Akina dada mpunguze kuomba omba


Hapa paliniacha hoi last week!

Mrembo nimekutana naye maeneo ya ofisi yake, basi tukabadilishana namba.

Siku ya pili yake nika call na kumpa salamu tu ya kawaida.

Baada ya siku mbili nikapita jirani na ofisi yake, kumbe aliniona kwa mbali. Kilichofuata ni 'ukirudi nipitishie chips na mishikaki miwili'! Nilichoka!

Kiukweli kaumbika! Lakini hii 'first impression' imefanya nifute hadi namba!
 


Kaka ndo posho zenyewe hizo za ofisini, utasubiri sanaa neema kutoka kwa bosi.
 

Je ungeombwa kodi ya nyumba miezi sita na simu ungetupa kabisa! Mi kuombwa sioni taabu maana kutoa si lazima. Kama vile ukimtaka si lazima akubali.
 

Wanatakiwa kujiongeza kidogo! Inaboa sana, wakati fulani wakati wa lunch unamuomba kampani anadakiza "unataka kunipa lunch!" Mfyuuu! Hadi appetite inaisha!
 
hajaeleza mazingira ya kuombwa je alimtongoza au. na kama alimtongoza ina maana anataka FREE P
cc lara 1

Sorry mkuu hii "FREE P" Maana yake nini Maana naona linatumika sana JF... Hapa nimeachwa....
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…