Akili ya mwanadamu inakaa wapi?

maamuzi sahihi

JF-Expert Member
Jun 4, 2014
288
165
Salamu wakuu nimekua nikijiuliza swali hili kwa mda sasa bila kupata jibu sahihi,ila kwasababu humu kuna watu wenye uelewa mkubwa wa mambo zaidi yangu naomba mnisaidie akili ya mwanadamu inakaa wapi?
 
Japo sina uelewa mkubwa sana wa haya mambo

Ila nachojua akili ya mwanadamu inakaa kwny ubongo ambao imegawanyika katika sehemu tatu kuu kwa kazi maalum
 
NINACHOFAHAMU MIMI AKILI NI NENO LAKUFIKILIKA LINALOELEZEA AU KUONESHA NAMNA MTU AU MNYAMA ANAVYOWEZA KUPAMBANA NA MAZINGIRA YAKE. KINACHOHIFADHIWA KWENYE UBONGO NI KUMBUKUMBU TUNAZOZIPATA KWA NJIA MBALIMBALI KAMA KUONA,KUSOMA, KUHISI N.K AKILI NI MATOKEO KUTUMIA KUMBUKUMBU ZILIZOHIFADHIWA KATIKA KUPAMBANA NA MAZINGIRA YETU. KWAHIYO HAKUNA KITU HARISI KINACHOITWA AKILI NDANI YA MWANADAMU AU MNYAMA NA MIFANO YA MANENO MENGINE KAMA AKILI NI ROHO, UPENDO, CHUKI N.K
 
Asante mkuu kwa maelezo yako jinsi unavyojua,ila mimi nahisi kuna mahali akili inakaa haiwezekan isiwe na sehemu sahihi ya kukaa maana akili ni muhimu sana,
 
Akili ni kama hewa tu inayopita kutoka huku kwenda kule au upepo,haiwezi kuelezeka kwa maana ya kitu kitu fulani.akili huwezi kuigusa wala kuiona ni kitu huwezi kukielezea sana.ila yamkini akili yaweza kujumlisha na nafsi ambayo hata hyo huwezi kuigusa kama kitu halisi au kuiona.wab'eeja sana nkooyi
 
Asante Mkuu maelezo yako yanaendana na ukweli lkn akili kuna sehemu inakaa embu endelea kufikiri huenda ukapata majibu.
 
NINACHOFAHAMU MIMI AKILI NI NENO LAKUFIKILIKA LINALOELEZEA AU KUONESHA NAMNA MTU AU MNYAMA ANAVYOWEZA KUPAMBANA NA MAZINGIRA YAKE. KINACHOHIFADHIWA KWENYE UBONGO NI KUMBUKUMBU TUNAZOZIPATA KWA NJIA MBALIMBALI KAMA KUONA,KUSOMA, KUHISI N.K AKILI NI MATOKEO KUTUMIA KUMBUKUMBU ZILIZOHIFADHIWA KATIKA KUPAMBANA NA MAZINGIRA YETU. KWAHIYO HAKUNA KITU HARISI KINACHOITWA AKILI NDANI YA MWANADAMU AU MNYAMA NA MIFANO YA MANENO MENGINE KAMA AKILI NI ROHO, UPENDO, CHUKI N.K
Kama ndivyo unasemaje kugusu IQ?
 
Akili sio kitu ni matokeo ya ubongo kufanya kazi ndio maana tuna namna tofauti ya "akili' kwasababu tuna namna tofauti ya ubongo wa kila mmoja wetu kufikiri.....

Huwezi kutafuta mahali ambapo utapata makazi ya matokeo yoyote yale.....

Mfano mwendo wa gari ni matokeo ya injini kufanya kazi,je unaweza kuuliza mahali ambapo mwendo unakaa ndani ya gari?

Mfano mwingine ni moshi wa gari,moshi ni matokeo ya mafuta kuchomwa,lakini unaona moshi unatoka kwenye gari,je unaweza kuuliza mahali ambapo moshi unakaa kwenye gari?

Nadhani hilo haliwezekani kabisa,akili kama ilivyo mwendo au moshi wa kwenye gari au kuni sio vitu ili vihitaji mahali pa kuwepo bali ni matokeo ya jambo fulani.....

Akili bni matokeo ya ubongo kufanya kazi hivyo huwezi kuuliza mahali inaokuwepo......
 
Shukrani mkuu kwa mawazo yako
 
Back
Top Bottom