Akina dada msipende kuwadharau vijana mnaofanyanao kazi ofisini

M2mishi

JF-Expert Member
Mar 2, 2013
714
267
Akina dada nipende kuwashauri kitu kimoja.

Msipende kuwadharau vijana mnaofanyanao kazi ofisi moja na kuwaona wa thamani kubwa watu msiowajua hasa wa kwenye mitandao mkidhani kuwa hao ndio wana maisha bora.

Ukweli ni kwamba akina dada wengi wanatabia ya kuwadharau vijana wanaoishinao wakiamini kwamba watawapata watu wenye sifa wanazozihitaji toka kwenye mitandao ya kijamii.

Matokeo yake kwa sasa kumekuwa na ongezeko kubwa la watoto wasiokuwa na baba au kwa jina maarufu kama watoto wa love connect, wakishazalishwa huko walikokimbilia na kuachwa ndio wanawaona wa thamani kubwa hawa waliowaacha mtaani.

Ushauri kwa wadada acheni tamaa rizikeni na vijana mnao ishi nao kwenye mazingira yenu kwani wengi wao ni watu wenye nia nzuri kwenu.
 
Mimi sio mtaalamu wa kiswahili wala si Mwalimu wa kiswahili kupangilia title na maudhui ila napeleka Ujumbe samahani kwa nilio wagusa
 
Ujumbe haujaeleweka, sasa wadada wa JF na hao unaofanya nao kazi au majirani zako waliokutenda vinahusianaje na kuchekesha kwao kukoje??? Hebu tueleze kisa chako labda tutakuelewa.....
 
Akina dada nipende kuwashauli kitu kimoja.

Msipende kuwadhalau vijana mnao fanya nao kazi ofisi moja na kuwaona wa thamani kubwa watu msio wajua hasa wa kwenye mitandao mkidhani kua hao ndio wana maisha bora.
Ukweli ni kwamba akina dada wengi wanatabia ya kuwadhalau vijana wanao ishi nao wakiamini kwamba watawapata watu wenye sifa wanazo zihitaji toka kwenye mitandao ya kijamii, matokeo yake kwa sasa kumekua na ongezeko kubwa la watoto wasio kua na baba au kwa jina maarufu kama watoto wa love connect, wakiisha zalishwa huko waliko kimbilia na kuachwa ndio wanawaona wa thamani kubwa hawa walio waacha mtaani.
Ushauri kwa wadada acheni tamaa rizikeni na vijana mnao ishi nao kwenye mazingira yenu kwani wengi wao ni watu wenye nia nzuri kwenu

Tuombe mungu tuu unaweza ukamjua mpaka mpaka kitovu chake kilipozikwa na akakutenda ukatamani akhera na bado mzima,chamsingi nikumtanguliza mwenyezi mungu mbele kwenye kila jambo khasa hili ....
 
Ujumbe haujaeleweka, sasa wadada wa JF na hao unaofanya nao kazi au majirani zako waliokutenda vinahusianaje na kuchekesha kwao kukoje??? Hebu tueleze kisa chako labda tutakuelewa.....
Jiwe limetupwa gizani ilooo ukisikia yalaaaaaaah ujue tayari uyo analo
 
Kiukweli hawa wadada inaweza ikawa ni kweli wengi wao wanapenda vya bure wanajisahau sana cjui wanajua kuwa na mtu mwenye pesa ndo kutafuta furaha maishani Mimi hata sielewi wakati mwingine nahic ndo adhabu zenyew wanazopata kupewa Mimba na kuachwa kwenye mataa hapo ndo anabaini mwanaume aliyemwacha het kwa kuwa hakuwa na pesa alikuwa na mapenz ya dhat kwake
 
Unajua sio kama wanawadharau, bali ni ile hali ya kukujua tabia zako vyema kwa vizuri kabsaa bila utata ndio inafanya tusiwe na nyinyi wa kazini au mitaani au mliotuzunguka karibu. pengine haziendani na matakwa yetu, hata kama ni wewe tumeishi mtaa mmoja na ulikwua unaona jinsi nilivyomjeuri kwa mama yangu na muda mwengine kuongea hata maneno ya kijeuri, akili yako inakuwa ishajenga mawazo ya kwamba huyu msichana hafai, lakini kuna mtu wa mbali kabsaa ananiona namfaa ni kwa vile hajui tabia zangu nyengine n.k., au wewe ulikuwa unaona jinsi nilivyokuwa nikigombana na dada zangu kisa usafi na kupika au kuchelewa kurudi n.k., kuna tabia tunajuana moja kwa moja zinaturudisha nyuma both side, kwa wanaume na wanawake.
 
Hivi ni kweli kina dada mmeshindwa kabisa kupambanua kuwa huyo chalii ni fake na huyu yuko real hadi muishie kumegwa na kuachwa...
 
ila mimi mwanume naye fanya naye kazi au yupo mtaa mmoja na mimi siwezi tembea naye hatas iku moja ,, na hijawahi tokea
 
Hivi ni kweli kina dada mmeshindwa kabisa kupambanua kuwa huyo chalii ni fake na huyu yuko real hadi muishie kumegwa na kuachwa...
wanaume wengi wamejificha kwenye mwavuli pendwa wa wakina dada ambao ni harusi,, sasa binti anajiachia tu akijua hata ikiingia nitaolewa kumbe mwanume hana hata mpango wa ndoa na yeye
 
wanaume wengi wamejificha kwenye mwavuli pendwa wa wakina dada ambao ni harusi,, sasa binti anajiachia tu akijua hata ikiingia nitaolewa kumbe mwanume hana hata mpango wa ndoa na yeye
Mkuu wacha nikupe siri kidogo ya kugundua sisi watu...Ukiona mtu kila akija kwako anaongelea mambo makubwa tu na ya kujisifia tu masifa yanayoendana na kumwonyesha yuko fit financially na kila akija anakuja na gari tofauti hadi kwenye list ya hayo magari unataja hammer na the like...Kimbiaaaaa huyo si muoaje yaanai ni anataka akuchanganye uingie kingi amege asepe..Nikweli tumewagundua kina dada wengi mnapenda mwanume mwenye nazo sasa wanaume wanafanya action kama kwenye movie kuakisi maisha ya mtu mwenye pesa na nyie mnajichanganya...Ukija shtuka kumbe mi nauza magazeti lakini ndiyo hivyo shamega na sitaki tena..
 
Unajua sio kama wanawadharau, bali ni ile hali ya kukujua tabia zako vyema kwa vizuri kabsaa bila utata ndio inafanya tusiwe na nyinyi wa kazini au mitaani au mliotuzunguka karibu. pengine haziendani na matakwa yetu, hata kama ni wewe tumeishi mtaa mmoja na ulikwua unaona jinsi nilivyomjeuri kwa mama yangu na muda mwengine kuongea hata maneno ya kijeuri, akili yako inakuwa ishajenga mawazo ya kwamba huyu msichana hafai, lakini kuna mtu wa mbali kabsaa ananiona namfaa ni kwa vile hajui tabia zangu nyengine n.k., au wewe ulikuwa unaona jinsi nilivyokuwa nikigombana na dada zangu kisa usafi na kupika au kuchelewa kurudi n.k., kuna tabia tunajuana moja kwa moja zinaturudisha nyuma both side, kwa wanaume na wanawake.
Hii inaweza ikawa sababu lakini haina nguvu kwa kuwa wadada waliowengi kwa nyakat hzi za sayansi na teknolojia wanapenda sana maisha rahis rahis anataka kutoka na mtu mwenye pesa wakati unakuta jamaa hana kitu lakini anauwezo wa kumvumilia mpaka atakapopata

Lakini wao huwa hawalioni hilo anachoamini akiwa na mwanaume mwenye pesa hakuna linaloshindikana, ni sawa lakini siku ukiachwa na Mimba juu inakuwa tabu nyingine unaanza kukumbuka nyuma kumbe yule alikuwa akinipenda japo hakuwa na kitu

Kinachomata katika maisha ya kimausiano siku zote ni upendo na kukubaliana na hali ya mwenzako coz ndicho alichojaaliwa na mwenyez mungu kumdharau na kumuona boya ni kumkosea adabu huyu mwenye mapenzi ya dhati kwako take it on your head
 
Back
Top Bottom