Nilipomaliza kazi nikasota mwaka mzima nilipopata niliambiwa nitalipwa laki 3 nikachukua diary nikaujumlisha kwa mwaka na kupanga matumizi, gari sikuuza na wala kufanyia biashara nililipaki home kwa braza nikapanga chumba kimoja mbali na home maana sipendi kuzinguana. Nilikunywa chai na mikate tena ilikuwa mitamu kweli ingawa leo haipandi, mboga yangu kuu ilikuwa mchicha wa kuchemsha na kitunguu (very delicious). Hapa saloon ilikuwa lazima maana sikutaka kujichoka na umri ndo ulikuwa hivyo tena.
Simu yangu ilikuwa naweka buku2 zikiishia kabla ya mwezi siongezi, Mungu akasaidia mwaka ukaisha nikaicheki account yangu ambayo nilijipangia kuwa naweka laki2 na moja ndo ya matumizi, nikaona naweza tumia gari mara mojamoja nikaipa bajeti ya elfu50 yakiisha napaki service iko kwenye ile laki ndipo nikaanza biashara ya kununua nguo Kariakoo nawauzia mtaani na ofisini nikaanza evening MBA wateja wakaongezeka buti ya gari ilijaa nguo mpaka inadidimia
Kamtaji kaliongezeka ndani ya mwezi nikanunua MAXCOM ya kuuza LUKU nikawa nawauzia wanafunzi wa chuo nikachukua tenda maofisi makubwa mjini. Nikapata scholarship ya mwaka mmoja nje ya nchi nikiwa nafanya dissertation yangu nikamuachia mtu akasepa khaaa. Sina hamu na biashara ya kuajiri mtu tena alikuwa swahiba na mimi kwasasa nasafiri sana
Ninachotaka kukwambia inawezekana ni mipango yako tu maana nimefanyia vitu vingi vya maana havina haja kuvitaja hapa