Aki afanya kufuru Nigeria | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aki afanya kufuru Nigeria

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Michael Amon, Jan 18, 2012.

 1. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #1
  Jan 18, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  HIVI karibuni kulikuwa na shangwe, hoihoi nderemo na vifijo pale muigizaji nyota wa filamu wa Nigeria, Chinedu Ikedieze, maarufu kwa jina la Aki (33), alipofunga pingu za maisha na mrembo Nneoma Hope Nwajah (20) katika kitongoji cha Mbano kilichopo katika Jimbo la Imo.


  Aki, mmoja wa mastaa `mbilikimo’ na `pacha wake katika filamu’, Osita Iheme (Ukwa) ni marafiki wakubwa ambao wamefanikiwa kuigiza filamu nyingi na kuliteka soko la tasnia hiyo katika mataifa mbalimbali ya Afrika na nje ya Afrika, Tanzania ikiwemo.

  Harusi hiyo iliyokuwa na vionjo vyote vya kimila ilifanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Theresa lililopo katika viwanja vya Shule ya Msingi ya Obolo katika kitongoji hicho cha Mbano.
  Haikuwa harusi ya ‘kitoto’ kwani Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan na mkewe walialikwa na kuhudhuria sherehe hiyo.

  Wageni wengine mashuhuri waliokuwa wamethibitisha ni magavana watatu kutoka majimbo ya Kusini Mashariki mwa nchi ya Nigeria. Hao si wengine bali Gavana wa Jimbo la Abia, T.A. Orji, Jimbo la Imo, Rochas Okorocha na wa Jimbo la Anambra, Peter Obi.

  Rafiki mkubwa wa karibu wa Aki kwa zaidi ya miaka kumi sasa, Osita Iheme (Ukwa), ndiye aliyekuwa mwambata (best man) wa bwana harusi. Chanzo cha uchumba wao Staa Aki na Nneoma wamekuwa wachumba kwa miaka mitatu sasa, katika kipindi ambacho wameoneshana mapenzi ya dhati baina yao.

  Hatimaye Aki amepata mwenza na kuweka mambo hadharani namna alivyoweza kukutana na mpenzi wake huyo na kujikuta akitumbukia katika dimbwi kubwa la mahaba mithili ya bahari na kuwa vigumu kwake kuweza kujinasua. Mwenyewe anasema mkewe huyo sasa ni sehemu ya maisha yake yote yaliyosalia hapa duniani.

  “Tumekuwa katika lindi la mahaba kwa miaka mitatu, nilikutana naye Lagos na katika hali isiyoelezeka ghafla tulijikuta tukizama katika ulimwengu wa mapenzi.Yeye sasa ni tumaini la maisha yangu yote, na hakuna zaidi ya kifo kitakachotutenganisha,” Aki aliapa.

  Anapoulizwa mkewe alivutiwa zaidi na nini kwake, Aki alikuwa na haya ya kusema “aliniambia ananipenda kwa vile mimi ni mtu mzima, ni mwelewa, mwenye mvuto, busara na upendo wa dhati.”

  Akijibu swali la ni watoto wangapi angependa kupata na mkewe huyo, Aki anasema “Si zaidi ya watoto watatu bila kujali jinsi yoyote watakayokuwa nayo.” Kuhusu tetesi kwamba alitumbukia kwenye penzi na mrembo huyo kutokana na haiba yake iliyojielekeza zaidi katika kumcha Mungu, Aki anasema hilo pia limechangia kuongeza nafasi ya pendo kwa mkewe.

  Muigizaji huyo ambaye amejinyakulia tuzo nyingi ikiwemo tuzo ya heshima ya Taifa la Nigeria ya MFR mwaka mmoja uliopita, anasema anajisikia mwenye faraja kwa vile tuzo hizo zinamuweka karibu na watu wengi wa kawaida.

  Mke wa Aki, Nneoma, akizungumzia uamuzi wake wa kufunga ndoa na Aki akiwa na umri huo wa miaka 20 huku akionekana kuwa mwanamke mrembo, anasema amechukua uamuzi huo kutokana na kuongozwa na matakwa ya Mungu.

  Machungu katika safari ya mapenzi

  Akiwa katika maumivu makali ya kumsaka mrembo wa kuishi naye kwa maisha yake yote yaliyosalia duniani, Aki alivumilia hali hiyo kwa miaka mingi. Kabla ya kupata mafanikio hayo, muigizaji huyo mwenye utajiri mkubwa wa fedha, akiwa na majumba na magari ya kifahari, alimchumbia ofisa wa benki, aitwaye Nkechi kutoka eneo la Delta, uchumba ambao ulikufa ghafla katika tukio ambalo halijatolewa maelezo yoyote ya maana hadi sasa.

  Haikuchukua muda mrefu baada ya hapo, milionea huyo alianzisha mahusiano mengine ya mapenzi ya nguvu na mwanamke mwingine. Uhusiano huo nao ulikatika ghafla. Sasa hatimaye Aki amekamilisha safari yake hiyo kwa kufunga pingu ya maisha na Nneoma.

  Sherehe hiyo ya harusi ya kimila iliyofanyika karibuni na kuwajumuisha ndugu, jamaa na marafiki ilishuhudiwa na mamia ya wananchi wa kitongoji hicho cha Mbano ambako Nneoma amezaliwa.

  Habari njema zinasema sherehe hiyo ya harusi itafuatiwa na pati babu kubwa iliyofanyika katika Jiji maarufu la Lagos, Desemba 10, mwaka huu.

  Historia ya maisha yake

  Aki, anasema kwa kila filamu yao hulipwa kati ya dola 8,000 na 30,000 (kati ya Sh milioni 15 na milioni 52), alizaliwa Desemba 12 mwaka 1977 katika kitongoji cha Bende katika Jimbo la Abia. Amejipatia umaarufu mkubwa kwa kuigiza filamu mbalimbali zijulikanazo duniani kwa jina la filamu za Aki na Ukwa.

  Mwaka 2007, Aki alipata mafanikio makubwa katika maisha yake pale alipotwaa taji la Muigizaji Bora wa Afrika, taji linalotolewa na Taasisi ya Filamu ya Afrika (AMA).

  Hadi mwaka 2002 ilipotokea bahati wakakutana katika mojawapo ya matamasha ya sanaa, si Aki wala Ukwa aliyekuwa anajua kwamba wanavyo vipaji na ubunifu ambao kama wataviunganisha kwa pamoja wataweza kuteka soko la filamu duniani.

  Umaarufu wao umewafanya waigizaji hao wafupi lakini wenye makeke mengi kupata mialiko mingi na yenye malipo makubwa kutoka nchi mbalimbali duniani.

  Aki ni msomi wa Shahada ya Mawasiliano kwa Umma aliyotunukiwa na Taasisi ya Uongozi na Teknolojia (IMT) ya Enugu wakati Ukwa hivi sasa ni mwanafunzi wa mwaka wa pili wa Kozi ya Mawasiliano kwa Umma katika Chuo Kikuu cha Serikali cha Enugu.

  Ingawa wamejipatia mafanikio makubwa katika tasnia ya filamu, lakini magwiji hao wa vichekesho wamebaini changamoto mbalimbali zinazowakabili wao na dunia kwa ujumla na hivyo kuamua kuongeza viwango vyao vya elimu.

  “Nilizaliwa katika familia ya Mzee Michael Ikedieze Ogbonna. Nimekulia katika kijiji cha Iluoma Nzeakoli ndani ya eneo la Bende katika Jimbo la Abia. Baada ya kuhitimu elimu ya msingi na sekondari , niliendelea na elimu ya juu katika Taasisi ya IMT Enugu, ambako nilihitimu kozi ya Mawasiliano kwa Umma.

  “Uigizaji ni kipaji nilichopewa na Mungu tangu nikiwa mtoto. Kwa mfano nikiwa sekondari nilikuwa mwanachama wa kikundi cha sanaa na uigizaji cha shule. Nafasi muhimu ilijitokeza wakati nikiwa mwaka wa kwanza Chuo cha IMT, Agosti mwaka 1998, siku ambayo nilikutana na rafiki ambaye nilimfahamisha kuhusu lengo langu la kuwa muigizaji.

  “Nilipomwambia kuhusu hilo na kwamba napenda kuona siku moja ninashiriki katika uigizaji wa filamu zinazozalishwa nchini mwangu Nigeria, aliniahidi kunichukua kesho yake hadi katika Hoteli ya Ogui hapa katika mji wa Enugu, ambako kulikuwa na tamasha la kuwasaka wasanii nyota ili kutengeneza filamu ya ‘Evil Men’. Waandaaji waliniona na kunichagua kuingia kushiriki katika filamu ile, hapo ndipo nilipoanzia,” anasema Aki.

  Jamii inazitazama vipi filamu zao?

  Kasheshe kubwa ilizuka hivi karibuni pale baadhi ya wazazi wa nchini Nigeria walipotishia kuzipiga marufuku filamu zilizochezwa na Aki na Ukwa kwa madai kuwa, zinatoa mafundisho mabaya kwa watoto wao.

  Wazazi hao wanasema, filamu nyingi zinazochezwa na waigizaji hao zinaonesha dharau kwa watu wazima na kuwafundisha wizi vijana. “Vijana wengi wamekuwa wakiiga matukio yanayofanywa na Aki na Ukwa kwenye filamu wanazocheza, hivyo kuathirika,” amesema mmoja wa wazazi hao, aliyehojiwa na mtandao wa Nigeriafilms.

  Mzazi mwingine anasema, matukio ya wizi yamekuwa yakiongezeka ikilinganishwa na miaka ya nyuma, wahusika wakuu wakiwa vijana wa umri mdogo kutokana na kuiga tabia za wacheza filamu hao.

  Wazazi hao wamedai kuwa, vijana wengi wa umri mdogo nchini Nigeria wanapenda kuishi maisha yanayofanana na yale ya Aki na Ukwa bila kujua kuwa ni ya uigizaji.

  Baadhi ya wazazi wamehoji ni kwa nini filamu zote wanazoshiriki kucheza vijana hao, zinaonesha vitendo vya uovu katika jamii badala ya mafundisho mema. “Kama huoneshi matendo mazuri kwa vijana wako nyumbani, lazima watakuiga,”anasema mmoja wa wazazi hao.

  Mzazi huyo anasema wanawapa changamoto waandaaji wa filamu wa Nollywood, kubadili mwelekeo kwa kuandaa sinema, ambazo haziwezi kuathiri maisha ya vijana wao. “Wanapaswa kutengeneza filamu zenye mwelekeo chanya. Vijana ni wepesi wa kuiga na wakifanya hivyo, wanaonesha picha mbaya ya Wanigeria,” anaongeza.

  Hata hivyo harusi ya Aki inaelezwa kwamba itamaliza kabisa hisia mbaya za wazazi wa Nigeria kwamba waigizaji hao si kioo kizuri kwa jamii kutokana na visa na mikasa ikiwemo ya usaliti katika mapenzi wanayoiigiza katika filamu zao.

  Ndoa ya Aki inatajwa kuwa mfano wa kuigwa ambao utaibua mwanzo wa mapinduzi mapya ya fikra za vijana wa Nigeria kuhusu ndoa na familia kwa ujumla katika misingi ya kuheshimu mila, desturi na Mungu.

  Huyo ndiye muigizaji Aki ambaye ameiaga rasmi kambi ya ukapera kwa kumuoa mrembo mbichi, Nneoma baada ya miaka mingi ya tabu, shida, mateso, na kero za mapenzi.
   
 2. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #2
  Jan 18, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  hadithi ni ndefu mno
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Jan 18, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,514
  Likes Received: 19,933
  Trophy Points: 280
  mwandishi unapoteza mda wako kuandika habari ndefu hivi kuhusu akwi...?lolllz
   
 4. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #4
  Jan 18, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  safi sana kijana ossita iheme,karibu ktk chama chetu

  tutakupa ushauri jinsi gani uishi na mkeo

  kwanza tambua kuwa ndoa ni ndoano,ukisha ingia hutoki na ukitoka unamatatizo,uvumilivu ktk ndoa ni jambo kubwa sana na ndilo lenye kuleta mifarakano

  haya mleta mada mpeleke huo ujumbe bwana iheme
   
 5. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #5
  Jan 18, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  penzi ni upofu, na kipenda roho hula nyama mbichi.
  Ila kama Isostacy theorem ina-hold hapo kazi ipo

  happy for them!
   
 6. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #6
  Jan 18, 2012
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,500
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160
  Thank you for the news!!!!
   
 7. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #7
  Jan 18, 2012
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  aki akileta fujo anabebwa tu juu juu na wife.
   
 8. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #8
  Jan 18, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  na mabusu je?
   
 9. Wang'wise

  Wang'wise JF-Expert Member

  #9
  Jan 19, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 273
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hata sijasoma, ila nimeunda idea kutoka kwenye Kichwa cha habari.
  Tooo loooong
   
 10. u

  utantambua JF-Expert Member

  #10
  Jan 19, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,373
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ndivyo na wanasheria wetu wanavyofanyaga wakienda kusaini mikataba nje na wawekezaji. Hawapendi kupoteza muda kusoma makabrasha yenye kurasa kibao
   
 11. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #11
  Jan 19, 2012
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,980
  Likes Received: 6,628
  Trophy Points: 280
  nina usingizi ntaimalizia kesho. nikumbusheni nmeishia hapo $30,000. mia
   
 12. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #12
  Jan 19, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,129
  Trophy Points: 280
  Watanzania wavivu sana. Kuna mwalimu nilipokuwa chuoni alikuwa anasema kwamba, ukitaka kumpoteza mTZ we mwekee tangazo kwa maandishi. Na ndio maana kuna majina yalikuwa yanatolewa kwa ajili ya kusaini loan ila kwa kuwa yalikuwa yanabandikwa, kuna watu mpaka siku zinaisha anakuwa hana taarifa kisa uvivu wa kusoma.
   
 13. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #13
  Jan 19, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  mbona hujaweka picha ya mkewe?
   
 14. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #14
  Jan 19, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,261
  Trophy Points: 280
  Acheni uvivu wa kusoma, hata browsing tu!
  Well, huyo mtoto wa 20 yrs kakubali mshiko hapo! Na hata wazazi wake nao wamekubali for same reason! Ukiwa na madolari unakuwa handsome tu! Nimefurahi walau wamesoma, nikaanza kuwawaza mahandsome wetu wa skirini.
   
 15. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #15
  Jan 19, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Pesa bwana, akishtuka mbilikimo apigwa chini
   
 16. Zabibu

  Zabibu JF-Expert Member

  #16
  Jan 19, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Aliyeoa anaitwa CHINEDU IKEDIEZE (aki) na sio ossita iheme(ukwa)

  CH4.jpg
   
 17. c

  christer Senior Member

  #17
  Jan 19, 2012
  Joined: Feb 12, 2010
  Messages: 131
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  unaonaje ukibadili avator?
   
 18. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #18
  Jan 19, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,635
  Likes Received: 1,994
  Trophy Points: 280
  nimependa jambo moja,elimu ya 'mzee'Aki....elimu huondoa ukungu mawazoni.
   
 19. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #19
  Jan 24, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  U are wellcome
   
 20. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #20
  Jan 24, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Umeona eee???
   
Loading...