
 
Big up to all the ladies who fix men. Some deserve it, utashangaa huyo anayetaka kuchat na madem kila siku na kuwafix na maneno matamu ya uongo ana mke ndani au ana committed r/ship na mtu. so at the end of the day ni kuwaumiza roho wadada wote wawili. Njia ya kudeal na viumbe wa aina hii ni full usanii.
 
anajifanya kumwaga mboga na we unamwaga ugali kama mpwa Gorgie Prjie vile!!!!

wao wanaendaga kwa lengo la kudanganya afu wakimkuta demu nae kabobea kwenye usanii wanaona si fair!!! kutendwa tutendwe sisi tu kwa nini?? acha mchezo uwe fair bana!!
 
Mimi huwa nafawanyia research hawa viumbe kwenye mitandao mbalimbali ya urafiki na uchumba.

Mwanzoni tunachati fresh tu, linapokuja swala la kutaja sehemu nilipo, ndo hapo ninapowachezeaga akili hawa dada zetu.

Mara nyingi nikiwaambia niko mamtoni nachukua nondoz au napiga mgalala/box, basi maongozi yanakwenda vizuri mpaka kufikia mikakati ya kupanga engejimenti na harusi.

Asilimia kubwa pia huendelea kuchati nami, iwapo nitawaambia niko Dar, na niko kwenye ofisi flan kubwa hapa mjini.

Usilongwe ukawaambia ukweli hawa viumbe, kuwa uko Tandahimba,Ukwale au mikoani huko hasa ya pembezoni, hupotea ghafla na namba za simu hubadilishwa.

Hivi nyie akina dada, fedha na kazi ni kitu gani hasa mpaka mvipapatikie kiasi hicho?

Hivi huwezi ukaanza maisha na mwenza wako kwa kulalia mkeka kwanza?

Hamuoni fahari kuanza maisha from the grass root na mwenza wako?

Hivi mke wa Obama alijua mmewe atakua rais, ndo akamkubali fasta?

we kweli hutofautiani na jina lako pole sana
 
Na wa kaka hivo hivyo.

Hata hapa JF atakuuliza hivi upo wapi Dada, ukisema ukweli kwamba Upo Tanzania Shinyanga, ndo utakuwa umeua mawasiliano Hupati tena cha PM, thanks wala nini. Ila ukisema upo nje ya nchi hasa US na Europe hapo kitaeleweka, na kwa Tanzania at leaaaaaaast Dar, nje ya Dar forget it.

So its not abt Wadada peke yao, na Wakaka mna/wana tatizo hilo.

Kabla sijasahau....Happy New year 2010.

Asavali yangu niliyeamua kujiandikia kuwa nipo Sumbawanga, now sipati usumbufu haaata kwa facebook, maana marafiki baadhi washanidelete bila kuniambia! kaazi kweriii!!
 
Back
Top Bottom