Akaunti ya Escrow yafichua mazito

Akaunti ya Escrow yafichua mazito

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,247
Reaction score
25,191

WAKATI Bunge likijiandaa kusomewa ripoti ya uchunguzi wa Akaunti ya Escrow bungeni Mjini Dodoma, ripoti hiyo imezidi kuwapasua vichwa wabunge baadhi yao wakienda mbali zaidi na kudai wamebaini ukweli wa fedha hizo.

Hatua hiyo inatokana na taarifa zinazodai malipo ambayo yanalalamikiwa kufanywa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kupitia Kampuni ya Independet Power Supply Limited (IPTL), yalikuwa halali si ya fedha za umma.

Taarifa zaidi kutoka kwa baadhi ya wabunge wanaodai kupata yaliyomo kwenye ripoti hiyo kuhusiana na malipo hayo, zinasema wabunge wengi wamefahamu ukweli na kinachofanyika ndani ya Bunge ni kupotosha ukweli kwa maslahi ya wachache.

Wakizungumza na gazeti hili, mmoja wa wabunge hao ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, alisema kinachoweza kufanyika sasa ndani ya Bunge ni uonevu kwa kuwa BoT ililipa malipo halali kwa IPTL na taarifa ziko wazi.

“Nimeipata ripoti ya CAG na taarifa zingine, nimezisoma kwa umakini mkubwa na kubaini kilichopo ni vita ya madaraka, kuna wakati tunafuatwa na watu ili tuwawajibishe viongozi hasa Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo,” alisema.

Alidai kuna baadhi ya wabunge ambao wamejiridhisha kuwa malipo hayo yalilipwa ili kutekeleza makubaliano kati ya IPTL na Serikali ambapo BoT ilichaguliwa kama wakala wa kutunza fedha.

Alisema hali hiyo ilitokana na uwepo wa mgogoro wa kimaslahi kati ya wabia wa IPTL ambao ni kampuni ya VIP (ilikuwa inamiliki asilimia 30 ya hisa) inayomilikiwa na James Rugemalila na kampuni ya Mechmar kutoka Malaysia (ilikuwa inamiliki asilimia 70).

Mbunge huyo alisema taarifa zinaonyesha kwamba Mahakama Kuu iliamua pande zote mbili VIP na Mechmar zisaini hati ya makubaliano (MoU) juu ya kutunza fedha za malipo ya kila mwezi ya umeme, ambayo IPTL inauzia TANESCO.

Aliongeza kuwa, nyaraka zinaonesha mahakama ilielekeza malipo hayo yahifadhiwe katika akaunti maalumu hadi mgogoro utakapoamriwa kati ya wabia hao ambao walikubaliana kufungua akaunti ya pamoja BoT na akaunti hiyo kuitwa Escrow.

“Ukitazama kwa umakini, kinachofanywa ni kumuonea Pinda kwa sababu ya upole wake, kuna watu wanaamini atagombea urais hivyo wanataka kumharibia,” alisema mbunge mmoja kutoka mkoani Morogoro.

Mbunge mwingine kutoka Dodoma, alisema ukisoma taarifa za Escrow, zinaonesha wazi kuwa BoT ilikuwa wakala wa kutunza fedha hizo ambapo TANESCO na Serikali walisaini hati kama sehemu ya wabia wakiwa walipaji wa umeme kwa IPTL.

Kwa mujibu wa nyaraka hizo, ambazo gazeti hili iliziona zinaonesha makubaliano hayo yalifikiwa Julai 5, 2006 na kila upande uliwakilishwa na wahusika, kutia saini ambapo kwa upande wa Serikali alisaini aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara wakati huo, Arthur Mwakapugi.

Taarifa hiyo ilionyesha kwa upande wa IPTL alisaini aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Datuk Baharuden Majid na upande wa BoT, alisaini aliyekuwa Gavana Mkuu, marehemu Daudi Balali kama wakala wa kuhifadhi fedha hizo.

Kusainiwa kwa makubaliano hayo ikiwa ni maelekezo ya mahakama, ilielezwa kuwa mgogoro utakapoisha kati ya wabia, BoT itatoa fedha zote ilizokuwa inazihifadhi katika akaunti hiyo kwa mujibu wa hati husika ya makubaliano kwa ajili ya malipo ya uuzaji wa umeme kwa TANESCO.

Kwa upande wake, mbunge mwingine kutoka mkoani Tabora, ambaye alikuwa na mbunge mwenzake kutoka Mkoa wa Pwani, alisema ukilitazama Bunge kwa umakini limeanza kugawanyika.

“Kuna wafanyabiashara waliokosa vitalu vya gesi wamekuja na yao ndani ya Bunge ili wamwajibishe Waziri wa Nishati na madini kwa maslahi yao na wengine walikuwa wanatoa ushauri wa kisheria katika suala hili,” alisema mbunge huyo.

Aliongeza kuwa, Serikali inapaswa kuwa makini na kuhakikisha inasimama imara kuelezwa ukweli wa jambo hilo kwani anaamini kinachofanyika ndani ya bunge ni hasira za watu.

Chanzo:Majira
 
Donatila ingawaje chanzo cha habari si wewe lakini kuiweka hii habari haiwezi kubadili upepo. Watanzania sasa hivi wanataka kuona wezi walitajwa kwenye hiyo ripoti wanafukuzwa kazi na kupandishwa mahakamani kujibu mashtaka ya wizi.

Habari hii ya majira inakinzana kabisa na maelezo ya mwenyekiti wa kamati ya PAC ambayo yanaashiria kabisa kuwa kuna "suspects" kwenye taarifa za uchunguzi wa ESCROW account
 
Last edited by a moderator:
Katika hili sakata la ESCROW yatasemwa meengi sana na tusipokuwa waangalifu huenda tukafika mahali tusimjue hata tunayemtafuta
 
Majira used ni kama mmeshachelewa sana kwenye utetezi huu. Na imeshasemwa funueni tu hilo kombe kwakuwa mwanaharamu amegoma kupita.
 
Katika hili sakata la ESCROW yatasemwa meengi sana na tusipokuwa waangalifu huenda tukafika mahali tusimjue hata tunayemtafuta
Hii pesa ya Mhariri Mtendaji wa Daily News Bw Gabriel Nderumaki ambayo kampuni yake ya Capital Promotions inalipwa kufanya PR ya IPTL, kuleni, lakini ukweli utabaki vilevile. Njaa kitu kibaya sana. Sikutarajia mhariri mkuu wa gazeti kama Majira anaweza kuchapa ujinga na upuuzi kama huu. Lakini kama halipwi mshahara afanyeje?
 
Na inaonekana zile bilioni ngapi sijui zilizotengwa na serikali kwa ajili ya kupigia kampeni katiba mpya kwenye vyombo vya habari (gazeti la Majira likiwemo), sasa kuna dokezo jipya kwamba teteeni kwanza hili li escrow la Tegeta, na mtaongezwa mshiko ili kuendeleza kampeni za katiba mpya baadaye. Wala sishangai.
 
Eti mbunge mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe! Anajificha nini kama anasema ukweli? Kweli magazeti yetu nayo ya ajabu. Fedha za Escrow zinafanya kazi kweli, usije kuta kwa kuandika makala hiyo tuu mtu kalipwa milioni 40!
 
watanzania tunajazwa chuki ya ajabu ni hatari kilichoandikwa na majira ni sahihi kabisa kama inafikia fitina kwa ajiri ya kukosa kitu ni hatari au kwa kuwa kuna mtu anataka kugombea urais huyo anayefanya vitina hiyo ni kumuogopa kama ukoma huyo aliokosa gass ndie alieifirisi bank ya NBC mpaka ikauzwa chee.
kwanini mtu huyo asijadiliwe bungeni? nawaombeni wabunge msipandikizwe chuki ni hatari
 
Donatila ingawaje chanzo cha habari si wewe lakini kuiweka hii habari haiwezi kubadili upepo. Watanzania sasa hivi wanataka kuona wezi walitajwa kwenye hiyo ripoti wanafukuzwa kazi na kupandishwa mahakamani kujibu mashtaka ya wizi.

Habari hii ya majira inakinzana kabisa na maelezo ya mwenyekiti wa kamati ya PAC ambayo yanaashiria kabisa kuwa kuna "suspects" kwenye taarifa za uchunguzi wa ESCROW account

Jee, wewe umeioana hiyo ripoti hata ujuwe kuna "wezi"?
 
Matumaini yangu yapo kwako kaka Zitto na team yako ya PAC. Nyie ndio mtakaotutoa katika mtihani huu unaotaka kufunikwa kwa dhulma kabisa.
 
Last edited by a moderator:
nani alikwambia Pinda ni mpole, wapigwe tu... si lugha ya kutolewa na kiongozi mkubwa kama yeye, hana upole wowote...
 
Kuanzia sasa gazeti la #majira ni marufuku kwangu.

Mjidharirisha sana, baadae mtataka watanzania wawe wazalendo na vyao, utaachaje kununua gazeti la wakenya wanaofichua kila uozo eti ununue gazeti la majira ambalo linatetea wezi?

Ukiangalia article yenyewe yaani haina fact wenyewe ni kuruka ruka tu kama hadithi ya juma na Roza.
 
Jee, wewe umeioana hiyo ripoti hata ujuwe kuna "wezi"?

Sijaiona hiyo ripoti ila kwa kufuatilia michango ya wabunge husani mwenyekiti wa PAC naweza kunusa kilichopo kwenye taarifa ya uchunguzi FaizaFoxy
 
Last edited by a moderator:
Sijaiona hiyo ripoti ila kwa kufuatilia michango ya wabunge husani mwenyekiti wa PAC naweza kunusa kilichopo kwenye taarifa ya uchunguzi FaizaFoxy

Aaah, kumbe unanusa tu? sasa sijui tunachobishana ni nini? ripoti hujaiona unaanza kutuhumu watu, huyo Mwenyekiti wa PAC ni wapi kamtuhumu mtu? wote tumemsikiliza na alichosema ni kuwa ripoti anayo na ipo tayari na wakati wowote akiambiwa ailete bungeni ataileta, na pia amesema ni vyema ikiletwa kwani matusi ya kila aina yamekuwa mengi.

Sasa wewe kunusa kwako hakukusaidii wala hakutusaidii kitu, tutakapoiona hiyo ripoti ndipo tutakuwa na uhakika kama kuna wezi au hakuna, lakini ukweli unabaki pale pale, fedha zilizowekwa escrow toka 2006 ni za malipo halali ya huduma walizotoa IPTL na PAP, na PAP wamesema na kutangaza kuanzia awali kuwa kama IPTL ilikuwa inadaiwa, madeni hayo yote sasa hivi ni yamehamia kwao.

isitoshe, PAP bado wanatoa huduma, mitambo ipo Tanzania, mizima na inazalisha na sidhani kama issue hapa ni wizi.

Kwa mujibu wa habari tunazozisoma kila siku, nnachokiona kwa sasa ni kuwa kuna watu wanaotafuta umaarufu wa kisiasa kuelekea uchaguzi, kuna wengine wamekasirishwa kukosa ulaji kwenye makesi yasioisha, kuna wengine wanaotaka PAP ifunge mitambo ili waweke ya wanaowawakilisha ili waendeleze ulaji, kuna wengine wametofautiana kwa kukoseshwa udalali na wao wanachangia huu uonekane ni mgogoro.

Sijui unaelewa hayo?

Think.
 
Back
Top Bottom