Akija Rais atakaye deal na bodaboda nitamshukuru

Akija Rais atakaye deal na bodaboda nitamshukuru

amarina

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2025
Posts
230
Reaction score
403
Hizi taka taka barabarani zinakera mno. Yaan nakumbuka enzinza tex maisha yalikuwa mazuri. Hawa waharibifu hata sijui nani amewaleta. Ni kero kero barabarani, kwenye ndoa, usalama wa mahouse girl, watoto wetu wa kike yaani ni tafrani.

Siku akaja kiongozi mkuu wa nchi akatoa oder ama wasiondolewe Bali wawe watu wenye heshima, waheshimu Sheria za usalama barabarani, Sheria Kali za kuingilia ndoa za watu, na dhid ya watu wengine nitamshukuru sana

Ninewavhoka na tusichoshane mamamae
 
Sasa fikiria hizo akili zote zihamie kwenye ukabaji
Kama nimemuelewa mtoa mada, hajasema kufungia kazi zao bali kudili na nidhamu na tabia zao wengi tabia zao mbaya,, na kinacho wapa jeuri ni ule wanaita umoja wao wa kishamba kwamba ukizinguana na mmoja wanakuja mia,,
 
Hakuna Rais mjinga wa hivyo,bodaboda ndio wanatumika na serikali kukwepa accountability kutengeneza ajira rasmi kwa vijana,so wakisema vijana wajiajiri wana refer bodaboda,.

Kama taifa Tumefikia uamuzi kua njia ya kusovu tatizo la ajira ni bodaboda,.
 
Unajua bodaboda zikiwa 2milions zimeiokoa kwa kiasi gani serikali na upungufu wa ajira na je zikitolewa nini itakua mbadala wa ajira na usafiri wa haraka na nafuu adi vichochoroni?
 
Kwenye ndoa yako bodaboda wanahusika vipi? Hizi lawama nyingine zimevuka mipaka
Hujamuelewa tu
1 bodaboda ni magaidi yaliyoidhinishwa na serikali
2 bodaboda wamekuwa watuhumiwa wa kutembea na wake za watu kuwatia mimba wanafunzi na wasaidizi wa ndani, na kesi nyingi za bodaboda kuuwawa chanzo kikubwa imekuwa ni wake za watu inatakiwa bodaboda wa Tanzania wakajifunze Rwanda🇷🇼 aisee wale bodaboda wa kule wamepiga hatua kubwa sana
 
Wadau mnamshambulia na kushupaza mishipa ya shingo, hebu msome mmalize na muelewe. Kasema angalau awabadilishe na kuwa wafuataji sheria na wenye maadili.

Sawa boda ni ajira na inaokoa vijana wengi mjini, kwa mantiki hii waachwe kupunguza msongamano wa wasiyo na ajira.

Ila hii isiwe sababu ya kuleta mazoea na wake za watu hadi kuwagonga, kutia mimba wanafunzi au kuwafanya wasifike shuleni kwa wakati.

Pia isiwe sababu ya kutotii sheria unakuta taa nyekundu simama na tii, unataka kuingia barabara kuu, subiri aliyepo huko akuruhusu hii ndiyo sheria, ya priority barabarani hutaka hivyo, si kuchomekea na kusababisha ajali zisizo na msingi halafu hodari wa kukimbia kuachia watu misala. Bado kosa likiwa la mmoja wao wanachoma hadi magari ya watu moto.

Tunawaheshimu ni fighter kama wengine mnaleta msosi mezani kwa wake na watoto wenu, mabachela mnakula hadi kuvaa hapohapo. Ila mkumbuke hizi barabara hamjaumbiwa nyinyi mpaka mfanye mnavyotaka.

Wacheni michezo ya kushindana na magari wakati wewe body ni mwili wako, mnaongeza idadi ya wajane, mayatima na wazazi wenye misongo ya mawazo.

Tiini sheria, ukipenda sketi ya shule mpe mkeo avae kiila ukirudi ndani, zipu yako ichunge wake za watu kisa kupanda bure.​
 
Unajua bodaboda zikiwa 2milions zimeiokoa kwa kiasi gani serikali na upungufu wa ajira na je zikitolewa nini itakua mbadala wa ajira na usafiri wa haraka na nafuu adi vichochoroni?
Si kwamba wapigwe marufuku hapana wathibitiwe kwa sheria kali tu mbona Rwanda🇷🇼 bodaboda wako vizuri kabisa njoo hapa sasa bodaboda imekuwa chaka la walevi vibaka majambazi wauza madawa ya kulevya wasafirisha magendo yasiyofuata sheria za usalama barabarani yaani ni kama watu waliokata tamaa na maisha wanejitoa muhanga kwa lolote
 
Ukituliza akili utaona bado wana faida nyingi sana kuliko hasara,

Kwasisi wafanya biashara delivery zetu zinaharakishwa na hawa jamaa,
Uwepo wa bodaboda umetoa ajira nyingi sana kaa vijana,
Soko la spare parties, mafundi wote wana maisha mazuri sababu ya bodaboda
 
Wadau mnamshambulia na kushupaza mishipa ya shingo, hebu msome mmalize na muelewe. Kasema angalau awabadilishe na kuwa wafuataji sheria na wenye maadili.

Sawa boda ni ajira na inaokoa vijana wengi mjini, kwa mantiki hii waachwe kupunguza msongamano wa wasiyo na ajira.

Ila hii isiwe sababu ya kuleta mazoea na wake za watu hadi kuwagonga, kutia mimba wanafunzi au kuwafanya wasifike shuleni kwa wakati.

Pia isiwe sababu ya kutotii sheria unakuta taa nyekundu simama na tii, unataka kuingia barabara kuu, subiri aliyepo huko akuruhusu hii ndiyo sheria, ya priority barabarani hutaka hivyo, si kuchomekea na kusababisha ajali zisizo na msingi halafu hodari wa kukimbia kuachia watu misala. Bado kosa likiwa la mmoja wao wanachoma hadi magari ya watu moto.

Tunawaheshimu ni fighter kama wengine mnaleta msosi mezani kwa wake na watoto wenu, mabachela mnakula hadi kuvaa hapohapo. Ila mkumbuke hizi barabara hamjaumbiwa nyinyi mpaka mfanye mnavyotaka.

Wacheni michezo ya kushindana na magari wakati wewe body ni mwili wako, mnaongeza idadi ya wajane, mayatima na wazazi wenye misongo ya mawazo.

Tiini sheria, ukipenda sketi ya shule mpe mkeo avae kiila ukirudi ndani, zipu yako ichunge wake za watu kisa kupanda bure.​
Wapo bodaboda wanaojitambua na wanajali kazi yao ila hawa wenye walioachia nywele kama makinda ya ndege hapana
 
Kuna uhusiano gani kua boda boda na kua mhuni ,mchafu, kua na tabia mbaya

Ni kwamba kuna athari ukianza kua boda boda unazipata hivi hili kundi shida ni nini?
Au bange na pombe ?
 
Kuna uhusiano gani kua boda boda na kua mhuni ,mchafu, kua na tabia mbaya

Ni kwamba kuna athari ukianza kua boda boda unazipata hivi hili kundi shida ni nini?
Au bange na pombe ?
Bangi na pombe ndiyo shida hii kazi imeshakuwa kichaka cha vibaka majambazi wauza madawa kusafirisha magendo
 
Back
Top Bottom