Akili ya Ally Mayai na Hekima za Mwl.Nyerere

amita bacha

Senior Member
Mar 10, 2017
180
411
Siku anazaliwa Mzanaki, Julius Nyerere, hakuna mtu yeyote duniani aliyetambua kuwa amezaliwa kiumbe wa aina gani! Si wazazi wake, majirani hata gavana wa Kiingereza wa wakati huo.. aliyedhani kuwa KICHWA kilikuwa kimeletwa duniani! Chambilecho kama utawala wa Kiingereza ungelifahamu juu ya ujio huo, basi labda wangegeuka na kuwa Herode...wakimtafuta Nyerere wamzime hata kabla ya arobaini yake! Lakini hawakufunuliwa mioyoni mwao....na kibaya zaidi kwa nyakati hizo hapakuwepo na MAMAJUSI wa kueneza ubuyu huo juu ya kuzaliwa kwa MWALIMU J. NYERERE.
Wao walikuwa bize kuendeleza UNYONYAJI katika koloni lao la Tanganyika. Hiyo ilikuwa ni miaka minne tangu vita ya kwanza kumalizika huku Mjerumani akiwa ameshindwa katika vita hiyo..!

Yawezekana pia wakati huu ambao Jamal Malinzi, rais wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania, TFF, akiwa anahitimisha uongozi wake wa miaka minne...yupo bize kabisa kuhangaika na wapiga kura ili wamrejeshe tena madarakani!
Haamini kama kuna mtu wa kumng'oa kwenye kiti hicho! Anaamini kabisa kuwa yeye ni rais wa miaka minne ijayo....kama walivyoamini Waingereza, wakidhani ya kuwa ingechukua muda mrefu kwa watanganyika kuja kugundua kile kilichoandikwa katika makablasha yaliyosainiwa kati yao na iliyokuwa LEAGUE OF NATION, sasa UN (Umoja wa Mataifa), katika ardhi ya Ufaransa.

Akili ya Ally Mayai Tembele, mgombea urais wa TFF mwaka huu...waweza ifananisha na hekima za Nyerere!
Wakati MWL Nyerere anaacha kazi ya ualimu pale Pugu Sekondari, na kuamua kujikita kwenye siasa za ukombozi wa nchi hii....Ally Mayai miaka kadhaa mbele anatangaza kuachana na soka!
Dunia ya wapenda kabumbu inashtuka mno, viongozi wa Yanga wanahaha kuyarudisha nyuma mawazo yake. Lakini tayari Ally Mayai hakuwa na muda wa kusubiri kutongozwa tena kwa maneno matamu ya viongozi wake....alitundika daruga na kuachana kabisa na Yanga. Akastaafu soka!
Mashabiki wa Yanga wakabaki na bumbuazi, wasijue ni vipi watampata mbadala wake. Walimpenda mno, kwani utulivu wake uwanjani uliwasuuza nyoyo zao...pale timu yao ilipokuwa imezidiwa mbinu na wapinzani wao.. Tembele pekee ndiye angeweza kuwarudisha mchezoni wachezaji wenzake, timu ikatulia na kurudi mchezoni na matokeo yakapatikana! Yawezekana katika nyakati kama hizi, Ally Mayai angecheza na Niyonzima, basi mashabiki wa Yanga wasingekuwa wakilia kuondoka kwa mnyarwanda huyo....ungeweza kuwasikia tu wakitamba mitaani...."Tunae Ali Mayai...nini Niyonzima..! Ndivyo ingekuwa hivyo!

Ali Mayai alitokomea kivyake, lakini baadaye akaibuka na kuweka wazi kuwa anaingia darasani, kwenda kuendelea na Chuo Kikuu...! Watu wakashangaa! Ali Mayai akazama kitabuni, akabukua na baadaye akahitimu! Akaibuka tena...lakini mara hii akiwa mtu wa tofauti kabisa! Akili yake ikiwa na elimu ya chuo kikuu pamoja na ile ya soka. Akawa ameiva bara'bara!
Akajikita kwenye uchambuzi wa mpira wa miguu huku akiendelea na maisha yake ya kawaida kama mtumishi wa umma. PATAMU HAPO!
Wapenda soka waliokuwa wameumisi utulivu wake dimbani, wakajikuta wakitabasamu tena. Dhamira yake ya kusema ukweli ilimtofautisha sana na wachambuzi wengine.. ambao makala zao zilimezwa na USIMBA na UYANGA! Ali ni mkweli na asiyeyumbishwa katika kuisimamia kweli yake. Ndivyo hivyo hivyo alivyokuwa Nyerere.

Labda wakati huu ambao Malinzi anadhani kuwa yeye ni kama Leodigar Tenga, basi anakosea...na mawazo yake yanampeleka CHAKA!

Soka la nchi hii limedidimia na liko hatarini kutumbukia korongoni kabisa. Nchi hii haihitaji tena kiongozi aina ya Malinzi...bali kiongozi aina ya Ali Mayai!
Malinzi alichemsha Yanga akiwa kama Katibu mkuu...lakini miaka minne nyuma wapiga kura wakamwamini, akaukwaa urais wa TFF. Ila sasa hapo napo amechemsha kwa muhura wake wa kwanza tu! Anahitaji kujisahihisha akiwa nje ya boksi!! Kuna mazuri kayafanya...Ila yapo mazuri zaidi ambayo wengine wanapaswa kuyafanya pia!

Yawezekana wakati ambao Nyerere aliacha kazi, kuna waliomshangaa...vile vile wakati ambao Ali Mayai anatundika daruga katika umri mdogo, kuna watu walimbeza...wakiongizwa na wachambuzi! Lakini je kuna mtu alijua kuwa yule Nyerere mwalimu, angeweza kuja kuwa kiongozi mkubwa katika ulimwengu huu?
Wakati wa vijana wenye dira kuongoza mpira wa nchi hii umefika!

Akili ya Ali Mayai imebeba hekima za mwalimu Nyerere!!

Makala haya yameandikwa na;
Baraka Mazigo.
(0679706568).
 
Huyu malinzi kakosa mipango hana jipya alilolifanya tff zaidi ya usjmba na uyanga ulimjaa mm naombea sana apigwe chini
 
Nakubali tunahitaji mabadiliko tff. Wahaya chonde chonde hii nchi yetu sote. Acheni ukabila vote for ma egg
 
Back
Top Bottom