Itafika point na muda katika maisha yake ambapo mwanaume ataamua kureevaluate maisha yake kama mwanamke alivyofanya kipindi cha kuanzisha feminism mpaka kufikia women empowerment na mwishowe supremacy over men rather than equality. Alichokosea mwanamke katika kureevaluate maisha yake aliingiza competition na kumuweka mwanaume kama adui wake na kipimo chakujipima kama kafanikiwa au laah, ila bado hakutafuta njia ya kumtoa mwanaume kama mtegemezi wake maana yote aliyoyafanya baada ya kuyapitia (kureevaluate) maisha yake alitegemea support ya mwanaume na mwanaume kubaki constant bila kubadilika hivyo hakufikiria siku mwanaume akiamua kubadilika. Naalijiwazia yeye kama yeye na maisha yake ila si yafamilia au jamii yake.
Tunapoelekea ni kuwa imefika muda na point ambayo mwanaume naye kwapolepole anaanza kureevaluate maisha yake. Wameanza kugusia swala la ndoa, wengine wameshaanza kugusia swala la majukumu katika jamii ilihali ajira zitolewazo zinazingatia usawa wa kijinsia wakati majukumu ni tofauti, nao wameanza kuzungumzia furaha yao na kuhusu swala la kushare mali au pesa zake na mwanamke na swala la kudelegate majukumu yako kwa mdada wakazi lakini bado ukitaka benefit ya mke ilihali mchango wako katika hiyo ajira hauonekani katika familia n.k. Muda ukifika wa mwanaume kuanza kuimplement mabadiliko yake kwauzito kama mwanamke alivyofanya basi nakwambia dunia itabadilika sana tena sana. Kwasababu last standing point ya nchi au taifa ni wanaume hata vitani na nchi ikiwa gizani. Wakiondoshwa hao, taifa linakufa na nchi inapotea kwa ujumla.
Hili swali jamaa alilouliza linamantiki sana tena sana ila kipindi chanyuma mwanaume hakujali kuhusu hiki kitu kabisa ila wanawake wengi huuliza. Sasa mwanaume naye ameamua kuuliza na wanawake wengi hawana majibu kwasababu katika mzunguko wao wa maisha na harakati zao mwanaume hawakumtoa na humtegemea sana tena sana ila mategemeo yao ya mwanaume kubadilika constant yameanza kubadilika.
Bare in mind, katika mzunguko wa maisha wa mwanaume, yeye jamii imeshamjenga na kuafikiana tangu kuzaliwa kwake kuwa mwanaume kumtegemea mwanamke ni laana na kujidharaulisha vibaya mno. If changes occur to 100% dunia itabadilika vibaya sana. Otherwise Mungu mwema.