Akili ya msomi wa kitanzania,je tutafika?

wikiliks

Member
Joined
Dec 15, 2012
Posts
84
Reaction score
27
MIMI NIMEMALIZA SHAHADA YA SANAA YA ELIMU `` NATAKA NIPATE KAZI ANGALAU IWE NA MSHAHARA WA KUANZIA SHILINGI 500,000 KWA MWEZI,baada ya miezi mitatu /probation ikiisha nitaomba mkopo wa milion 10 ili niweze kununua gari ya kwendea kazini na kula bata ya milioni 7,na inayobaki nipange chumba full furniture, nitakuwa nakatwa sh. 280,000 kama sehemu ya kulipa deni hivyo kufanya kipato changu kibakie 230,000/- kwa mwezi, nawaza kwa sauti tu jamani``

naomba mnisaidie maswali haya
1.mafuta ya gari nitatoa wapi?
2. je katika muono wangu nimefikiri kwa kutumia degree hapa?
3.mnadhani kwa namna hii nitapata maendeleo?

HIVI NDIVYO WASOMI TANZANIA WALIVYOANDALIWA KISAIKOLOJIA,JE TUTAFIKA?
 
Tatizo vijana wanapo garuate wanakuwa na expectations kuubwa sana.
Hii yote ni kwasababu vyuo vyetu humwandaa mwanafunzi kufaulu mitihani tuu.
 
umenena sahihi, na sio tu expectations kubwa ila pia wanafikiri mambo hayo yanapatikana kirahisi mno.
wakishaingia mtaani wanaona kuwa mambo hayako namna ile walivyofikiri wanaishia kutaka uiba iba ili watimize malengo na kuishia kuwa na matatizo juu ya matatizo
 
Sishangai hata mimi nilikuwa na expectation kama hizo nashukuru Mungu nikafanikiwa, ila inahitaji uwe na bidii binafsi kumaintain status unayoitaka. Mafuta si tatizo bali kuwa na usafiri, unajua wabongo wengi wanakula sana na kunywa mapombe faida kuota vitambi na makalio wote wanawake na wanaume.

Ukiwa na gari utakuwa unasanya posta Mwenge kila jioni vichwa vitano buku2 per hd na asubuhi wanakuchangia mafuta mbona maisha mjini simpo jamani? Hamuoni magari yamejaa kwani wote wanapata mamilioni wale.

I bought my first car kwa boom la chuo walikuwa wananiona mchovu nakula mlo mmoja kwa siku, outing zangu kanisani, no saloon wala cha maurembo full bint Africa nilipobadilika wakanambia nimehongwa I was like YES mtabakia hivyo. Nina binamu yangu nilimpa hiyo trick ya kuishi yeye akiwa mwaka wa pili akafungua stationary sasa anamaliza ana usafiri na kiwanja Pugu and he is just 22 ananishangazaga mpaka niliyempa ushauri
 
Nilipomaliza kazi nikasota mwaka mzima nilipopata niliambiwa nitalipwa laki 3 nikachukua diary nikaujumlisha kwa mwaka na kupanga matumizi, gari sikuuza na wala kufanyia biashara nililipaki home kwa braza nikapanga chumba kimoja mbali na home maana sipendi kuzinguana. Nilikunywa chai na mikate tena ilikuwa mitamu kweli ingawa leo haipandi, mboga yangu kuu ilikuwa mchicha wa kuchemsha na kitunguu (very delicious). Hapa saloon ilikuwa lazima maana sikutaka kujichoka na umri ndo ulikuwa hivyo tena.

Simu yangu ilikuwa naweka buku2 zikiishia kabla ya mwezi siongezi, Mungu akasaidia mwaka ukaisha nikaicheki account yangu ambayo nilijipangia kuwa naweka laki2 na moja ndo ya matumizi, nikaona naweza tumia gari mara mojamoja nikaipa bajeti ya elfu50 yakiisha napaki service iko kwenye ile laki ndipo nikaanza biashara ya kununua nguo Kariakoo nawauzia mtaani na ofisini nikaanza evening MBA wateja wakaongezeka buti ya gari ilijaa nguo mpaka inadidimia

Kamtaji kaliongezeka ndani ya mwezi nikanunua MAXCOM ya kuuza LUKU nikawa nawauzia wanafunzi wa chuo nikachukua tenda maofisi makubwa mjini. Nikapata scholarship ya mwaka mmoja nje ya nchi nikiwa nafanya dissertation yangu nikamuachia mtu akasepa khaaa. Sina hamu na biashara ya kuajiri mtu tena alikuwa swahiba na mimi kwasasa nasafiri sana

Ninachotaka kukwambia inawezekana ni mipango yako tu maana nimefanyia vitu vingi vya maana havina haja kuvitaja hapa
 
Tatizo vijana wanapo garuate wanakuwa na expectations kuubwa sana.
Hii yote ni kwasababu vyuo vyetu humwandaa mwanafunzi kufaulu mitihani tuu.

Naungana na wewe 100%, pia tatizo sio vyuo tu, bali hata mfumo mzima wa Elimu unawaandaa wasosomi wawe hivyo.

Ila, kadiri ya uwezo wangu mdogo, mtu akihitimu shahada anapaswa kusoma na kuchambua mawazo sahihi na kuyafanyia kazi. Hivyo basi, mtitimu anaweza kusoma vitabu juu ya uwekezaji, mitaji, masoko, n.k na kuvifanyia kazi, kisha kufanikiwa.

Nimesikia kuna mpango wa kuweka kozi ya Ujasiriamali kwa wanafunzi wa Shahada ya kwanza kwa vyuo vyote nchini, inaweza ikawa vizuri kufanya hivyo.

Natofautiana kidogo na huo mpango, kwa kuwa, kadiri ya uelewa wangu mdogo, wanachuo wakomalia madesa tu, kunukuu kutoka kwenye tovuti (copy & paste) ili wafaulu; ili kukwepa suplementary au karai (C). Dhana nzima ya Ujasiriamali inaweza isifanye kazi, kwa kuwa Wanachuo, na mfumo wa Elimu, huangalia mtu amesoma nini na kupata nini.

PENDEKEZO LANGU. Mfumo wa Elimu unaweza kuachwa kama ulivyo, Wanachuo wakapewa nasaha (guidance), kujitambua, kukawa na vitabu vingi na bora juu ya maswala ya Ujasriamali, kisha kila Mwanachuo akawa huru kusoma na kutekeleza au akaacha kabisa.

Wasiwasi wangu pia ni kwamba wanaweza kuwaajiri Waalimu (lecturers) wasio na uwezo wa kufundisha ujasiriamali kwa gharama kubwa, vitabu visipatikane, au vikapatikana vitabu visivyo na ubora, pia, kwa gharama kubwa. Je huoni hasara itakuwa ma mbili?

Kumbuka kile anachofanya mtu kwa hiari yake akiwa amejiwekea viwango vya ubora na ukaguzi, hufanya kwa unadhifu mkubwa sana ililinganishwa na alifefanyk i hususani la kufau.
 
MIMI NIMEMALIZA SHAHADA YA SANAA YA ELIMU `` NATAKA NIPATE KAZI ANGALAU IWE NA MSHAHARA WA KUANZIA SHILINGI 500,000 KWA MWEZI,baada ya miezi mitatu /probation ikiisha nitaomba mkopo wa milion 10 ili niweze kununua gari ya kwendea kazini na kula bata ya milioni 7,na inayobaki nipange chumba full furniture, nitakuwa nakatwa sh. 280,000 kama sehemu ya kulipa deni hivyo kufanya kipato changu kibakie 230,000/- kwa mwezi, nawaza kwa sauti tu jamani``

naomba mnisaidie maswali haya
1.mafuta ya gari nitatoa wapi?
2. je katika muono wangu nimefikiri kwa kutumia degree hapa?
3.mnadhani kwa namna hii nitapata maendeleo?

HIVI NDIVYO WASOMI TANZANIA WALIVYOANDALIWA KISAIKOLOJIA,JE TUTAFIKA?
si kosa la vijana ni kosa la mfumo, duniani nchi zilizo serious watu karibu wote huishi kwa mikopo ya muda mrefu sana ili wasiwaze kutafuta rushwa
 
Mawazo potofu sana, utakula bata hiyo kwa muda gani na hiyo million 10 kabla hujafukuzwa kazi? Labda ubahatike kuajiriwa na serikali ambapo ufatilianaji na kuwajibishana ni kidogo sana unapomaliza vidato kazaa jiangalie kwanza namna ya kusimama mwenyewe kwa miguu yako, bola na huyu binti alienunua gari kwa boom la chuoni. Lkn cha msingi jiangalie kujiajiri mwenyewe na kutazama maisha yako mbele ya miaka 40
 
He! Shahada ya sanaa ya elimu!!!! Sijakupata kabisa. Unatafuta kazi gani?? Kwa fani hiyo sijui utafanya kazi gani labda ualimu wa chuo ila soma kwanza masters ndipo utakuwa competitive. Ila upate upper second au first class.Pia fanya utafiti ujue masomo yanayotakiwa kwenye vyuo ndio usomee. Mbona mshahara wa walimu vyuo sio mbaya!! Yote uliyoandika uteyafanya ila ushauri wa bure MAMBO MAZURI HAYATAKI HARAKA. Uwe na subira. Rome haikujengwa kwa siku moja.
MIMI NIMEMALIZA SHAHADA YA SANAA YA ELIMU `` NATAKA NIPATE KAZI ANGALAU IWE NA MSHAHARA WA KUANZIA SHILINGI 500,000 KWA MWEZI,baada ya miezi mitatu /probation ikiisha nitaomba mkopo wa milion 10 ili niweze kununua gari ya kwendea kazini na kula bata ya milioni 7,na inayobaki nipange chumba full furniture, nitakuwa nakatwa sh. 280,000 kama sehemu ya kulipa deni hivyo kufanya kipato changu kibakie 230,000/- kwa mwezi, nawaza kwa sauti tu jamani``

naomba mnisaidie maswali haya
1.mafuta ya gari nitatoa wapi?
2. je katika muono wangu nimefikiri kwa kutumia degree hapa?
3.mnadhani kwa namna hii nitapata maendeleo?

HIVI NDIVYO WASOMI TANZANIA WALIVYOANDALIWA KISAIKOLOJIA,JE TUTAFIKA?
 
Sishangai hata mimi nilikuwa na expectation kama hizo nashukuru Mungu nikafanikiwa, ila inahitaji uwe na bidii binafsi kumaintain status unayoitaka. Mafuta si tatizo bali kuwa na usafiri, unajua wabongo wengi wanakula sana na kunywa mapombe faida kuota vitambi na makalio wote wanawake na wanaume.

Ukiwa na gari utakuwa unasanya posta Mwenge kila jioni vichwa vitano buku2 per hd na asubuhi wanakuchangia mafuta mbona maisha mjini simpo jamani? Hamuoni magari yamejaa kwani wote wanapata mamilioni wale.

I bought my first car kwa boom la chuo walikuwa wananiona mchovu nakula mlo mmoja kwa siku, outing zangu kanisani, no saloon wala cha maurembo full bint Africa nilipobadilika wakanambia nimehongwa I was like YES mtabakia hivyo. Nina binamu yangu nilimpa hiyo trick ya kuishi yeye akiwa mwaka wa pili akafungua stationary sasa anamaliza ana usafiri na kiwanja Pugu and he is just 22 ananishangazaga mpaka niliyempa ushauri

kawadanganye watoto..
 
boom hilo ulikua unapata sh ngapi mpaka ununue gari???????????
 
kawadanganye watoto..

teh teh!umemstukia eeh???eti hela ya boom anunue gari!wkt hilo boom lenyewe lilikua buku5 pa day enzi hizo na ilikua haitoshi kwa mahitaji ya kawaida!

Semister ina siku 120*5000=600,000!so kwa semister boom lilikua ni laki6,degree inasomwa kwa semista 6,so 600,000*6 =3600,000
jumla kwa miaka mitatu ya masomo boom lilikua ni sh 3.6m!so gari hiyo ni aina gani aliyoweza kuinunua kwa 3m???na je alikua hali ???manake pesa hiyo hiyo inajumuisha na meal and acomodation!huyu bibie anatudanganya!

Otherwise aseme kua alikua anapata sapot pembeni then pesa yake ya boom ilikua haitumiki bali anaiweka tu mpaka ilipotimia ya kununua starlet!
 
Fikra mbadala za mtoto wa kitaa anayejua maisha

capital tzs 10,000,000

bodaboda tatu(3)@ 1,800,000 =5,400,000.
Mpesa tigopesa airtelmoney =2,000,000.
Salon ya kiume ya kitaa, = 1,000,000.
Chumba kimoja 50 000 kodi miezi 6 = 300 000
mazaga ya geto. =1 000 0000
pamba za kuendea job na maskan = 200 000

jumla ni laki 9,900,000

laki iliyobaki naweka heshima baaaa.......
 
Mi naona tusikate tamaa kila jambo lawezekana ukipanga. Wanasema kuwa na Vision tengeneza strategy ukiwa na missions zako utaiona future yako
 
kuchukua mkopo na kununua gari ni sawa na kujitia jipu uchungu
 
teh teh!umemstukia eeh???eti hela ya boom anunue gari!wkt hilo boom lenyewe lilikua buku5 pa day enzi hizo na ilikua haitoshi kwa mahitaji ya kawaida!

Semister ina siku 120*5000=600,000!so kwa semister boom lilikua ni laki6,degree inasomwa kwa semista 6,so 600,000*6 =3600,000
jumla kwa miaka mitatu ya masomo boom lilikua ni sh 3.6m!so gari hiyo ni aina gani aliyoweza kuinunua kwa 3m???na je alikua hali ???manake pesa hiyo hiyo inajumuisha na meal and acomodation!huyu bibie anatudanganya!

Otherwise aseme kua alikua anapata sapot pembeni then pesa yake ya boom ilikua haitumiki bali anaiweka tu mpaka ilipotimia ya kununua starlet!

Muulize alinunua hilo gari bei gani.
Enzi zetu kulikuwa na michongo serikalini. Baadhi ya magari ya serikali yalikuwa yananyofolewa kitu kidogo tu kuyafanya yasitembee halafu yanawekwa benchi muda mrefu kana kwamba ni gharama kubwa kuyakarabati. Baada ya hapo yanapelekwa kwenye minada bubu ya magari mabovu ya serikali, hapo unaweza ukapata gari kwa laki tatu. Nakumbuka tulinunua land rover 110 kwa laki tano, na kuitengeneza kurudi barabarani gharama haikufika laki moja.Si sahihi lakini michezo mingi mingine pia inafanyika.
 
Sishangai hata mimi nilikuwa na expectation kama hizo nashukuru Mungu nikafanikiwa, ila inahitaji uwe na bidii binafsi kumaintain status unayoitaka. Mafuta si tatizo bali kuwa na usafiri, unajua wabongo wengi wanakula sana na kunywa mapombe faida kuota vitambi na makalio wote wanawake na wanaume.

Ukiwa na gari utakuwa unasanya posta Mwenge kila jioni vichwa vitano buku2 per hd na asubuhi wanakuchangia mafuta mbona maisha mjini simpo jamani? Hamuoni magari yamejaa kwani wote wanapata mamilioni wale.

I bought my first car kwa boom la chuo walikuwa wananiona mchovu nakula mlo mmoja kwa siku, outing zangu kanisani, no saloon wala cha maurembo full bint Africa nilipobadilika wakanambia nimehongwa I was like YES mtabakia hivyo. Nina binamu yangu nilimpa hiyo trick ya kuishi yeye akiwa mwaka wa pili akafungua stationary sasa anamaliza ana usafiri na kiwanja Pugu and he is just 22 ananishangazaga mpaka niliyempa ushauri

Hii itakua inapatikana kwako tu, katika hali ya kwaida siyo rahisi hiyo pesa itumike kwa mahitaji ya kila siku chuoni halafu ubakishe hela ya kununua gari labda kama kulikua na vyanzo vingine.
 
Back
Top Bottom