MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 19,395
- 40,222
Waefeso 6:4
"Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana".
Kabla ya yote niweke wazi kwamba ninaamini biblia ni kitabu kitakatifu chenye mafundisho yote muhimu kwa binadamu. Pia ni kitabu chenye kuburudisha na kusisimu sana. Kimsingi biblia ni kitabu chenye kila kitu na kamwe hutajutia kukisoma kila siku. Kwa wale wasio na imani kama yangu pia wako sahihi maana nao wana wanachoamini.
Tukirudi kwenye nia nzima ya uzi ni kwamba biblia kupitia Waefeso ina maonyo kwa kina baba dhidi ya watoto wao. Ukisoma imeandikwa straight kwamba kina baba tusiwachokoze watoto bali tuwalee katika maadili mema. Kwanini imeandikwa hivi? Jibu ni kwamba hata Mungu mwenyewe alishaona upuuzi wa wakina baba wengi kuendekeza ubabe usio na tija kwa watoto wao kiasi kwamba wakati mwingine inakuwa kama uchokozi. Hivyo kupitia neno lake akatoa mwongozo.
Nikiangalia makuzi ya wengi wetu nazidi kuamini hayo maneno ya Waefeso 6:4. Wengi wetu tumekuzwa katika namna ambayo baba huwa ni kama adui yaani HAZOELEKI. Madhara yake ni kwamba huku ukubwani automatically baba anakuwa kama ametengwa. Watoto wengi wakishakuwa watu wazima huelekeza mapenzi kwa mama huku baba akipambana kivyake. Hali huwa mbaya kwa familia za vipato vya chini kwasababu watoto humjali zaidi mama kwa kumtumia pesa mara kwa mara. Baba hufanywa kama ziada tu. Kimsingi uzee wa wa kina baba wengi huwa na changamoto sana.
Ninawasihi sana kina baba wenzangu tusibaki kwenye yale maandiko ya kumbana mtoto aheshimu huku tukikazia na ule mstari usemao USIMNYIME MTOTO MAPIGO. Tukumbuke pia hatutakiwi KUWACHOKOZA WATOTO. Mtoto kukuogopa sana utajutia sana uzeeni. Utaanza kuwalaumu watoto kumjali mama yao zaidi wakati wewe ndo ulijichagulia mwenyewe mwisho wako.
Nawapongeza sana single mothers kwenye malezi ya watoto wao hasa wa kiume. Hawa single mama huwa wanacheza vizuri nafasi zao kwenye kuwakuza watoto wa kiume. Wengi wa watoto wa single mama huja kuwa masupastaa wakubwa na mzazi kuishia kula bata.